Watanzania wengi wanalala Stoo/Store

Watanzania wengi wanalala Stoo/Store

Wakati ndugu zao walioko kijijini uhisi ndugu zao wa mjini wanaishi vizuri.

Ukweli ni kuwa wengi wamepanga chumba kimoja, umo umo ndoo za maji ya kunywa na kuoga, kitanda, vyombo etc.

Hawana na tofauti na wanafunzi wa hostel. Lengo langu si kuwasema vibaya bali mjitahidi mpige kazi kwa juhudi mtoke kulala stoo na kupanga nyumba nzima.

Siyo wageni wakija washindwa hadi kubadilisha nguo na kwenda kubadilisha nje.

Juhudi yako binafsi ndio itakunasua usilale stoo cha muhimu upige kazi usupoteze muda kupiga majungu.

Kazi kwenu sasa

wewe uko kundi gani?
 
Ninamaanisha uzidi kufanikiwa. Mafanikio hayana mwisho

Unajuaje kila mtu anataka mafanikio?

Kuna wengine hawataki mafanikio, wanataka kuishi bila ya responsibilities zinazokuja na mafanikio.

Hujanijibu unajuaje kwamba kila mtu anataka wageni.
 
Mleta mada pengine ulikua una dhamira njema ya kuelezea asilimia kubwa ya wakazi wa Dar wanavyoishi.
Lakini umeileta vibaya maana inaonekana kama kebehi,dharau au umefanya majivuno kwa kua labda wewe huishi ktk mazingira ya aina hiyo.
 
Hii mada inanihusu sna, kwani ni jambo ambalo kila siku rafiki yangu inaniimbia huu wimbo kwamba ifike siku tutoke kuishi kwenye stoo!
 
Kwani hivi mafanikio maana yake nini hasa?.
Kuishi kwenye nyumba nzima?.
 
UTAFITI unaonyesha zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanalala "Stoo/Store", Haiwezekani chumba cha kulala Mtu kiwe na vitu vyote hivi: Ndoo za maji, Sufuria, Jiko, viroba vya Mkaa, Sofa, Kitanda, Kabati, Friji, Kopo la Kuogea, Mabegi ya Nguo, Meza ya chakula, Baiskeli, Pikipiki, mifagio.
Je, Wewe kwako kuko hivyo?

Mkuu, nianze kwa kujibu..hapana, kwangu "hakuko" hivyo.

Lakini, ninajiuliza utagiti huu ni wa lini, ulifanyikaje na kwa lengo/dhumuni gani/lipi?
 
Wote tunaish poa sio case,tukilala kwenye mabox mnasema sis mafukara tukitahdi tupange at room 1 mnasema tunalala store!

tufanye jipi ambalo kwen ni jema aaaaah nenda zako na utafit wako wa kishamba
 
heeeeeeee sikujua kuwa kumbe stoo nako ni malazi ya watu
UTAFITI unaonyesha zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanalala "Stoo/Store", Haiwezekani chumba cha kulala Mtu kiwe na vitu vyote hivi: Ndoo za maji, Sufuria, Jiko, viroba vya Mkaa, Sofa, Kitanda, Kabati, Friji, Kopo la Kuogea, Mabegi ya Nguo, Meza ya chakula, Baiskeli, Pikipiki, mifagio.
Je, Wewe kwako kuko hivyo?
 
Daah kwahyo hii rum yangu store?? My God !! Nimetukanwa mwenzenu!!
 
Nimechekaje,ni kwelii kabisa umesemaa
 
bila kuficha ukweli ni kuwa watanzania wengi (hasa waajiriwa) wengi wetu tunaishi au kulala stoo,
maana haiwezekani chumba cha kulala kuna
-ndoo za maji,
-music system,
-vyombo vya cha kula,
-nguo,
-viatu,
-viroba vya mahindi na mchele,
jamani hiyo si ni stoo jamani,
vp wana jf wenzangu mnalala wapi..?
naomba kuwasilisha..!
 
Back
Top Bottom