Watanzania "wanyonge" na "masikini" tutaje nafuu tuliyoipata tangu awamu ya tano iingie madarakani

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwamba ina kazi ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii.

Kama taifa hatujapata tafsiri ya hakika ya "mnyonge" pengine masikini tunaweza kuelewa.

Bajeti imepita, maisha yanaendelea, wale wanyonge na masikini mpaka sasa mmeona dalili za unafuu tangu serikali iingie madarakani?

Binafsi ninachokiona ni umasikini mkali kupindukia na uliokosa suluhisho la muda mfupi na mrefu,badala yake tunaambiwa tulizoea hela za bure na hatufanyi Kazi.

Sheria kandamizi za kodi ikiwamo ile ya miamala zinapigilia misumari kwenye umasikini huh kwa kuwa serikali imelenga kuzipata hata elfu mbilimbili za masikini.

Kwa upande wa unyonge ndio haswa,hakuna anqyejua unyonge ni nini mpaka sasa pengine ikiwamo hao wanaotuhubiria.

Ewe maskini na mnyonge, hebu tuambie mwenzetu. Maisha yako sasa yako vizuri, angalau hata dalili?
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali.
Hoja iliyoko hapa ni kuhusu masikini na wanyonge......ukimgusa bakhresa inamsaidia nini mkazi wa tandahimba ambaye umempa jukumu la kulipa VAT 18% na ananunua sukari 3200?
 
1468057417447.jpg
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
No vzr kuuujibu hoja kama hz bila jazba wala siasa maana nchi hii n yetubsote. Kama kuumia twaumia site na kama no naumivu twaumia sote bila kujali irikadi zetu. Naomba rujadili kwa hoja. Nikweli kuwa ukijipa muda nafuu itapatikana ? Au tunahitaji miaka 5 tuje na kauli mbiu nyingine ya kiwahadaa waz?
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
mambo mazuri kwa mtanzania ni kuona hakuna mfumuko wa bei ili hata kwa kile kidogo alichonacho aweze kununua mahitaji muhimu. sasa katika bajeti iliyopitishwa unaweza kunitajia mkakati upi unaolenga kutimiza hilo? bidhaa madukani bei juu,tuliambiwa vifaa vya ujenzi vitateremshwa bei lakini imeshindikana.au kama una fununu kuwa hicho kipini cha mpito ni miaka mingapi utujuze.
 
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa.

Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala.

Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000.

Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati.

Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje?

Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.
 
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa. Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala. Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000. Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati. Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje? Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.
Umeme ulishushwa tangu enzi ya jk
 
mambo mazuri kwa mtanzania ni kuona hakuna mfumuko wa bei ili hata kwa kile kidogo alichonacho aweze kununua mahitaji muhimu. sasa katika bajeti iliyopitishwa unaweza kunitajia mkakati upi unaolenga kutimiza hilo? bidhaa madukani bei juu,tuliambiwa vifaa vya ujenzi vitateremshwa bei lakini imeshindikana.au kama una fununu kuwa hicho kipini cha mpito ni miaka mingapi utujuze.
Maisha yamekuwa magumu sana .....wanauchumi wa awamu ya tano wanasema watanzania walizoea hela za bure......hivi hela ya bure ingekuwepo si angekuta nusu ya nchi wanaendesha benzi?
 
Niliplan ku- top up mkopo ili nipaue! Sasa nimeshindwa maana hakuna nyongeza ya mshahara isipokuwa hiyo 3800/= ya pungozo la PAYE!
Nilikuwa nafundisha tuition ili nipate hela ya kulipia pango ,sasa hamna tena wanafunzi,matokeo yake itabidi nihamie uswahilini!
Nilikuwa nawapatia ndugu zangu elfu 30 ya matumizi,sasa basi! Hata wakinilaani,laana itaenda kwa serikali!
 
Umeme ulishushwa tangu enzi ya jk

Siyo kweli, Mh. Mhongo ndiye aliyeiagiza Ewura na Tanesco kureview bei za umeme downwards, baada ya kuteuliwa na Mh. Rais kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa wizara husika.

Pia, tanki za gesi ya kupikia za uzito wa kilo 15, kwa jiji la Mbeya ilikuwa inauzwa kwa shilingi 54,000/- Baada ya Magufuli kuingia hivi sasa ni shilingi 46,500/- Na watanzania wengi wanahamia kwenye gesi kwa kuwa ukilinganisha na mkaa (gunia Shs. 35,000/) tofauti siyo kubwa sana.

Hivi sasa hospitali za umma mtu unaulizwa tukusaidie nini? umeshahudumiwa? Watoto wanafundishwa mashuleni. Wale waliokuwa wanapenda kupiga stori makazini ndiyo wanaumia, na wapiga dili (aka miungu watu) katika ofisi za umma.

Nimepata hatii za viwanja vyangu ndani ya wiki moja. Hakuna ubabaishaji wala senti ya kulainisha mchakato. Kama unajishughulisha mambo ni mazuri, ila kama ulikuwa dalali wa huduma za serikali au mpambe wa wanasiasa, karibu shambani. Vitunguu na viazi vinalipa kwelikweli.

NB: Ukishaanzisha mada waache wengine wachangie. Kitendo cha mtoa mada kuwa ndiye commenter mkuu kinaleta picha ya mtu anayependa ligi just for the sake of it. Ukishaiweka ajenda mezani, iangalie inavyorutubishwa au kukatwakatwa kwa misingi ya uzito na ukweli wake.
 
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwamba ina kazi ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii.

Kama taifa hatujapata tafsiri ya hakika ya "mnyonge" pengine masikini tunaweza kuelewa.

Bajeti imepita,maisha yanaendelea,wale wanyonge na masikini mpaka sasa mmeona dalili za unafuu tangu serikali iingie madarakani?
Binafsi ninachokiona ni umasikini mkali kupindukia na uliokosa suluhisho la muda mfupi na mrefu,badala yake tunaambiwa tulizoea hela za bure na hatufanyi Kazi.

Sheria kandamizi za kodi ikiwamo ile ya miamala zinapigilia misumari kwenye umasikini huh kwa kuwa serikali imelenga kuzipata hata elfu mbilimbili za masikini.

Kwa upande wa unyonge ndio haswa,hakuna anqyejua unyonge ni nini mpaka sasa pengine ikiwamo hao wanaotuhubiria. .

Ewe maskini na mnyonge,hebu tuambie mwenzetu,Maisha yako sasa yako vizuri,angalau hata dalili?

Ninachokiona hapa "UCHWARA" umetumfanya watz kuwa watu wajabu sana, tulilala masikimi tumeamka matajili hata kuwazidi wamareka. bei za vitu zinazidi kulilo kule marekani, bei ya sukari ni hapa kazi tu, bei za vitu vingini tunaendele kuzisoma namba za maluwe luwe utazani ccm imetupepeka kuzimu
 
Maisha yamekuwa magumu sana .....wanauchumi wa awamu ya tano wanasema watanzania walizoea hela za bure......hivi hela ya bure ingekuwepo si angekuta nusu ya nchi wanaendesha benzi?
kuna wenzetu humu hawataki kuzungumzia hali halisi ya maisha ya kiuchumi ya watanzania walio wengi kwa sasa.hata kama serikali imekosea ukikosoa unaitwa mpinzani maana hawawezi kujibu hoja.
 
Back
Top Bottom