Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira na Kazi)

mconservative

New Member
Aug 18, 2016
3
8
Waziri wa Ajira na Kazi; je unajua katika taifa hili huru bado kuna namna fulani ya ukoloni na ubaguzi mkubwa sana ambao unajikita katika misingi ya rangi ya ngozi zetu.

Mheshimiwa Waziri, kuna watanzania ambao kwa asili wanatoka bara lingine lakini wana uraia wa Tanzania, Watanzania hao wakianzisha kampuni zao basi wakitoa nafasi za ajira zile benifits wanazotoa kwa waajiriwa wao zinajikita katika kuangalia race zao ikiwa race yako inaendana na mwanzilishi/bosi wa kampuni hiyo basi utakuwa na upendeleo wa kupata remuneration kubwa zaidi ya wenzio ambao mnasifa moja na mnafanya kazi yenye majukumu sawa.

Mheshiwa, naomba serikali ifanye uchunguzi wenu muweze kupata majibu kwanini kunakuwa na waajiriwa wawili (different race) lakini sifa nyingine zote zinazofanana, ofisi moja, uraia nchi moja (Tanzania), sifa za elimu ni sawa, majukumu sawa, lakini katika haki ya malipo pamoja na haki nyingine kama bima za afya mnawekewa mipaka mwingine based on his race harusiwi kutibiwa katika hospital fulani kubwa lakini mwingine kwasababu ya race yake anaruhusiwe kwenda kutibiwa hapo.

Natambua hiyo ni sekta binafsi wanazo haki ya zakuwalipa na kuwapa stahiki mbalimbali waajiriwa wao vile wanavyopenda wao lakini treatment za namna hii ambazo kwa akili ya kawaida unatambua kwamba wanakuwa treat hivyo kwasababu tu ya race yao hii ni typical NEO-apartheid na hii inaleta unyonge mkubwa sana kwa wafanyakazi waofanyiwa hivyo najua wengi hawawezi kulalamika kwababu hawananamna nyingine yakupata vipato.

Nashauri serikali ifanye random research kwa kampuni kadhaa zinazomilikiwa na Watanzania hao wengi kutoka bara la mashariki mwa dunia wapeni onyo watakaobanika kufanya ubaguzi huu mkubwa. Tuweke misingi ya kudumisha usawa zaidi tusirudi tulikotoka.

Naomba kuwasilisha.
 
Itakuwa kanjibhai hao ndo wana tabia ya kulipa waswahili mishahara mbuzi, bila kusimamia kwa karibu sheria za kazi watu watakandamizwa sana huko kwenye ajira binafsi, ingawaje serikali na yenyewe ingeonyesha mfano kwa kulipa mishahara minono na marupurupu yote kwa watumishi wake ili waweze kuwa na pa kusimamia jinsi maslahi ya mfanyakazi yanavyotakiwa kuwa ikiwemo kima cha chini cha mshahara/posho.​
 
Back
Top Bottom