Watanzania wanaona nini kwa David Kafulila?

Watanzania wanaona nini kwa David Kafulila?

ABC ZA 2025

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2018
Posts
1,381
Reaction score
869

Baada ya David Kafulila kusimama na kuanza kumtetea Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ufasaha na weledi unaostahili kwenye mambo mbalimbali, Kitendo hiki kimeibua kundi linalomuunga mkono Rais Samia pamoja na David Kafulila mwenyewe.

Sayansi ya siasa inasema kwenye uwanja wa kisiasa ni kosa kumpuuza mtu yotote hasa mwenye record za wazi kama ilivyo kwa David Kafulila leo na record zake za Tegeta Escrow.

Limezuka pia kundi kinzani hasa toka Upinzani, hawataki kusikia David Kafulila akitajwa kwa jema lolote kisa tu aliwakimbia na kurejea chama mama cha Mapinduzi CCM wakati akitekeleza moja ya haki zake za kikatiba za kuwa katika chama chochote Cha siasa anachokipenda.

Wapo pia wanaosema kila anayemtaja David Kafulila hapa Jf basi ni yeye mwenyewe David Kafulila, Kwa lugha rahisi wanamaanisha David Kafulila anajipigia debe hawa pia wanahitaji kujipa muda na kufuatilia kwa makini kama nilivyofanya Mimi.

Swali langu kwao, Kama hawa wote wanaomtajataja Kafulila hapa, hao ni Kafulila wenyewe au wanatumwa na Kafulila Je, Yale makofi aliyopigiwa Kafulila pale Bungeni mpaka Spika akayasitisha kibabe alikuwa pia ni yeye Kafulila mwenyewe akijipigia Makofi hayo? kama sivyo, kwani hao Wabunge waliompigia makofi bungeni wao humu Jf hawaruhusiwi kuwepo au kujiunga?
(nitaomba mwenye ile clip ya Kafulila Bungeni anipatie inbox)

Nimejipa muda wa kufanya utafiti hasa hapa Jf na huku mitaani nimeridhika kuwa David Kafulila ni tishio huko mbeleni kama tu Mungu atampa uhai na afya njema kwani ni kweli Watanzania wanataka kijana ambae anaaminika, kijana ambae anachukizwa na rushwa pamoja na ufisadi mwenye kaliba ya David Kafulila.

Naomba na Mimi nitumie haki yangu hii ya kikatiba ya kutoa maoni yangu.

soma pia haya maoni Je, ni nani kati ya hawa 10 anasifa za ziada za kuwa Mrithi wa Rais Samia atakapomaliza kipindi chake?
 
Utakuwa akili haiko sawa km unaona ni heshima mtu kupigiwa makofi na bunge la sasa..pili hata kwa kutizama tu Kafulila hayuko timamu pengine alipata shida wakati akiwa mtoto kupelekea kuonekana hivyo alivyo, tatu kashindwa kukaa na mtu mmoja ndani hata miaka 10 haijafika huyo ndio unamuona anao uwezo kuongoza watu 10? Elimu ya kuokota okota na kusoma soma vihabari magazetini na kuanza kusifia hata school leaver anaweza kufanya ni jambo dogo sana!
 
Utakuwa akili haiko sawa km unaona ni heshima mtu kupigiwa makofi na bunge la sasa..pili hata kwa kutizama tu Kafulila hayuko timamu pengine alipata shida wakati akiwa mtoto kupelekea kuonekana hivyo alivyo, tatu kashindwa kukaa na mtu mmoja ndani hata miaka 10 haijafika huyo ndio unamuona anao uwezo kuongoza watu 10? Elimu ya kuokota okota na kusoma soma vihabari magazetini na kuanza kusifia hata school leaver anaweza kufanya ni jambo dogo sana!
Bahati mbaya kwenye Siasa hakuna kumdharau mtu, Mandela pia ndoa ilimshinda lakini ndio baba wa Taifa la SA, Mkapa pia ndoa haikuwa sawa.
 
Harafu huyu tumbili mama achukue hatua watu wanao penda kujiona wao ndo wapambanajii huku wakiwa na tamaa ya uongozi hao mama awatupe huko ni watu hatari sana.Yaan humu kuna thread za kumsfia kafulila kibao kama ndo mzalendo no moja tz.Mama piga chini huyu hata hicho kicheo ulicho mpa fukuzia mbali hii tumbili maana ana tamaa sana mtu huyu.
 
Back
Top Bottom