Watendaji wakuu wa ACT Wazalendo mnachomfanyia Zitto Kabwe siyo kitu kizuri, Pia Magufuli anakosea

Zipo tetesi kwamba hata yeye alitakiwa apewe uwaziri , mgogoro umetokea kwa vile anataka wizara ya fedha , sasa ccm imekuja juu , lakini mazungumzo bado yanaendelea .

Nitamwaga mboga hapa hapa jf kwa kadiri nzi wangu atakavyokuwa ananipa taarifa .
Lete Lete mkuu tujue wasaliti na wanao kwamisha juhudi za wapinzani wa kweli
 
Pia rais Magufuli anakosea sana kuwasiliana na viongozi wa ACT Wazalendo na hatimaye kuwapa nyadhifa mbalimbali za kiutendaji bila hata ya kuomba ushauri na mapendekezo kwa kiongozi mkuu wa chama hicho ndugu Zitto Kabwe.



Kumteua mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho kinapinga sera za chama tawala kwenda kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala na kupokea maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa mwenyekiti mwenzake wa chama kingine cha siasa ni kitendo cha kudhoofisha siasa za vyama."



Endelea kupopoma!
 
Kumekuwa na taarifa kuwa viongozi na watendaji wakuu wa ACT Wazalendo wanapewa nafasi za kiutendaji huku wao wenyewe wakiwa tayari kutumikia nafasi hizo na kuahidi ushirikiano kwa rais Magufuli bila hata ya kiongozi wao mkuu ndugu Zitto Kabwe kupewa taarifa za awali.

Pia rais Magufuli anakosea sana kuwasiliana na viongozi wa ACT Wazalendo na hatimaye kuwapa nyadhifa mbalimbali za kiutendaji bila hata ya kuomba ushauri na mapendekezo kwa kiongozi mkuu wa chama hicho ndugu Zitto Kabwe.

Kumteua mwenyekiti wa chama cha siasa ambacho kinapinga sera za chama tawala kwenda kuwa msimamizi mkuu wa ilani ya chama tawala na kupokea maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa mwenyekiti mwenzake wa chama kingine cha siasa ni kitendo cha kudhoofisha siasa za vyama. Rais Magufuli ameonyesha kuwa ACT Wazalendo sii chochote mbele yake na ndiyo maana anajichagulia tu anayemtaka ndani ya chama hicho. Huu ni mtego ambao rais Magufuli anautumia kufuta demokrasia ya vyama vingi nchini. Hivi kweli inaingia akilini kwa mwenyekiti wa chama cha upinzani kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa na hatimaye akasimamie na kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama tawala ili kukizidishia sifa chama hicho? Mwenyekiti huyo wa chama cha siasa ni pandikizi? Chama cha upinzani kinakuwa na mwenyekiti pandikizi!

Naamini kuwa hata Zitto anaelewa kuwa mama Mghwira hakustahili hata kusubiri kamati kuu ili wajadili uteuzi huo. Alitakiwa kuukataa palepale kutokana na hali halisi ilivyo.
Njaa mbaya mno sioombee au kutokuwa na misimamo kwenye chama husika
 
Democrasia ya kweli haiji Tanzania kwa vile jamii imetawaliwa na unafiki ? Ukiwa na vijisent unaweza kununua utu wa watanzania wengi .

Watanzania Bara ndio wanashika bendera ukilinganisha na na visiwani, kambo hili ndio litachukua muda kuipata democrasia ya kweli Na Tanzania ku move katika uhuru wa raia kujiuna ni raia ndani ya nchi yao.
 
Mbona Mbowe kaSex na Wema Sepetu bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa Mke wake wa ndoa? Tena mtoto wa Muanzilishi wa chadema Mzee Mtei, kuna usaliti zaidi ya huo Dunia hii? Hivyo ziba kwanza Paa la nyumba yako kwanza kabla ya kuhamia kwa jirani!

ulikuepo wakati ana sex nae? au uliwaona wakati wanafanya hilo tendo la ndoa? bila shaka utakua mpiga chabo mzoezi wa kiwango cha kibashite
 
Shida ni kwa hao wanaokubali huo uteuzi, lakini pia magufuli anajijengea chuki ndani ya chama chake. Iweje awaache wanaccm kibao kwenye foleni halafu akateue wapinzani?
 
Wanaoteuliwa si wakatae? Haya namimi nakuteua na wewe kuwa Katibu kata wa kata Mkata
 
Swala la kuwaacha wanaccm sio kwamba kalipenda yeye tatizo mambo hayaendi kama inavyoyakiwa ktk uingongozi. Yeye anaona akilichagua kutoka ktk hili tawi lao dogo ilani itakelezeka kumbe ndo anazidi kujichanganya Ukitaka kulijua hili angalia teuzi zake ambazo haziishi tutaenda miaka miwili kwa Viongozi wanaojua teuzi ulitakiwa uwe umeshaisha ili timu ya watenda kazi ikamilike tutaenda wa tatu mambo atakuwa hayahaya mwisho uchaguzi umewadia. Kwa mtu aliyewahi kumskiliza Afande Selle aliyekuwa Act kuwa alichokuwa anataka Zitto na Mkumbo ktk hiki chama ni wanacha kumuunga mkono Lipumba kwa asiyejua kazi ya huyu mzee ni nani ktk siasa za hii nchi Mwenyezi Mungu akiamua kuwaonyesha ambayo tulikuwa hatujui ndo kama hivi kuchagua Viongozi kutoka ktk hili tawi ambalo Zitto kama Kiongozi anajua hili analopitia linatokea kwa sababu gani yeye baada ya kuona mambo yake hayaendi kuanzia nssf na kutochaguliwa kuwa mwenyekiti ktk awamu hii yeye akamua kuwa tofauti na yeye mwisho wa siku Zitto lazima yamkute haya hapo ndo ubaya wa kutumika kwa maslahi ya watu flani ili mambo yaende. Na hapa ndo mwisho ndo hapa atajutia kumsukia zengwe Lukas Limbu aliyemng'oa kama anachokifanya Lipumba kwa Maalim Seif kwa sasa .Siasa ni wakati ukikubali kutumika matunda yake yapo ndo haya tunayoyaona

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
mimi kinachonishangaza zaidi ni kitendo cha mama mgwira kujivua uwanachama wa act kisa kateuliwa ukuu wa mkoa. hapo sijaelewa kabisa...
 
Zipo tetesi kwamba hata yeye alitakiwa apewe uwaziri , mgogoro umetokea kwa vile anataka wizara ya fedha , sasa ccm imekuja juu , lakini mazungumzo bado yanaendelea .

Nitamwaga mboga hapa hapa jf kwa kadiri nzi wangu atakavyokuwa ananipa taarifa .
Hana ujanja wa kugoma, yule hats wakimpa uwaziri wa Kanda maalum ya Mwanza, Geita na Chato harembi, anauchukua faster tu.
 
Kuukataa ukuu wa mkoa sio jambo rahisi labda kama hujui masurufi ya mkuu wa mkoa.
 
Viongozi wote nchini wanatimiza ilani ya chama chenye dola that is CCM. Uwe mbunge, Waziri, RC, DC, mkurugenzi wote wanafanyia Kazi ilani ya CCM
Watumishi wote wa umma ndio wanatimiza ilani ila sio viongozi wote
 
Back
Top Bottom