Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,603
Watendaji wa Uchaguzi Mkuu wametakiwa kuitumia ipasavyo elimu waliyoipata katika mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi ikiwalenga waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchagyuzi ngazi ya jimbo. Rai hiyo imetolewa na mratibu wa mafunzo hayo ngazi ya Mkoa Bi Tumaini Munga akiwasilisha hotuba ya kufunga mafunzo hayo yaliyoanza tangu tarehe 21 na kutamatika leo Julai 23, akimuwakilisha Bi. Magdalena Rwebangira Mjumbe wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi.
Aidha Munga amewataka watendaji hao kuwa makini na matumizi ya mitandao ikiwemo kusambaza taarifa za tume katika makundi sogozi huku akiwataka watoe taarifa kwa vyombo vya habari pale inapobidi. Nao washiriki wa mafunzo hayo wametoa shukrani kwa tume kwa kuwawezesha kwa elimu hiyo huku wakiahidi kutekeleza ipasavyo yale yote waliyojifunza.