Watanzania wanaweza kuufanya huu muujiza, halafu tuone vioja?

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Tuseme itakuwepo tume huru ya uchaguzi, na uchaguzi uwe huru na wa haki bila ya mizengwe yoyote.

- Wananchi kwa ridhaa yao wenyewe waamue kumrudisha Magufuli katika urais, kwa kura za kutosha, (sio za kishindo, <70%)

- WaTanzania wachague wabunge wengi toka vyama vya upinzani (>80%) - why not? kama utabisha.

Najua wengi wenu kwa ushabiki wenu tu mtasema hili haliwezekani; lakini hamna sababu za msingi kuonyesha kwa nini haliwezekani.

Hii ni ngwe ya pili na ya mwisho kwa Magufuli, atakuwa hana wigo wa kufurukuta na 'ku'ride rough shod' kama alivyofanya kwenye hii ya mwanzo.

Atakuwa amepata uzoefu wa kutosha, na kutokana na karipio la wananchi, kwa kumpa bunge hilo, atakuwa na utambuzi wa kujua ni nani 'boss' katika hali hiyo.

Kutumia 'dola' kukandamiza kutakuwa hakupo tena, na itamlazimu afuate sheria na katiba katika utendaji wake wa kazi.

Katika hali hiyo, najua 'vioja' vitakuwa vimewekwa pembeni

Je, waTanzania wakielezwa manufaa ya uwiano huo wa kiutawala watasita kuunga mkono hapo Oktoba 2020?

CCM akili zitakuwa zimewaingia kichwani na kuanza kujua wenye nchi ni akina nani.

Wapinzani watapata fursa nzuri ya kuwa na uzoefu wa kiutawala kupitia bungeni.

Itakuwa ni hatua moja mhimu sana ya mabadiliko katika taifa letu.
 
Amini usiamini Rais wa wanyonge mwenye huruma na wananchi wake atachangia milion mia yeye peke yake kupitia viongozi wa chadema kuwa huru siku ya leo
 
Back
Top Bottom