MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,285
- 50,552
Nimetembelea mikoa mingi na wilaya nyingi za Tanzania, kuna kitu kimoja nilikiona kila nilikoenda, watoto wenu wakiwa wadogo mnawafundisha heshima vizuri sana hadi ilinigusa kweli. Yaani kila nikipita sehemu watoto wanacheza, ghafla wanasitisha na kunipa shikamoo, najikuta nimesimama na kupokea salamu zao kwa furaha sana, hilo nimeliona kwenye kila wilaya ambayo nimewahi kupitia, japo Dar kidogo hamnazo maana halipo sana pale.
Sasa huwa najiuliza, ikiwa mnakua kwenye mazingira yenye heshima kiasi hicho, hivi huwa mnapinda baadaye vipi. Haya majungu na cheche za wivu ambazo huwa mumelea mnayapatia wapi na katika umri upi, au itakua mitaala kwenye shule zenu ndio huwa zinaanza kuwapindisha.
Takwimu za nchi zenye furaha duniani, Tanzania huwa imeorodheshwa kama nchi ya watu wenye majungu sana. Yaani ya nane kutoka mwisho, ambapo ya mwisho kabisa ni jirani wenu Burundi. Africa's 'happiest' countries revealed - CNN.com
Na hilo halina uwongo maana kwa watu ambao wameishi na nyie, lipo wazi tu, unakuta unaweza kumkaribisha Mtanzania kwako, uendeshe gari hadi uwanja wa ndege kumpokea, na kumpeleka hotelini, uwe naye muda wote anakuhitaji na umwelekeze kwa kila kitu. Hatimaye umkaribishe nyumbani kabisa, apokelewe na watoto kwa furaha, mcheke na kula na kunywa wote, hatimaye umpeleke hadi uwanjani aondoke, baadaye unakuja kusikia maneno amezungumza kuhusu maisha yenu hadi inatamausha.
Unakuta hata mtu akiwatembelea hapo Tanzania, mnacheka naye na kunywa pamoja na kuonyesha furaha isiyo na kifani, lakini kimya kimya mnakusanya majungu full ya kutisha. Kama hizi mada huwa mnaanzishanga 'eti nipo na Wakenya hapa, hawa watu.....', halafu utakuta huyo mtu anacheka cheka na kukenua meno na hao hao Wakenya na kuonyesha undugu wa hali ya juu. Halafu mnafanya kwa wote, unakuta leo mnaongea ya Wanyarwanda kesho ya Waganda na wengineo