Watanzania wengi wanataka kwenda peponi lakini hawataki kufa!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Ndugu zanguni salamus!
Tangu awamu ya tano iingie madarakani kumekuwa na mwamko mkubwa wa majadiliano ya kisiasa vijiweni na kwenye mitandao ya kijamii karibu yote.wanajadili kwa mapana hatua mbalimbali ambazo serikali ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli anachukua,UTUMBUAJI WA MAJIPU.

Kuna watu wanabeza ubomoaji wa nyumba zilizo jengwa mabondeni na sehemu zisizo ruhusiwa kisheria kama maeneo ya wazi, viwanja vya shule, jeshi n.k .Lakini watu hawahawa wanataka miji inayo pendeza na iliyo pangiliwa! huku ni kutamani kuingia peponi lakini hupendi kufa.

Watu wanatamani Nchi yetu iwe kama China kiuchumi lakini hawpendi kuona Rais wetu ana bana matumizi na kuelekeza fedha zetu kwenye matumizi ya maana tu.Wana sahau kuwa hata china walipitia kipindi cha kubana matumizi, kuongeza uzalishaji na kukusanya kila senti ya kodi yake.

Inatakiwa kuwa hivi, Mfanyakazi mzembe weka pembeni leta mchapakazi. Asiye bana matumizi weka pembeni leta anae bana matumizi.Mfanyakazi asiye mbunifu weka pembeni leta mbunifu.Aliye jenga eneo lisilotakiwa bomoa nyumba yake na alipe gharama za ubomoaji.Mla rushwa akithibitika jela miaka 30 na kufilisi mali yake.Wapo watakao dhurika, anaweza kuwa ndugu yako rafiki yako,mzazi wako au mpenzi wako lakini ukweli unabaki kuwa ukitaka kwenda peponi kufa ni lazima.
 
Kawaambie viongozi wako kwanza, wao ndo wamekuwa vinara wa kuhubir habar za pepo lkn kufa hawataki
 
Kawaambie viongozi wako kwanza, wao ndo wamekuwa vinara wa kuhubir habar za pepo lkn kufa hawataki
hatua mbalimbali anazo chukua mheshimiwa John Magufuli za kubana matumizi, kuzuia watu kwenda nje ya Nchi kwa kutumia fedha za serikali, kwenda kupima afya tu ughaibuni hatua hizi zote zikitekelezwa ipasavyo zinaweza kudhibiti thamani ya fedha yetu lakini pia tutakuwa na akiba ya fedha za kigeni za kutosha kwakuwa sasa hazitumiki ovyo kama hapo awali. kimsingi kila anae bana matumizi leo nd ndio tajiri wa kesho.Hii bomoabamoa ya sasa inalenga kujenga miji yenye hadhi, siyo kama ilivyo sasa kila sehemu ni hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom