Watetezi wa 'scorpion' walikurupuka

Watetezi wa 'scorpion' walikurupuka

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,828
Reaction score
831,052
1476872318570.jpg

Hii mada haina mahusiano na kile kilichotokea mahakamani leo wala kile kinachosemwa semwa kuhusu yule mhanga wa tukio husika. Hii ni kujaribu kuchambua kwa undani zaidi kile kitendo cha kumng'oa mtu macho na wale watetezi kusema kuwa mtuhumiwa ni mtu mzuri mcheshi na mshika dini sana kiasi kwamba hawezi kufanya hivyo.

Kuna mengi hayakuzingatiwa kwenye huo utetezi, hii ni kawaida kwakuwa nia ilikuwa ni kutetea hasa kutokana na hao watetezi jinsi walivyomfahamu mtuhumiwa na kufanya naye kazi. Mtu mbaya hawezi kuwa mbaya kwa wote na mtu mwema pia hawezi kuwa mwema kwa wote hata kama angekuwa mpole kama hua kuna degree za vichokoo vya kihisia huweza kumfanya abadilike na kuwa mtu mwingine kabisa ndani ya dakika moja.

Moyo wa mtu ni kiza kinene!ni ngumu kujua kilichomo ndani ya giza.

1476873019392.jpg

Dhana ya kuwa mtu mwema mpole na mcheshi haiondoi ile roho ya kinyama aliyonayo binadamu yoyote yule. Huyu mtuhumiwa kwa jina la utani la scorpion au Nge tayari alikuwa na degree za vichokoo hasi mwilini tangu udogoni alipokuwa anaonewa na wengine! Vichokoo na vichocheo hasi hivyo vilimfanya mpaka akaamua kuingia kwenye kufanya mazoezi makali sana ya mapigano na ulinzi binafsi na kwa maneno yake alishawahi kumshikisha mbaya wake adabu kwa kipigo kitakatifu! Hii ni roho ya kisasi yenye viashiria vya ukatili.

Kigezo cha kushika dini

Kiasili dini ililetwa kuwa daraja kati ya Mungu na wanadamu, ilichukuliwa kama kitu chema sana lakini ni kupitia dini hiyo hiyo imepoteza watu kwa maelfu! Dini imetumika kuua na kufanya mambo mabaya kabisa katika jamii.

Mifano ipo mingi na mfano wa hivi karibuni kabisa ni ule wa Dodoma yule aliyesababisha mauti ya wale watafiti! Washika dini wamegeuka kuwa watu wa kuogopwa siku hizi si kwa imani zao bali matendo yao.

Huyu bwana alikuwa mfanya mazoezi makali ya mapigano hasa karate na boxing! Wacheza karate na boxing ni wakorofi tofauti na wacheza kung fu na tai chi...sababu ni moja kwamba karate na boxing zinatumia nguvu za mwili wakati kung fu na tai chi vinatumia vital power nguvu ya ndani.

Bila kujali unajifunza kipi kati ya hivyo ni lazima upate kujifunza na masomo ya darasani pia kuhusiana na mojawapo ya hilo na somo muhimu ni humanity loving kindness na compassion (ubinadamu upendo na huruma). Usipojifunza ukayaelewa haya vizuri ukakimbilia tu kwenye mazoezi athari zake ni kutaka kuonyesha ubabe wako hata kwa wasiostahili.

Wengi wa wanamichezo wetu kwenye hii field wanakosa elimu hiyo ya darasani ndio maana wanakuwa wakorofi na ubabe mwingi. Kwahiyo huyu mtuhumiwa alikuwa na dalili zote na viashiria vyote vya kufanya kile kinachosemekana amekifanya! Ana mazoezi ya kutosha jinsi ya kukaba jinsi ya kutoboa macho nk nk lakini hana pa kujaribia! Mikono inawasha kikitokea kisababishi chochote lazima vile vichokoo hasi viamrishe mwili ufanye kazi.

Nimeongea kwa muktadha wa ujumla kutokana na kile kilichotokea
 
Naweza nikasimama kumlaumu "mtoa macho" lakini lililo bayana kitendo alichofanya ni ishala ya wazi kuonyesha sura halisi ya jamii yetu.

Jamii ya watu wasiofikiri kwa mantiki na maamuzi yao kuongozwa na "hisia" zaidi.

Tumeona jinsi watanzania wenzetu walivyong'oa viti kwenye uwanja mkuu, tumeona jinsi mwamuzi "alivyovunjiwa" heshima kule Tanga,tumeona jinsi wataalam wetu walivyopoteza maisha kule Dodoma.

Tuna Tatizo kubwa kijamii. Ni wakati muafaka wa kujielekeza kwenye tafiti za kisanyansi ili tuje na majawabu.
 
Ila ana moyo mgumu aiseee duuuuu! yaani unamtoboa mwenzio macho yanamwaga maji unatoboa unatoboa unatoboaaaaa uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kwenye vitabu vitakatifu vinaelekeza mwizi hua anakatwa mkono,mzinzi hua anapondwa mawe hadi kufa,hivyo ni vitabu vya dini uswahilini mwizi hua anapigwa na kuchomwa moto,muhanga wa macho alikua mfadhili wa wezi hivyo na yeye ni mwizi
Hili linasemwa lakini sijajua ukweli wake japo kidogo umetoka nje ya kiini cha mada
 
Naweza nikasimama kumlaumu "mtoa macho" lakini lililo bayana kitendo alichofanya ni ishala ya wazi kuonyesha sura halisi ya jamii yetu.

Jamii ya watu wasiofikiri kwa mantiki na maamuzi yao kuongozwa na "hisia" zaidi.

Tumeona jinsi watanzania wenzetu walivyong'oa viti kwenye uwanja mkuu, tumeona jinsi mwamuzi "alivyovunjiwa" heshima kule Tanga,tumeona jinsi wataalam wetu walivyopoteza maisha kule Dodoma.

Tuna Tatizo kubwa kijamii. Ni wakati muafaka wa kujielekeza kwenye tafiti za kisanyansi ili tuje na majawabu.
Hii yote ni kiashiria cha tatizo kubwa lililojificha ndani ya jamii yetu ambalo aidha halijapewa umuhimu au linaonekana si tatizo kabisa
 
Hii yote ni kiashiria cha tatizo kubwa lililojificha ndani ya jamii yetu ambalo aidha halijapewa umuhimu au linaonekana si tatizo kabisa
Dar hapafai kabisa
mm niliporwa mzigo wa bidhaa za dukani na wabeba mizigo maeneo ya Kariakoo
nimembebesha kijana (kuli) box maeneo ya Kariakoo na Congo yeye akaniambia nitangulie kwani watu wengi wanamzuia kupita mm kwa ubabe na kelele nikasafisha njia hatua 10 nageuka HAYUPO na box silioni
nawauliza wote wakazi wa ule mtaa eti wananiambia HAWAJAMUONA binadamu aliyebeba box nikarudi mpaka duka la mwisho, kweli walinicheka, nikaenda shtaki Kituo cha POLISI Msimbazi nako wakanitumbulia macho.
Leo namkumbuka mbabe km Scirpion aongezeke vibaka waishe la sivyo Dar siji lada nijenge mwili
 
Pole kaka shemeji zangu walipigwa mzigo toroli zima kwa style hiyo! Huu mji huu Mungu anauona
 
Dar hapafai kabisa
mm niliporwa mzigo wa bidhaa za dukani na wabeba mizigo maeneo ya Kariakoo
nimembebesha kijana (kuli) box maeneo ya Kariakoo na Congo yeye akaniambia nitangulie kwani watu wengi wanamzuia kupita mm kwa ubabe na kelele nikasafisha njia hatua 10 nageuka HAYUPO na box silioni
nawauliza wote wakazi wa ule mtaa eti wananiambia HAWAJAMUONA binadamu aliyebeba box nikarudi mpaka duka la mwisho, kweli walinicheka, nikaenda shtaki Kituo cha POLISI Msimbazi nako wakanitumbulia macho.
Leo namkumbuka mbabe km Scirpion aongezeke vibaka waishe la sivyo Dar siji lada nijenge mwili

Ukwaju;
Daah! Pole mkuu, yalikufika hayo!! Najiwazia tu, ulivyo fadhaika ulipojikuta unatumbua mimacho bila kujifaham yalokupata. Fikiri, ukute hela yenyewe umekopa ka mtaji, sasa umebaki na risiti zisizokusaidia. Najiuliza, hivi ulipokuwa waenda panda basi lako kujirudia home labda Manerumengo, ungelimkuta kibaka anashughulikiwa na wenye hasira kali; Nawaza tu, angelikuangukia miguuni kuwa, nisaidie kaka nauawa!! Ungeanzia wapi kumchuna ngozi?? Ni mawazo tu!
Wababe hawatasaidia, huruma ndo itasaidia. Ukimhurumia, akitaka kuiba tena, dhamira itamsuta.
 
Scorpion ni wakupewa zawadi.sema nchi hii inafuata sheria basi tu.

Mtu anayekupenda na kukutakia mema siku zote huwa anakupa muda wa kurekebisha uripoharibu.
 
Kwenye vitabu vitakatifu vinaelekeza mwizi hua anakatwa mkono,mzinzi hua anapondwa mawe hadi kufa,hivyo ni vitabu vya dini uswahilini mwizi hua anapigwa na kuchomwa moto,muhanga wa macho alikua mfadhili wa wezi hivyo na yeye ni mwizi

Una uhakika,,au jamaa kupewa bajaj mbili na pikipiki tano na nyumba roho zimewauma kenge nyinyi,,, MNASHINDWA KUTAMBUA THAMANI YA MACHO NI ZAIDI YA ALIVYOPEWA,,hata kama alikuwa mfadhili wa vibaka,ndio ilikuwa ni haki atobolewe macho,,,acheni roho za kwann
 
Back
Top Bottom