Watanzania wanaangamia kwa kukosa maarifa

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,578
1,984
Nimefuatilia sana mjadala wa kunyimwa msaada wa MCC na Marekani, nikakugundua kuwa bado Watanzania wengi ni wajinga na wanaongozwa na ushabiki badala ya kutafakari mambo.

Eti kisa Rais Magufuli kasema hatutabembeleza wahisani, ndio wanawatukana Marekani na misaada yao. Mi binafsi sitetei utegemezi wa misaada, lakini hebu tuambieni, lini Tanzania iliishj bila misaada? CCM wanaojifanya kujitegemea leo, ndio waliokubali bila kupenda kurejesha mfumo wa vyama vingi kama sharti la wahisani kuendele kutoa misaada mwaka 1992.

Ndio hao waliopiga teke azimio la Arusha na kuweka Azimio la Zanzibar. Ndio hao hao waliokubali masharti ya SAP ya benki ya dunia ili kuendele kupata misaada.

Leo wanaimba kunitegemea. Sikatai lakini tulishakosea tangu awali.
Mwalimu Nyerere alipambana na adui watatu ambao ni ujinga, umasikini na maradhi. Inasikitisha kuona leo miaka 54 ya uhuru Watanzania wengi ni wajinga wamebaki kuwa washabiki tu na bendera fuata upepo.
 
Wapinzani hawana hoja wanasubiri rais akosee ndiyo waongee #HapaKaziTu
 
Back
Top Bottom