Watanzania wengi akili yao ni ''shake well'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wengi akili yao ni ''shake well''

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anyisile Obheli, Jul 2, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wengi wa watanzania akili yao ni ya kutingisha, maana hainingii akilini kama akili yao iko standard ama lah,
  we mtu anawezaje kuuza haki yake, tena kwa kulaghaiwa na furana, doti za khanga na kofia? kwa kukaribisha shida zaidi?
  katika maisha yake, maana hizo khanga, fulana na kofia zitakwisha kwa muda wa miezi tu na pengine wiki tu, lakini vipi tuendako?
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwanza inabidi uelewe kuwa 80% ya watanzania wanaishi vijijini. Sijui wewe mwenzangu kama ulishawahi kuishi kijijini.Ila sio siri hali ni mbaya sana kule. watu kuvaa nguo mpya ni swala jipya kabisa katika mfumo wao wa kimaisha. So hata akitokea mtu wa kumpa doti ya Kitenge huwa mkombozi kwake. Njaa ni kali ajabu. So kuwalaumu inakua sio vizuri kwa sababu wengi hawajui mfumo mzima wa uongozi wao hakuchi kunakucha bora siku ziende. Mimi nafikiri uwepo mfumo wa kuelimisha wananchi hasa wa vijijini (Ndo CCM inaposhindia) juu ya swala la uongozi wa nchi na madhara yake pale linapofanyika kosa kwa kumchagua kiongozi bora. Otherwise tutabaki kuwa nchi masikini kwa sababu ya umasikini wa nkufikiri wa viongozi tunawachagua.
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uko sahihi mkuu,
  ukweli ndiyo maana watu wa mijini tunaonekana wapiga kelele tu, hasa kwa kuwa ili hawa majambazi wa serikali yetu waendelee kutesa ni lazima wabane elimu ambayo ndiyo mtaji mkuu wa mwanadamu kimaisha, na wakibana elimu ni lazima taifa litakuwa na uwingi wa watu masikini ambao baadaye hutumiwa kama mtaji kwenye uchaguzi, hasa kwa sababu kama ulizozitoa hapo juu,

  mizizi yao ya kuwashikilia kwenye madaraka ya unyonyaji ni watu waishio vijijini amba chai kwao huikia tu kwenye matangazo ya viredio vya wajumbe wa nyumba wa nyumba kumi kumi ''chai bora iwe chai bora,...chai bora kiboko cha ubora.'' hili jambo ni hatari sana, lakini nani wa kumfunga paka kengere?
  hata mjini nako wako wasomi na wasomi ambao nao vinywani mwao kunatoka harufu mbaya ya ulevi wa mvinyo chapa ''ccm'' sasa kama hawa wanaoona japo chembe ya upuzi ambao serikali yetu imekuwa ikifanya, wanadiriki hata kutoa visenti vyao mifukoni kwa ajili ya kuifadhiri mijizi ya mali za umma unategemea nini?
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  :sick: tatizo niufinyu wa elimu ya uraia. kama elimu husika itaenezwa nina uhakika watanzania watafanya maamuzi kwa ridhaa yao na sio takrima. mbona jirani zetu kenya, malawi, na zambia wananchi wanaelewa haki na wajibu wao kama raia? ni suala la elimu hiyo ndilo hata kanisa katoliki lilikuwa linajaribu kusema kwa njia ya waraka wake lakini watanzania hao hao tukawabeza CPT.
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sikubaliani na nyie wote, angalau huko vijijini utapata wabunge na viongozi wa upinzani. Kama mnayoyasema ni kweli kuna wabunge wangapi wa upinzani Dar, hapa si ndio wapo wenye elimu, wenye mwanga wa kuona mambo n.k. Matokeo yake mijini ndio kunakotia aibu, tukubali tu kuwa waTZ tuna kasoro. Pamoja na jitihada zote walizofanya waliojitoa muhanga kutuonyesha jinzi tunavyoibiwa ndio kwanza, watu na digirii zao wanaunga mkono na kutoa maksi kwa uongozi mzuri.
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sawa sawa kabisa mkuu, tatizo ni kwamba tushazoea kubwata, lakini ukweli ni kwamba tungejaaliwa kuwa watu wa kukaa na kujisumbu akili zetu juu ya jambo furani tungegundua kwamba rc walikuwa sahihi na kutaka kufikisha kile ambacho wanaona kitaifaa jamii, kumbuka kuwa waliojaribu kuupotosha ule waraka baadhi ni wale tunaowaona wasomi nchini tena wengine wakajaribu kuuhusianisha kidini zaidi, wengine nao wakija huku na za kwao pasi na kuangalia kwanza kwamba hawa wenzetu wamevumbua nini?
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tutajie wabunge wapinzani wa vijijini ni wangapi, akina nani?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Matatizo yote yako mjini msiwalaumu Watanzania wa vijijini.. hadi hivi sasa ni vijijini ndio kuna mwamko zaidi wa kisiasa kuliko mjini!
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ukweli ndiyo huo Mzee Mwanakijiji,
  mjini unafiki ni mwingi na kujifanya tunajua sana, kwa hili linaweza kunifumbua macho na kuona kuwa inawezekana vijijini huko watu wameelimika sana katika nyanja ya, kujitambua kifahamu kuliko watu wa mjini, mjini watu too much talking but nothing decision at the end of the point, an we still stupid people, ujanja ujanja tu midomoni na kujifanya paka katikati ya kundi la paka huku tuna harufu ya panya,
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Labda uvute hii fikra na dhana zaidi ya hapo ulipoifikisha. Fikiria haya:
  1. Mwenye njaa utamwelimisha vipi?
  2. Nani atafanya kazi ya kuelimisha?
  3. Je mfumo unaridhia kufunulia waliolala? Kwa maneno mengine - ujinga wa hawa watu wa vijijini ( hata maskini wa mjini) ni mtaji wa nani?
  ALALAYE USIMWASHE....
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Barabara, hujakosea ni kweli wana mwamko wa siasa ni kwa ajili ya matatizo yao. Lakini ni jinsi gani wanaruhusiwa kuyakataa na au kuyapinga. Unajua kuwa DC akiita mutani hawaruhusiwi kukosa na wakikosa ni issue.Watalalamika wapi Hakimu wa mahakama ya mwanzo ndo hivyo, hakimu wa wilaya anataka cheo nagazi za juu ndo usiseme .

  Mjini tunaona Poa kwa sababu majority ya wakazi wa mjini tunaishi kwa kubomu kwa utamu wa ulimi wao, na wengine wanaoshindwa wanachukua vyao kwa nguvu Bongo tambarare si unaona wanavyosema wenyewe.

  Nakumbuka LOGO ya TIB ile ya enzi zile inarepresent typically maisha yalivyo sasa hivi.

  Mwenye kuweza kutundia aiweke.
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mjini alternatives nyingi, vishoka, madalali, wapigadebe, wakakapoa, wadadapoa etc vijijini huwezi kufanya hivyo utakuwa outcast i swear. Kutokana na hizo alteranatives wa mjini wanaona maisha tambarare wa vijijini wanajikalia kimya tu wakisubiri niujiza.
   
 13. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
  Vijijini kuna dadapoa tena sana ndugu! Kinachokosekana ni sofistikesheni ya mjini .Kwa standadi zao usipime!Vijijini bei ni makubaliano - ulimiwe shamba lako, ununuliwe kaulanzi, nk.mnabadilishana tu siyo lazima cash.
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tausi, nakubaliana na wewe, hakuna mahali niloapa kwa jina la mungu. Sikutaka kuongelea vijijini kwa sababu wengi tumejikita mjini, ukienda kijijini kwa jinsi sisi wa mjini tulivyo hatuwezi jua kuwa kuna mambo haya.

  Nashukuru kuwa umepanua wigo, ladba niongezee wigo shuleni watoto wasio na ada, hospitali wagonjwa wasio na hela na bwana shamba, ma afisa mifugo, mahakimu na wenyeviti wa mitaa just to mention a few.

  Nashukuru unaelewa jinsi gani mtu wa kijijini anavyopata shida kuishi, it is sadand pathetic.
   
Loading...