Wateja wasio wastaarabu, chanzo cha customer care mbaya

Wateja wasio wastaarabu, chanzo cha customer care mbaya

Mleta mada hii si sahihi, badilisha mtazamo wako haraka sana vinginevyo utakwenda na maji. Kama huu ndio mtazamo wa Wabongo wengi, basi ndiomaana biashara nyingi Bongo zinakwama kwasababu ya mitazamo mibovu kama hii. Kwa maelezo yako inaonekana wewe ni mfanyakazi/mtoa huduma wa biashara fulani lakini si mmiliki wa biashara hiyo, kwasababu mmiliki halisi asingekuwa na mtazamo kama huu.

Kwa watu wanaojua na kuzingatia masuala ya biashara 'hakuna mteja mkorofi' bali kuna wateja wenye mahitaji tofauti au mitindo tofauti ya uhitaji kwenye biashara yako. Unahitaji kujifunza jinsi ya kuwahudumia wateja wenye mahitaji na mitindo tofauti ya uhitaji wa huduma.

Hebu jiulize, mara ngapi 'mteja huyo mkorofi ' akifika kwenye biashara yako wakati mwingine anachagua mtu fulani wa kumhudumia na si kila mtu? Kwanini? Huyu mtoa huduma aliyechaguliwa na 'mteja mkorofi' anafanya nini cha ajabu mpaka kukubaliwa na 'mteja huyu mkorofi?', ina maana mtoa huduma huyu anajua jinsi ya kushughulika na huyo ambaye wewe unamwita mkorofi.

Kitu kikubwa kwenye biashara unapaswa kujua matakwa na matarajio ya wateja wako, ukishayajua na ukikidhi matakwa na matarajio yao utakuwa umekonga roho ya mteja huyu na wengi wengine. Kama wewe ni mtoa hduma au mmiliki wa biashara unapaswa kumshukuru sana huyu unayemwita 'mteja mkorofi' kwani kitendo chake cha kulalamika kwako, chukulia kama ni 'mrejesho wa jinsi unavyotoa na kuendesha biashara yako. Unapaswa uyatumie malalamiko yake kama njia ya kuboresha biashara yako badala ya kumwoa yeye kama mkorofi.

Kama umefika mahali unawaona na unawaita wateja wako ni wakorofi, basi hapo ulipo si mahali sahihi kwako inabidi utafakari na utafute mahali pengine na fani nyingine ya kufanya maana ulipo si pako.
I'll Work on it [emoji120]
 
Mleta maada labda ungeelezea mifano ya hao wateja wakorofi ambao wanasababisha mpaka watu wengine innocent tuadhibiwe kwa kupewa customer care mbovu. Nchi hii nahisi suala la customer care liingizwe kwenye mitaala ya elimu.

Nawapongeza angalau wale mabinti/wavulana wa mitandaoni ambao hata uwatukane matusi wenyewe wanaendelea kukujibu kwa upole ili wasikupoteze hata mteja mmoja.

Angalia mifano ifuatatayo:-

√Halmashauri ukifika kulipia labda leseni utafikiri kuna vita.

√Benki mnapanga foleni masaa kadhaa wakati wafanyakazi wapo bize ndani na simu,na madirisha mengine yamefungwa na no one cares,ukiilizia labda cheque deposit,MTU anakujibu angalia paleee,halafu huyooo anasepa zake akikuacha umesimama.

√Kwenye mabaa ndio balaa zaidi. Unafika bar unakaa dk30 hakuna mwenye time na wewe, barmaids wapo bize na mabwana zao mpk uanze kupiga mamiluzi kama inaita mbwa. Sasa jichanganye uende na pisi kali aisee utanuniwa na wahudumu wote hadi na meneja.

√Hospitals kumeoza, mgonjwa anafika yupo hoi,nesi anaelekeza huku anachati tu.Jamaa yangu mmoja mkewe alizidiwa na uchungu wa ujauzito,manesi wakawa wanachart zao tu,wanamwambia ampeleke labour,kumfikisha akajifungua yy mwenyewe,jamaa yangu akaenda kutembeza kichapo kwa manesi ndio akapata huduma na baadae wakamuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom