Baada ya David Kafulila kusimama na kuanza kumtetea Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ufasaha na weledi unaostahili kwenye mambo mbalimbali imepelekea kuibuka kwa kundi linalomuunga mkono Rais Samia na huyu jamaa Kafulila.
Sayansi ya siasa inasema kwenye uwanja wa kisiasa ni kosa kumpuuza mtu yotote hasa mwenye record za wazi kama ilivyo kwa Kafulila leo na record za Tegeta Escrow.
Limezuka pia kundi kinzani hasa toka Upinzani, hawataki kusikia Kafulila akitajwa kwa jema lolote kisa tu aliwakimbia na kurejea chama mama cha CCM wakati akitekeleza moja ya haki zake za kikatiba.
Wapo pia wanaosema kila anayemtaja humu Kafulila basi ni yeye mwenyewe Kafulila Kwa lugha nyepesi wanasema David Kafulila anajipigia debe hawa pia wanahitaji kujipa muda na kufuatilia kwa makini kama nilivyofanya Mimi.
Swali langu kwao,
Kama hawa wote wanaomtajataja Kafulila humu wao wenyewe ni Kafulila au wanatumwa na Kafulila Je, Yale makofi aliyopigiwa Kafulila pale Bungeni mpaka Spika akayasitisha kibabe alikuwa pia ni Kafulila mwenyewe anajipigia Makofi hayo? kama sivyo, kwani hao Wabunge waliompigia makofi bungeni wao humu Jf hawaruhusiwi kuwepo au kujiunga?
(nitaomba mwenye ile clip ya Kafulila Bungeni anipatie inbox)
Nimejipa muda wa kufanya utafiti hasa hapa Jf nimeridhika kuwa David Kafulila ni tishio huko mbeleni kama tu Mungu atampa uhai na Afya kwani ni kweli Watanzania wanataka kijana ambae anaaminika, kijana ambae anachukizwa na rushwa pamoja na ufisadi kaliba ya Kafulila.
Naomba na Mimi nitumie haki yangu hii ya kutoa maoni yangu.
soma pia haya maoni Je, ni nani kati ya hawa 10 anasifa za ziada za kuwa Mrithi wa Rais Samia atakapomaliza kipindi chake?