Hakuna Taifa lolote duniani lililowahi kuua upinzani kwa kutumia vyombo vya dola kama anavyotaka kufanya Bwana mkubwa wetu.
Kama kweli yeye anaamini yeye ni Rais wa wanyonge kama anavyojinadi na amekuwa wakati wote akipigania maslahi ya Taifa letu.
Sasa ni kitu gani kinachomfanya aogope kupambana kwa hoja na wapinzani majukwaani na wananchi ndiyo waamue MCHELE upi na PUMBA
ipi?
Kwani yeye Mkulu haujui ule msemo unaosema kuwa kizuri chajiuza na kubaya chajitembeza?
Kama kweli wapinzani wameishiwa Sera za kuwaeleza watanzania , awaache WAJITEMBEZE na yeye na CCM yake WAJIUZE na wawaachie wananchi waamue mchele upi na pumba ipi......