G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Kumekuwa na taarifa kuwa viongozi na watendaji wakuu wa ACT Wazalendo wanapewa nafasi za kiutendaji huku wao wenyewe wakiwa tayari kutumikia nafasi hizo na kuahidi ushirikiano kwa rais Magufuli bila hata ya kiongozi wao mkuu ndugu Zitto Kabwe kupewa taarifa za awali.
Pia rais Magufuli anakosea sana kuwasiliana na viongozi wa ACT Wazalendo na hatimaye kuwapa nyadhifa mbalimbali za kiutendaji bila hata ya kuomba ushauri na mapendekezo kwa kiongozi mkuu wa chama hicho ndugu Zitto Kabwe.
Kumteua mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho kinapinga sera za chama tawala kwenda kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala na kupokea maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa mwenyekiti mwenzake wa chama kingine cha siasa ni kitendo cha kudhoofisha siasa za vyama. Rais Magufuli ameonyesha kuwa ACT Wazalendo sii chochote mbele yake na ndiyo maana anajichagulia tu anayemtaka ndani ya chama hicho. Huu ni mtego ambao rais Magufuli anautumia kufuta demokrasia ya vyama vingi nchini. Hivi kweli inaingia akilini kwa mwenyekiti wa chama cha upinzani kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa na hatimaye akasimamie na kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama tawala ili kukizidishia sifa chama hicho? Mwenyekiti huyo wa chama cha siasa ni pandikizi? Chama cha upinzani kinakuwa na mwenyekiti pandikizi!
Naamini kuwa hata Zitto anaelewa kuwa mama Mghwira hakustahili hata kusubiri kamati kuu ili wajadili uteuzi huo. Alitakiwa kuukataa palepale kutokana na hali halisi ilivyo.