Elections 2010 Watanzania wenzetu walioko uingereza- washerehekee au wajutie

shilanona

Member
Oct 31, 2010
55
95
SALAAM ZA PONGEZI KWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA USHINDI WA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 2010 – 2015
----

Chama cha Mapinduzi Tawi la UK kinatuma salaam za pongezi kwako Dr. Jakaya M Kikwete kwa ushindi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu 2010 – 2015.
Wana CCM na Watanzania UK waliridhika sana nawe Dkt. Kikwete kwa uwezo wako mkubwa wa kuzielezea na kuzitetea kwa uwazi sera endelevu za CCM na pia kumudu kuwahamasisha Watanzania kuielewa na kuikubali ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010 – 2015.
Aidha awali kabla na wakati wa kampeni za kuinadi ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 – 2015 uliendelea kudhihirisha ukomavu na uzoefu wa uongozi wa kidemokrasia ndani ya chama na baina ya vyama kitaifa na mfano wa kuiga katika medani za siasa za kimataifa.
Ushindi wako ni ishara ya IMANI ya Watanzania kwako na kwa CCM. Ni matumaini yao utekelezaji wa ilani ya CCM 2010 – 2015 utaendelea kuzingatia kasi na uwezo mkubwa katika ngazi zote za utawala na uwakilishi kuanzia chini waliko wananchi wanaoathirika na kero za umasikini.
Kwa kuwa umekiongoza Chama na Serikali yake vizuri na kusajili mafanikio makubwa toka mwaka 2005 hadi 2010, kipindi hiki cha pili ni DHAMANA nyingine tena kwako na kwa CCM kuendelea kuvuna na kutumia rasilimali za Taifa letu kuongeza maendeleo na maisha bora yenye usawa kwa kila Mtanzania. Aidha kuapishwa mbele ya halaiki ya Watanzania ni MKATABA mpya na rasmi wa kuwalinda na kuwatetea Wananchi na mali zao ndani na nje ya nchi.
Kwamba utaendelea kujenga Demokrasia yenye nidhamu kama ilivyoshamiri leo Tanzania na kuimarisha Utawala Bora ambao hautamvumilia mtu awaye yote kuchochea na kuhatarisha ulinzi na usalama wa raia au kuhujumu uchumi wa taifa letu katika kiwango chochote.
Kwa kuwa wewe ni MWASISI wa ushirikishwaji wa Watanzania ughaibuni, CCM-UK inaamini utaendelea kuiongoza serikali kufungua milango ya uwezeshaji na uwekezaji na kuhamasisha asasi binafsi kushirikisha na kuvuna rasilimali za Watanzania ughaibuni kwa maendeleo ya Taifa letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MAPINDUZI DAIMA.
 

shilanona

Member
Oct 31, 2010
55
95
mbona hizi pongezi hazitoki kwa watu walio na maono ya fikra za kitanzania? Ni wapi Kikwete alijenga demokrasia tanzania? Ni wapi Kikwete amewachukulia hatua mafisadi wanaotafuna nchi yetu? nadhani hawa ni kina Makamba na siyo ile CCM tunayoisikia kila kukicha huko UK. Wanajamii kaze ipo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,147
2,000
I feel hawa jamaa wa UK wako out of place and out of touch with reality. Nachelea kuhisi kuwa hili ni genge la watu ambao hawarudi kunusa nusa home .. Poleni sana
 

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,040
1,500
Maboksi haya yanasumbua jamani eti kwa kuzielezea kwa ufanisi....Pumba tupu hapa sioni lolote.....
 

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,040
1,500
Nimesoma mstari mmoja tu wa kwanza nikaanza kukutana na PUMBA...Hawa wote watoto wa mafisadi na wamepelekwa huko na fedha zetu walalahoi....Hivi Mijitu inayojiita miana UK au Miana CCM ya UK ina akili kweli? RADAR mbovu ilinOZI wa TZ Uk uliongoza kwa matumizi bado inamsifia huyu FISADI mkubwa...MIPUMBAVU KABISA ILIYOANDIKA HII PONGEZI...
 

Mountainmover

Member
Nov 9, 2010
45
95
Nimesoma hizo pongezi za hao CCM-UK wamerudia maneno 'kuvuna rasilimali za Taifa letu' mara mbili..mi naona ni mafisi tu nyie mlioko huko UK, mawazo yenu ni ukiritimba mtupu.
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,477
2,000
Kama ccm nzuri mnafanya nini kwa wazungu si mrudi nyumbani mkaishi maisha bora kwa kila mtanzania!! mmefulia. No wonder mna matawi kila kona mpaka uchochoroni.
 

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
0
Tanzanians in UK Kweli Wanamatatizo. Tunaona Jinsi Gani CCM Imejiimarisha Huko UK. This is Truly Shame for Those Tanzanians. Hakuna Wananchi Wanaona Wanatumiwa na CCM Huko Tanzania as Rubber Stamp Huko Kwenye European Face. CCM-Tanzania Wanawatumia Hawa CCM-UK kuonekana Wako Legitimate Huko Tanzania. Hao Hao Wanachama Wao Kila Leo Ndio Wanafanya Kazi Masaa Mengi Bila Kulala na Kutafuta Pesa Kutuma Kwa Wazazi Wao na Ndugu Zao Waweze Kumudu na Maisha Yao. Ndugu Zao Wanakufa Mahospitalini Hawana Dawa, Hawana Kazi na Wao Wanafanyiwa Party na Balozi wa Tanzania UK Ili Wajisikia Vizuri na Hii Hali ya Nchi. Wengi Tunaona ni Ujinga na Irresponsible to Be and Act Like This. Kitu cha Ajabu Wanasahau the Main Reason Why They are in UK, Beacause of Failures of CCM Policies Kama Inchi Yetu Ingekuwa Inashule Nzuri na Kazi Za Kutosha Nani Angehangaika Kuhamia UK? Kingine UK ni Hiyo Nchi Iliokupa Huo Uhuru na Wewe Utaki kuutumia Unataka Utumiwe na CCM. Thats Simple Shame! Watanzania UK Need to Get UP na Kuanza Kuuliza Maswali. Watanzania in Foreign Countries Need to Scrutinize The Truth and Stand for Transparency and Unite to Bring Awareness to Other Countries. Now We See Why UK Ambassador was Transfered to Washington to Expand CCM Foolishness, We Will See How That's Going to Work.
"CCM Sikuzote Inawapata Wananchi Wenye Njaa na Shida na Wajinga wa Kuwatumia na Siku Hizi Wamebaki Wachache Sana Inchini na Duniani"
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Tanzanians in UK Kweli Wanamatatizo. Tunaona Jinsi Gani CCM Imejiimarisha Huko UK. This is Truly Shame for Those Tanzanians. Hakuna Wananchi Wanaona Wanatumiwa na CCM Huko Tanzania as Rubber Stamp Huko Kwenye European Face. CCM-Tanzania Wanawatumia Hawa CCM-UK kuonekana Wako Legitimate Huko Tanzania. Hao Hao Wanachama Wao Kila Leo Ndio Wanafanya Kazi Masaa Mengi Bila Kulala na Kutafuta Pesa Kutuma Kwa Wazazi Wao na Ndugu Zao Waweze Kumuduz na Maisha Yao. Ndugu Zao Wanakufa Mahospitalini Hawana Dawa, Hawana Kazi na Wao Wanafanyiwa Party na Balozi wa Tanzania UK Ili Wajisikia Vizuri na Hii Hali ya Nchi. Wengi Tunaona ni Ujinga na Irresponsible to Be and Act Like This. Kitu cha Ajabu Wanasahau the Main Reason Why They are in UK, Beacause of Failures of CCM Policies Kama Inchi Yetu Ingekuwa Inashule Nzuri na Kazi Za Kutosha Nani Angehangaika Kuhamia UK? Kingine UK ni Hiyo Nchi Iliokupa Huo Uhuru na Wewe Utaki kuutumia Unataka Utumiwe na CCM. Thats Simple Shame! Watanzania UK Need to Get UP na Kuanza Kuuliza Maswali. Watanzania in Foreign Countries Need to Scrutinize The Truth and Stand for Transparency and Unit to Bring Awareness to Other Countries. Now We See Why UK Ambassador was Transfered to Washington to Expand CCM Foolishness, We Will See How That's Going to Work.
"CCM Sikuzote Inawapata Wananchi Wenye Njaa na Shida na Wajinga wa Kuwatumia na Siku Hizi Wamebaki Wachache Sana Inchini na Duniani"

Easy!

Sisi wengine tulikuja huku baada ya kudunduliza kwa miaka nenda rudi.
USije ukatujumrisha Sisi na Wao.
Watoto wa Mafisadi wamejaa sana huku First World, wengine wanakula nchi wengine wana soteshwa kana kwamba waliondoka kwao kwa Laana.
Ukisikia Matawi ya CCM huku First World ujue yameanzishwa na Wazushi kama wazushi waliko huko nyumbani Tanzania.

Unaongelea Party Ubalozini??

Mbona Balozi za Tanzania watu wana njaa kama nini? Hata bajeti ya chai taabu ,sembuse Mnuso?.

Huku tukitaka Party tunafanya wenyewe kwa Hela yetu ya Mabox.

Jamii ya watu wa ina yangu huku Ughaibuni wanajua ukweli kuhusu Tanzania kuliko Watanzania wengi walao wachuya kila siku na kuikumbatia CCM.

Huyu Balozi hapa atawapata Watoto wa mafisadi,Mabbwege na watu wenye tabia ya kujipendekezawengi tu wa kuunda Tawi la CCM kwa sababu watu wa aina hiyo hawakosekani mahali popote.

Sijui ni vipi atawapata watu na akili zao kujiunga na Msafara wao wa Kifisifisi??
 

Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
681
500
Nakerwa na hii generalization sana eti "Wana CCM na Watanzania UK waliridhika sana nawe Dkt. Kikwete" this is rubbish and not true kabisa. Ninyi watoto wa wakubwa mnaojiita wana ccm hapa Ughaibuni mkitaka kufanya mambo yenu acheni kusema all Tanzanians here. Where did we meet and send you to write such a statement. Huu ni uongo ninyi mnaojiita wana ccm msiopiga kura kila mwaka na mnapiga box hamtaki kurudi kushiriki taabu za nyumbani waacheni watanzania wenzetu waendeee na mchakato wao and when u write don't generalize all of us. Kwa namna hii unamdaganya mtawala wa nchi kuwa wote tumeridhika. Kuna watu tuko hapa na hatukubaliani kabisa na mwenendo wa mfumo mzima wa uchaguzi na utawala. Hata kama ni lazima ccm kuendelea kuongoza bado tunadhani kuwa chama hicho kinahitaji kufanya mabadiliko makukbwa ya kimfumo ili kumkomboa mtanzania wa kawaida. yaani be fair in writing guys
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom