Watanzania "wanyonge" na "masikini" tutaje nafuu tuliyoipata tangu awamu ya tano iingie madarakani

Mkuu, Sikia majibu watakayokuambia
1) Bora sasa tunapanda wote daladala
2) Bora sasa tunasugua wote na tunapata wote msoto uswahilini
3) Bora sasa wote tunaenda shule kwa miguu hakuna tena school bus
4) Idd tulisotea wote pilau bila mbwembwe
5) Mwisho wanakwambia heshima imerudi mtaani na wanamalizia HAPA KAZI TU!

Hayo ndo wanayojivunia kwenye huu utawala hao majobless!!
Naona hata JF wale jamaa wana majibu kama haya,wao hawadili na ishu,wanadili na watu.

Hapo ndipo wanapowadanganya watanzania.Watanzania hawahoji tena mambo ya msingi,wanasubiri mkubwa fulani kamfukuza mwenzie,akirudi nyumbani hana chochote kabakiza stork tu kwa Mke NA wanae wanaopiga miayo.
 
Unaelewa kazi ya msingi ya wizara ya viwanda ni nini katika suala hili? ama unahisi wizara iko pale kutoa mtaji kwa kila kiwanda? Sasa jiulize hizo pesa za hiyo general tire 60bn zimetoka wizara gani kama kufinance viwanda ni bajeti ya wizara.
Pesa za general tire hawana,hizo bilioni 80 ni za mishahara,juisi na mikate,wakipeleka bilioni 60 general tire wizara itashindwa kujiendesha,general tire wana bajeti ya hela ya mlinzi
 
Ongeza na elimu bure hapo
Hata kuona serikali inaanza kukusanya kodi kwa kila anayetakiwa kwangu ni unafuhu mkubwa sana, haiwezekani udai maendeleo wakati hutaki kulipa kodi, unadai maji, unadai umeme lakini wewe kodi hutaki kutoa.

Pili, Kupatikana umeme pasipo usumbufu mkubwa sahivi, ukikuta sahivi umeme umekatika basi jua kuna tatizo kubwa sana mahala.

Tatu, Kushuka bei ya umeme majumbani, sahivi mie nalipia 10000 mwezi mzima wakati nilikuwa lazima nitoe 40000.

Nikiwa na shida sahivi kuanzia ofisi ya mtaa mpaka manispaa ni chap chap nashughulikiwa na naendelea na majukumu mengine kwa wakati.

Kwenda hospitali sahivi natibiwa tena na kundi kubwa la wahudumu kila mmoja ananiuliza najisikiaje?

Yako mengi na nategemea mengi sana pale bajeti hii ikielekea kwenye miezi ya sept na okt hasa kwenye miundombinu.
 
Hoja iliyoko hapa ni kuhusu masikini na wanyonge......ukimgusa bakhresa inamsaidia nini mkazi wa tandahimba ambaye umempa jukumu la kulipa VAT 18% na ananunua sukari 3200?
mkuu mpaka tandahimba unakufaham
 
Mtumishi gani anapewa mshahala baada ya siku tano,hebu acha uongo siku hizi ikifika tarehe 25 tuu mshahara unakiwepo bank..kama ww unachelewa basi labda ni tatizo la bank yako ambapo mshahara unapitia.
Ungekuwa Mwanangu ningekuchapa vibao hata kusoma hujui .
 
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwamba ina kazi ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii.

Kama taifa hatujapata tafsiri ya hakika ya "mnyonge" pengine masikini tunaweza kuelewa.

Bajeti imepita, maisha yanaendelea, wale wanyonge na masikini mpaka sasa mmeona dalili za unafuu tangu serikali iingie madarakani?

Binafsi ninachokiona ni umasikini mkali kupindukia na uliokosa suluhisho la muda mfupi na mrefu,badala yake tunaambiwa tulizoea hela za bure na hatufanyi Kazi.

Sheria kandamizi za kodi ikiwamo ile ya miamala zinapigilia misumari kwenye umasikini huh kwa kuwa serikali imelenga kuzipata hata elfu mbilimbili za masikini.

Kwa upande wa unyonge ndio haswa,hakuna anqyejua unyonge ni nini mpaka sasa pengine ikiwamo hao wanaotuhubiria.

Ewe maskini na mnyonge, hebu tuambie mwenzetu. Maisha yako sasa yako vizuri, angalau hata dalili?
Awamu ya 4 mishahara ilipanda sana kiasi cha kutia moyo ,ila Awamu wa 5 tu asubiri..ili tupate unafuu wa maisha na heshima ya mfanyakazi ionekane, ijapo mkubwa ametuahidi hatawaangusha wafanya kazi..tu nasubiri
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
Ukiwa masikini sana na kuwaza kuna kuwa chini sana. kiukweli maisha sasa yamekuwa magumu mara mbili kuliko awamu ya nne. Masikini wanafurahi tu kusikia mkubwa fulani kaachishwa kazi bila kujali haki imetendeka? masikini sana ni sawa na mchawi anae furahia mtu anateseka kwa maradhi ya kumroga wakati yeye hana anachopata.The head of a poor man is a workshop of a devil.Hata akiwa kiongozi masikini huwaza kimasikini.
 
Angalau serikali ya awamu ya tano imethubutu kuwagusa wale waliokuwa hawagusiki, kufanya yale yaliyoonekana haiwezekani. Kwa sababu hiyo maisha bora kwa Mtz yanaonekana japo kwa mbali. Tumaini jipya limezuka ndani ya mioyo ya wengi. Inajionyesha dhahiri Tz iliyonyooka inakuja na ile ya ujanjajanja inelekea kaburini. Usitake kuleta mihemuko, maskini na wanyonge tunatambua hiki ni kipindi cha mpito. Mambo mazuri yanahitaji muda na gharama.
Tatizo la masikini ni kuwa tajiri akiguswa unapata usingizi mnono wakati hata shuka ya usingizi huo huna. Ndicho unachokiongea hapa.
 
Siyo kweli, Mh. Mhongo ndiye aliyeiagiza Ewura na Tanesco kureview bei za umeme downwards, baada ya kuteuliwa na Mh. Rais kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa wizara husika.

Pia, tanki za gesi ya kupikia za uzito wa kilo 15, kwa jiji la Mbeya ilikuwa inauzwa kwa shilingi 54,000/- Baada ya Magufuli kuingia hivi sasa ni shilingi 46,500/- Na watanzania wengi wanahamia kwenye gesi kwa kuwa ukilinganisha na mkaa (gunia Shs. 35,000/) tofauti siyo kubwa sana.

Hivi sasa hospitali za umma mtu unaulizwa tukusaidie nini? umeshahudumiwa? Watoto wanafundishwa mashuleni. Wale waliokuwa wanapenda kupiga stori makazini ndiyo wanaumia, na wapiga dili (aka miungu watu) katika ofisi za umma.

Nimepata hatii za viwanja vyangu ndani ya wiki moja. Hakuna ubabaishaji wala senti ya kulainisha mchakato. Kama unajishughulisha mambo ni mazuri, ila kama ulikuwa dalali wa huduma za serikali au mpambe wa wanasiasa, karibu shambani. Vitunguu na viazi vinalipa kwelikweli.

NB: Ukishaanzisha mada waache wengine wachangie. Kitendo cha mtoa mada kuwa ndiye commenter mkuu kinaleta picha ya mtu anayependa ligi just for the sake of it. Ukishaiweka ajenda mezani, iangalie inavyorutubishwa au kukatwakatwa kwa misingi ya uzito na ukweli wake.
Utaratibu wa wapi huo?
 
Ongeza na elimu bure hapo
Hatujagusia barabara mwenge-morocco. Faida nyingine ni kwamba sahivi wapinzani wameonekana vihoja mtaani. Hawaeleweki na wala hawaaminiki tena make wanapinga hata yale waliyokuwa wakiyadai ..sahivi wanajifanya hawayataki tena kwa kuyapiga mateke.
 
Tungoje nini?
Watumishi wa umma wanapewa mshahara,baada ya siku tano umeisha!!!
Nyuso zao zimefubaa kama wamepaka majivu

Akili ni nywele Na kila mtu ana zake, inawezekana wamewekeza fedha zao, au wamenywea pombe it's more of personal stop generalising
 
Back
Top Bottom