Popote pale Duniani, uchaguzi ni issue nyeti sana. Lakini kwa Nchi yetu kwa sasa ni kama tumepuuza unyeti wake. Hali hii ikiachwa iendelee hivi, tunakwenda kuliangamiza Taifa hili.
Kitendo cha watawala kumkamata Tundu Lissu na kumfungulia mashtaka ambayo kimsingi hayana ukweli wowote kimeongeza chuki kubwa sana kwa Watanzania.
Kitendo hiki pia kimewafanya hata wale waliokuwa wakipuuza madai ya CHADEMA kuamini zaidi madai hayo.
Kilichopo sasa ni kwamba, wafuasi wa CHADEMA wanawachukia watawala pamoja na wafuasi wao. Huku mtaani watu wamechukia sana.
Kila aliye upande wa watawala anaonekana ni adui mkubwa katika jamii.
Chuki/hasira ya watu ikishafika kwenye kiwango cha juu kabisa cha mwisho, kinachofuata ni Nchi kuwaka moto. Moto huo ukiwaka kuuzima siyo leo, inawezekana ikapita miongo kadhaa moto huo kuuzima.
Ili tusifike huko, nitoe rai yangu kwa watawala kwamba:-
(i)Wamwachie Lissu na wafute mashtaka yake yote.
(ii)Kama kuna nia njema, watafute mpatanishi baina yao na wakae meza moja kujadili na kuondoa tofauti zao na kila mmoja awe tayari kupata na kupoteza baadhi ya mambo
Lengo tuingie kwenye uchaguzi tukiwa wamoja kuliko ilivyo sasa.
Ikumbukwe kuwa, CHADEMA ni WATANZANIA hali kadhalika CCM. Kwa hiyo, kati yao hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine. Wote wana haki sawa.
Kama watawala wetu wanaweza kusikia, basi wasikie na wafanyie kazi maoni haya.