Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,520
- 41,034
Marais wote wa Tanzania, nyakati zote, wamefanana kwa jambo moja kubwa, KUDIDIMIZA NA KUUA DEMOKRASIA.
Wakati wa mkoloni, kulikuwa na vyama vingi vya kisiasa. Mwingereza, pamoja na kwamba alikuwa mkoloni, hakuwahi kufuta au kuzuia shughuli za vyama vya siasa. Ndiyo maana kulikuwa na chama cha TAA (Tanganyika African Association).
Baada ya kupata uhuru, tofauti na matarajio ya walio wengi kuwa uhuru na demokrasia vingeongezeka, Mwalimu Nyerere aliharamisha uwepo wa vyama vingine vyote vya siasa isipokuwa chama chake cha TANU.
Tuliendelea na mfumo wa chama kimoja mpaka mabeberu walipozidisha mbinyo dhidi ya nchi zote zisizoheshimu demokrasia, ikiwemo demokrasia ya vyama vingi.
Mwalimu akaelekeza kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. Lakini, kiuhalisia ulikuwa ni mfumo wa vyama vingi bandia. Vikosi vya jeshi vikageuzwa kuwa matawi ya CCM, na wakuu wa vikosi wakawa ndio wenyeviti wa matawi ya CCM jeshini.
Taasisi za Elimu ya juu zikafanywa kuwa matawi ya CCM, na kila mahali pa kazi palilazimishwa kuanzishwa tawi la CCM. Chini ya mfumo huo, kitu chochote cha CCM pamoja na michango vikafanywa kuwa ni lazima kwa watu wote.
Hata kujiunga chuo kikuu ulitakiwa kuwa na kadi ya CCM.
Mrema alipogombea Urais kupitia NCCR, ndipo ilipojulikana kuwa hatukuwa na mfumo wa vyama vingi, bali ni kiinimacho cha kuwahadaa mabeberu.
Kwa kutumia makada wake waliopo Polisi, CCM iliwatandika virungu waliokuwa wanamshabikia Mrema, mpaka Mwalimu Nyerere akapiga kelele kukemea. Wakati huo Mwalimu akiwa amestaafu, na Mwinyi ndiye Rais.
Mkapa alipokuwa Rais, naye hakuiacha agenda kuu ya watawala ya kuhakikisha Tanzania hatuwi na demokrasia ya kweli. Wizi wa kura ikawa jambo la kawaida. Kule Zanzibar wananchi walipotaka kuandamana kupinga wizi wa kura za Hayati Maalim Seif, walikutana na risasi za moto, watu takribani 20 wakapoteza maisha.
Kikwete alipoingia akaja na staili ya kuuma na kupuliza. Kelele za kutaka katiba mpya zilipozidi, akaunda Tume, akatengeneza Bunge la katiba, lakini lengo siyo kupata katiba mpya, ilikuwa ni kufifisha jitihada za kudai katiba.
Mwishoni wakaamua kuyaondoa yale yote yaliyo muhimu waliyoyataka Wananchi, wakijua wapinzani watachukia, ikawa hivyo, lengo likatimia, muda wa uchaguzi ukafika, uchaguzi ukafanyika bila ya katiba mpya, bila ya Tume huru ya Uchaguzi, wizi wa kura ukafanyika kama ilivyo desturi ya CCM ya nyakati zote.
Yeye naye akafanya mauaji kwenye mikutano ya wapinzani ili watu waogope kuhudhuria mikutano ya vyama vya upinzani. Waliuawa watu Arusha, Morogoro, Geita na Iringa.
Akaja Magufuli, yeye hakutaka mbinu zile za kuzunguka, akaja moja kwa moja, hakuna cha kuuma wala kupuliza, msimamo akauweka wazi kuwa CCM haitaki katiba mpya, haitaki Tume huru ya Uchaguzi, haitaki Bunge wala haitaki mahakama.
Na akasema atahakikisha anaua vyama vyote vya siasa vya upinzani, na aliishi katika hilo. Wapinzani vidomodomo waliuawa au kupotezwa. Wengine kuwatandika rusasi mchana kweupe. Ikawa kabla hayatekeleza kikamilifu lengo lake la kuua vyama vya upinzani, akafa yeye, vyama vya upinzani akiviacha bado vipo, licha ya udikteta wote aliovifanyia.
Akaja Rais Samia, yeye akapokea ushauri, anaendesha utawala wake kwa mbinu za Kikwete, za kuuma na kupuliza, lakini anahakikisha hatoki kwenye lengo kuu la watawala wa CCM, la kuhakikisha Tanzania HAIPATI DEMOKRASIA YA KWELI. Jiulize mpaka leo hii:
1) Magufuli alikataa suala la katiba mpya, Samia ameleta katiba mpya? HAPANA. Anatumia mbinu ile ile ya Kikwete, kuunda kamati, mpaka utafika wakati wa uchaguzi, atakuwa anaongelea tu masuala ya mapendekezo ya kamati.
2) Magufuli hakushughulika kabisa na kuweka utaratibu wa kuhakikisha kuna uchaguzi wa kidemokrasia. Alimpachika mamluki wake kuhakikisha anapokea maagizo toka kwake, ya juu ya nani awe mbunge wapi, nani asiwe. Tangu Samia amekuwa Rais, amemwondoa Mahera?
Au amesimamia utaratibu wa kupata Tume huru ya uchaguzi? HAPANA. Anatumia style ya Kikwete, ya kuuma na kupuliza, ameunda kamati ambayo haina maendeleo yoyote. Ukifika wakati wa uchaguzi atamwelekeza Mahera, wape wapinzani, labda wabunge hamsini ili wakisema hakuna demokrasia, tutawauliza hao 50 wamepatikanaje?
3) Marehemu Magufuli alilitumia sana Jeshi la Polisi kugandamiza haki za wananchi. Rais Samia amebadilisha sheria yoyote inayosimamia utendaji wa haki na weledi wa jeshi la Polisi? HAPANA. Ameacha vile vile ili liendelee kutumika kisiasa, kuwagandamiza washindani wa CCM.
4) Marehemu Magufuli alianzisha sheria mbaya kabisa za vyombo vya habari ili kuua uhuru wa maoni.; sheria ya mitandao ili watu wasihoji chochote; na sheria ya hovyo kabisa ya vyama vya siasa ili aweze kuvifuta vyama vya upinzani kiurahisi.
Ni sheria ipi Rais Samia ameifuta katika orodha hii ya sheria gandamizi? HAKUNA. Mara chache anakemea uonevu wa Polisi lakini hagusi sheria ambayo ndiyo chimbuko la yote. Na hiyo siyo kwa bahati mbaya. Anataka kuhakikisha jeshi la polisi linaendelea kuwa chombo muhimu kabisa cha kuhakikisha NCHI HAIWI NA DEMOMRADIA YA KWELI.
5) Magufuli hakutaka mjadala na vyama vya upinzani. Samia, kwa staili ile ile ya Kikwete, ya kuwaalika wapinzani na kuwanywesha juice ikulu, amewaita mara kadhaa wapinzani ikulu, na kuonesha ukaribu. Lakini je, Rais Samia ameruhusu vyama vya siasa kufanya shughuli zake za siasa kwa mujibu wa katiba? HAPANA.
Anawavutia muda, kwa staili ile ya kupuliza na kuuma. Wapinzani watapelekwa kwa ujanja huu huu, mpaka itafika 2024, halafu wataambiwa muda ni mfupi sana, baada ya uchaguzi tutashughulikia suala la katiba.
Watanzania wamefanywa watoto wadogo, wanapozwa kwa pipi, wakati matatizo yao ya msingi yakiwa yamebakia pale pale siku zote.