Watanzania wengi ni wapenda haki

Watanzania wengi ni wapenda haki

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,648
Reaction score
10,844
Ukiangalia comments za watu wengi waliotoa maoni kwenye hotuba ya Dr. Josephath Gwajima aliyoitoa Jana, utagundua kuwa asilimia kubwa sana wanamuunga mkono na kumpongeza kwa sababu ya aliyoyasema!

Inajulikana kuwa Askofu Gwajima ni CCM, lakini kwa sababu hoja zake zimeweka mbele maslahi ya nchi, amepata uungwaji mkono toka kwa watu mbali mbali bila kujali itikadi zao. Mada yake imeungwa mkono kama ambazo za watu wengine wazalendo zimekuwa zikiungwa mkono. Naweza fananisha "nondo" zake na za akina DR. BENSON BAGONZA, DR. CHARLES KITIMA, ASKOFU BANDIKILE MWAMAKULA, SHEHE PONDA, JAJI WARIOBA, MZEE BUTIKU, PROFESA ISSA SHIVJI, n.k.

Ukiangalia comments za hotuba ya Gwajima Jana, pamoja na comments za mada za watajwa hapo juu, utabaini kuwa Watanzania wengi:
1. Hawana udini linapokuja suala lenye maslahi kwa umma

2. Hawana uchama kwenye masuala yanayohusu maslahi ya nchi

3. Wako tayari kushirikiana na yeyote mwenye uzalendo bila kujali dini yake, kabila lake na hata Chama chake!
 
Back
Top Bottom