maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kitendo cha serikali ya Rais Kikwete kuwahamisha, kuwapangia vituo vipya na kuwateua watendaji wapya dakika za mwisho mwisho kabisa za utawala wake kulizua kelele na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wajuzi wa mambo ya utawala.
Kwa sababu hiyo, nadhani kuna uwezekano mkubwa ile ilikuwa mbinu ya kufichiana siri, kukwepa kubainika au kupiga dili dakika za mwisho.
Naomba serikali itupie macho watumishi na watendaji wote wanaoangukia kwenye sifa hii ya kuhamishwa ama kuteuliwa dakika za mwisho.
Hili likifanyika kwa weledi na kwa umakini mkubwa nina hakika itagundulika siri iliyojificha nyuma ya uteuzi ule.