Watawala wetu wachafu wanavyopenda utukufu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watawala wetu wachafu wanavyopenda utukufu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Apr 24, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [h=3]Chanzo: Freethinking Unabii (mpayukaji blog)[/h]

  [​IMG]
  Ethel Mutharika Mausoleum Thylo Malawi

  Jiulize ni mamilioni mangapi ya kwacha hata dola yameteketezwa kwenye kujenga jumba hili ambamo amezikwa rais wa zamani wa Malawi Bingu wa Mutharika? Zidi kujiuliza: ni pesa kiasi gani imeshaunguzwa nchini Kenya kuhifadhi mwili wa rais wa kwanza wa nchi hiyo Mzee Jomo Kenyatta tangu afariki mwaka 1978? Jiulize ni pesa kiasi gani ilteketea kwenye kujenga mji wa Gbadolite kijijini kwa mwizi wa zamani wa DRC Joseph Desire Mobutu au kanisa kubwa (kuliko la Mt. Petro la Roma) huko Yamoussoukro kijini mwa rais wa kwanza wa nchi ya Ivory Coast , Felix-Houphet Boigny na upuuzi mwingine mwingi uliotapakaa barani Afrika? Hakika watawala wetu wachafu wanapenda utukufu kwa utukutu wao na ujambazi wao.
  [​IMG]
  Baadhi ya majengo katika kijiji cha Gbadolite huko DRC yaliyojengwa na Mobutu na yasikaliwe na watu.

  [​IMG]KKanisa kubwa la Yamoussoukro huko Ivory Coast.
   
Loading...