Watanzania "wanyonge" na "masikini" tutaje nafuu tuliyoipata tangu awamu ya tano iingie madarakani

Maskini na wanyonge full maumivu,hospital za serikali kila kitu unalipa file,vipimo kumuona dokta,madawa na kulazwa
Hivi hao wanyonge wanasaidiwaje?
Sasa Wewe Ulitaka Kila Kitu Kiwe Bure? Lipa Kodi Leta Maendeleo
 
angalau kodi iliokuwa inakatwa kila mwisho wa mwez ya umeme imeondolewa
1. foleni ya sukari na bei juu.
2. foleni ya mafuta, petrol, deseli,
3. kuto muona mbunge wangu akinitetea akiwa bungeni
4. Ajira na promotion kwa wafanyakazi kusitishwa ghafla,
5. kuto kosoa serikali
 
Juzi Nilienda Hospitar Ya Mkoa Nikakuta Bei Ya Card Pale Mapokezi Imepanda Toka 1000 Hadi 5000. Nilipo Huliza Nini Tatizo?? Nikajibiwa HAPA KAZI TU.

Basi Maskini Mimi Ikabidi Tu Niwe Mpole.
 
Mpaka Sasa Nampongeza Sana JPM Karudisha Heshima Kwa Na Tumaini Kwa Watz.
Wanasiasa Wamekuwa Wanafiki Coz Of Pesa, Wanatengeneza Figisu Tuendelee Kuumizwa.
Piga Kazi JPM.
Yapo mazuri ya kumpongeza rais wetu kwa kweli lakin pia bila unafiki mapungufu yapo pia.
 
huku uswahilini kwetu hatuangalii kama maisha yetu yamekuwa bora ama lah,tumefurahi kwelikweli wale waliokuwa wanatutesa na hela zao kwa kubadilisha magari sasa hivi kila ikifika kuanzia tarehe 15 ya mwezi tunapanda nao daladala wanapaki magari yao wanajifanya wanapenda nao kupanda mabasi ya mwendokazi kumbe hela ya mafuta imewaishia!
 
CBG ziko shule chache sana, Ni wanafunzi wachache tu wanaochaguliwa kusomea combination subjects hizi. Hata shule za binafsi ni hivyo. Shule ni chache na wanachagua wanafunzi waliofaulu Div. 1 na kwa uhache sana 2 pekee. Jaribu Marian Boys au St. Joseph Cathedral.

shule chache serikali imelala tu kila mwaka waseme shule chache :):):) maana CBG ni comb rahisi sana kuanzisha kwenye shule yenye PCB na HGL haihitaji hata walimu wa ziada!
 
huku uswahilini kwetu hatuangalii kama maisha yetu yamekuwa bora ama lah,tumefurahi kwelikweli wale waliokuwa wanatutesa na hela zao kwa kubadilisha magari sasa hivi kila ikifika kuanzia tarehe 15 ya mwezi tunapanda nao daladala wanapaki magari yao wanajifanya wanapenda nao kupanda mabasi ya mwendokazi kumbe hela ya mafuta imewaishia!
huo ni ujinga ,roho mbaya au uchawi,angalia maisha yako na watoto wako akipaki nyumbani aifanyi mwanao aende chooni jali yako kwanza
 
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa.

Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala.

Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000.

Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati.

Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje?

Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.

hilo kundi kubwa la wahudumu limetoka wapi!? au ndo akili za mwendo kasi
 
shule chache serikali imelala tu kila mwaka waseme shule chache :):):) maana CBG ni comb rahisi sana kuanzisha kwenye shule yenye PCB na HGL haihitaji hata walimu wa ziada!
Ndugu, kuna kitu kinaitwa economics of education and planning. Kusoma combination yoyote ya A-level is not the end in itself. Kuna mambo kadhaa yanafikiriwa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa uwiano wa uhitaji wa taifa wa wataalam kutokana na combination husika.

Jipe muda kufikiria. PCB ni core science combination kama ilivyo HGE kwa masomo ya arts. Sehemu kuwa ya wanafunzi wanaosoma na kufaulu PCB wanaweza kusoma kiwango cha shahada course zozote kiwango cha shahada zinazosomwa na wanafunzi wanaosoma CBG. Ila kwa kuzingatia kuwa baadhi ya wanafunzi wanaweza kushindwa kufanya vizuri PCB, CBG inatoa fursa kuziba pengo kidogo. Mipango mingine ya namna hiyo inasukwa kwa kuzingatia dhana hiyo ya economics of education and planning.

Tusikimbilie kulaumu tu badala ya kufahamu rationality kwa kila uamuzi kuhusu masomo ya elimu ya juu. Ni vizuri pia kwa wazazi kuwashauri watoto kusoma masomo ambayo kuingia A-level inakuwa na fursa kubwa Zaidi, provided wamefaulu.
 
umejeukia madesa mapema sana....sababu walioitoa wenye mamlaka ni shule kujaa, nimekwambia CBG ni rahisi kuanzishwa kwenye shule yenye PCB na HG yeyote maana walewale walimu waliopo watatumika...kinachohitajika ni madarasa tu.
 
Hii shock ya kiuchumi imesababisha mzunguko wa pesa kuwa mdogo matokeo yake wafanyabiashara wadogo wanashuhudia kushuka kwa biashara zao na hawa ndio wanaousukuma uchumi si ajabu wengi wakafilisika au kufilisiwa na taasisi za fedha kutokana na kutomudu marejesho, sasa hawa ndio wahangaikaji wenyewe sio wale mafisadi au mapapa mabilionea wanaoweza kwenda hata nchi za nje wakaendelea na biashara zao. Ajira zimepungua, miradi mingi pia imesimama kwa sababu moja au nyingine, kusema kweli hali kwa mlalahoi si nzuri kwa hili hakuna ubishi. Je tunakwenda wapi hii ndio itatuletea faraja au karaha inategemea na vision ya viongozi wetu. Tunavumilia joto la bakery ili tuje kula mkate, lakini wapishi wasiongeze sana moto maana unaweza kuta mkate umeungua. Du tuombe Mungu.
 
Hoja iliyoko hapa ni kuhusu masikini na wanyonge......ukimgusa bakhresa inamsaidia nini mkazi wa tandahimba ambaye umempa jukumu la kulipa VAT 18% na ananunua sukari 3200?
Nanunua 2800 - 2600, usinisingizie 3200 ... Ila mengne umesema kweli
 
Kingine wahisani wawekezaji wanaondoja nchini watalii hawaji.. Kisa kodi ya kukurupuka kuiga Kenya..
 
Naona Magu ni selfish sana.. Kichwami anawaza kukomoa watu,.. Muangalieni hata hotuba zake zimekaa kishari shari.. Hana hotuba smbayo ni balanced.. Ni za kishari na za visasi..
 
Naona Magu ni selfish sana.. Kichwami anawaza kukomoa watu,.. Muangalieni hata hotuba zake zimekaa kishari shari.. Hana hotuba smbayo ni balanced.. Ni za kishari na za visasi.. ..
 
Heshma imerejea na soko la Chimpumu lımeongezeka,Uzınzi na uasherati umepungua,wake zetu sasa wametulia,foleni zimepungua sana brbrn,ulevi wa kupindukıa umepungua, uwajibikaji umeongezeka.
 
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwamba ina kazi ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii.

Kama taifa hatujapata tafsiri ya hakika ya "mnyonge" pengine masikini tunaweza kuelewa.

Bajeti imepita, maisha yanaendelea, wale wanyonge na masikini mpaka sasa mmeona dalili za unafuu tangu serikali iingie madarakani?

Binafsi ninachokiona ni umasikini mkali kupindukia na uliokosa suluhisho la muda mfupi na mrefu,badala yake tunaambiwa tulizoea hela za bure na hatufanyi Kazi.

Sheria kandamizi za kodi ikiwamo ile ya miamala zinapigilia misumari kwenye umasikini huh kwa kuwa serikali imelenga kuzipata hata elfu mbilimbili za masikini.

Kwa upande wa unyonge ndio haswa,hakuna anqyejua unyonge ni nini mpaka sasa pengine ikiwamo hao wanaotuhubiria.

Ewe maskini na mnyonge, hebu tuambie mwenzetu. Maisha yako sasa yako vizuri, angalau hata dalili?
Wakati nasoma hii post taarifa ya habari ITV inaonyesha wananchi wa Mbaka huko Rugwe wakifurahia kujengewa daraja la kuwawezesha kuvuka mto walilojengewa na serikali ya awamu ya tano na wamelipa jina la Mhagama! Kwa miaka nenda rudi walikuwa wakivuka kwa shida wakitumia kamba. Hawa ni wananchi wa Tanzania ambao serikali imeona shida yao na kuwasaidia. Kuna mengi ambayo kwa muda mfupi sana Serikali hii imeyafanya kwa manufaa ya wananchi wanyonge ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja wa kuwajaza mapesa bali kushughulikia kero zao mbalimbali na kuwajengea mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo na hatimaye waweze kujijaza mapesa kutokana na kufanyakazi kwa bidiii.
 
Back
Top Bottom