Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk
Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?
Ni kweli tuna kundi kubwa la watu wavivu (kama mimi). Lakini kama viongozi wangekuwa wanawajibika, wangekuwa na uwezo wa kukemea wasiowajibika. Kwa vile viongozi wengi ni watawala wasiowajibika, watawaliwa nao tumelemaa. Watanzania wanatakiwa kusahau kuwa maendeleo yao yatatokana na uongozi bora (ambao haupo). Kwa hali ya sasa maendeleo ya Mtanzania yatatokana na kila mmoja kuchukia hali aliyonayo na kuamua kubadilika. Ni vigumu kwa Tanzania kubadilika kama kundi.
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk
Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?
Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:
n.k, nk.
- Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
- Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
- Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
- Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
- Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
- Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
- Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
- Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
- Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
- Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.
Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?
Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana
-Motisha mdogo
-Mapenzi madogo
-Mishahara midogo
Sikubaliani na hii dhana ya kuwa watanzania ni wavivu, ninachofahamu ni kuwa watanzania hawako serious na kazi za umma. Ukimkuta kaajiriwa katika kampuni ya binafsi, au kama anafanya shughuli zake binafsi utagundua kuwa mtanzania ni mchapaji kazi mzuri sana. Hebu fuatlia watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi uone jinsi wanavyobeba maboksi bila kujali.
........................!!!
Tatizo lililopo Tanzania ni mfumo mbovu wa uongozi na usimamizi tu. Kama viongozi wa kazi hawako serious ni dhahiri hata wafuasi pia hawatakuwa serious. Nadhani swali la kujiuliza ni kwa nini mfumo wetu wa usimamizi na uongozi uko vile katika taasisi zote za umma.
........................!!!
Katika experience yangu hiyo, ninachoona ni kuwa mfumo wa uongozi na usimamizi ndio uliobadilika na kusababisha utendaji wa kazi nao kuharibika.
Hivi ni visingizio tu maana hata wale wanaolipwa mamilioni hawana toafuti yeyote katika vigezo alivyovitoa Alien.
WaTanzania sisi Ni wavivu sana, kwa kukuhakikishia hebu hapo ulipo kama unaweza kutizama nje, ama waeza kutoka nje na kuangalia wapitao njiani utaona jinsi wanavyotembea kivivu. mtu hana haraka wala malengo ya aendako.
Kwa ukweli usimamizi wa kazi ni mbovu sana Bongo.
Wenzetu wana time-sheets na performance reviews hata kwa wabeba box!! Ukichelewa hata dakika kumi inakua noma! Ukifanya ndo tabia lazima uitwe na HR manager!! Cant even imagine eti uchomoke lisaa lizima ukanywe Chai! ukirudi hauna kazi. Vilevile watu wana lead by example, ukimwona supervisor wako amekamata ufagio anasafisha duka unajua watu wako serious.
...labda serikali ibadili system, tuwe nasi tunalipwa kwa masaa tunayoyafanyia kazi.
mfano; kima cha chini,
tshs 1'000/- kwa saa moja * masaa 7.5 (saba na nusu) ya kazi
=tshs 7'500/- kwa siku
mtu huyo kwa wiki ataingiza
tshs 7'500/- kwa siku * siku 5 za wiki = 37'500/- malipo yake ya jumla kwa wiki
ambayo ni sawa na
tshs 37'500/- kwa wiki * majuma manne katika mwezi = 150'000/-
kinyume na hapo, haya mambo ya uhakika wa malipo mwisho wa mwezi, hata kama kila wiki mfanyakazi anavisingizio vya 'nimefiwa na shemeji yake mke wa jirani', nk hayatakwisha!
Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.
Huo ndiyo ukweli viongozi wa serikali na mashirika wanachangia sana kuhusu hili suala la uvivu. Angalia ATCL Management na Board wamechangia kuliingiza shirika hili ktika matatizo makubwa sana, lakini hadi hii leo bado wanapeta tu na kupokea mishahara yao minono na marupurupu wakati shirika haliingizi pesa yoyote katika hali kama hii tunategemea kweli mfanyakazi wa kawaida awe na motisha wa kufanya kazi wakati anaona shirika limehujumiwa na viongozi wa juu lakini hakuna wa kuwagusa.
Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.
Mimi napiga kazi mahali fulani , najituma sana kibinafsi maana nimeona wenzetu huko nje wanavyofanya, ila sehemu hii ya kazi inaboa sana . Wakuu ni wabinafsi, wana upendeleo wa wazi wazi na mishahara sio even . Mimi na kimaster changu naona upuuzi, nimeamua kufanya biashara ambayo natumia muda wao mwingi kuimonitor. Sababu ni kuwa haka kabishara kananijali zaidi kuliko mwajiri wangu wa sasas. This is how life is in Bongo.