Uchaguzi 2020 Watia nia waitwa kusaidia kampeni. Watumishi watia nia wapo hoi kiuchumi

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
275
802
Ni kawaida kwa watia nia wa ubunge na udiwani ambao hawakuteuliwa kuitwa majimboni kusaidia kampeni za wagombea wa CCM kuanzia Urais, Ubunge na Udiwani.

Baadhi wameitikia wito huu. Kimbembe sasa kipo kwa watumishi wa umma ambao huu ni mwezi wa pili hawajalipwa mishahara yao.

Taarifa zinasema, wengi wa watia nia hawa wanaweza kushindwa kuhushuria kampeni hizo kwa sababu ya ukata na ugumu wa kupewa ruhusa kwa miezi mingine miwili ya kampeni. Kwani maelekezo ya waraka ni kuwa hawatalipwa mishahara ya mwezi wa 7 na 8.

Lakini, kwa upande mwingine watumishi hawa wasioteuliwa wapo kwenye uangalizi kama kweli walikuwa na nia ya kukipigania chama, basi huu ni wakati muhimu wa kukifanyia kampeni chama hicho
 
Mtumishi wa umma ukiudhuria na kushiriki kampeni za uchaguzi mkuu unakatwa Tena mshahara wa mwezi September,ukumbuke waliokatwa mishahara ya July na August 2020.
 
Mi kuna mmoja namdai mwezi sasa hata kupokea cm hapokei,kweli magu kiboko kawanyosha wakanyoka, lisu alitabiri siku nyingi kuwa hakuna alie salama kila mtu ataguswa.
 
Back
Top Bottom