Watawala, Binadamu Hutawaliwa na Utashi wake Mwenyewe.

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Unaweza, na ni rahisi mno kuwatawala na kuwadhibiti wanyama wakali kama simba, faru, nyati, na wengine kama hao lakini haiwi hivyo kwa binadamu!
Hata Mwenyezi Mungu aliyetuumba huwa hatushurutishi kufuata matakwa yake, bali ametupa uhuru wa kumchagua au kumkataa.
Na iwapo mtu hataki kuwa chini yako wewe; pengine kwa sababu ya miguvu uliyonayo unaweza kujaribu kumtawala kwa mabavu, ingawa hata hivyo utakuwa ukifanya kosa kubwa ukisahau kuwa bado mtu huyo yuko huru nafsini mwake na kwamba tayari ameshakukataa.
Nasema tena, binadamu ni kiumbe huru!
Huru kupenda
Huru kuchukia
Huru kukubari.
Huru kukataa.
Hebu jaribu kufikiri iwapo Muumbaji hakutaka kuutwaa Uhuru huo kutoka kwetu ni nani huyo mwenye misuri minene ya kuupora Uhuru huu?
Kujaribu kufanya hivyo ni kuifinyangia jamii madhara makubwa!
Historia ni mwalimu mzuri ambaye tukimnyenyekea atatufunza.
 
Back
Top Bottom