Watanzania wana huzuni kuu, Wasilazimishwe kufurahi

Watanzania wana huzuni kuu, Wasilazimishwe kufurahi

Ahsante, hebu sema na kidogo kuhusu wazungu wanaokuja mikono mitupu isipokuwa project write ups Kisha wanakabidhiwa migodi, mbuga na baadae kuondoka wakiwa Matajiri wa kutupwa. Umewahi kuwagusa ktk maandiko Yako?!!! Wale wakurya walioachiwa mashimo tu na mazebaki yakiwa yameingia kwenye vyanzo vyao vya maji hatimaye kuwababua ngozi uliwaona?!!! Hawa wachina walioachiwa enzi na enzi wskiondoka na maliasili umewahi kuandika na kumwita mtawala kibaraka wa wachina?!!! Unafikiri wazungu hawajakabidhiwa mapori?!!! Pole km hujui hilo, hao ndo kitambo tu.
Tupambane na ujinga wetu, tuache chuki za kidini.


Dini lisifanywe chaka la kujitetea au kuwatetea waovu. Umeshasema kuwa kuna wachina wanaondoka na rasilimali za nchi bila nchi kunufaika, na ukauliza kama nimewahi kuwazungumzia. Kwa hiyo kwa akili yako, sijawaongelea wachina kwa sababu ni wa dini yangu?

North Mara, watu waluenda kuiba cover za plastics zinazozuia kemikali kuzagaa, wakazichana, wakaondoka na vipande. kemikali za sumu zilikaingia kwenye mifumo ya maji. Pamoja na kwamba hao vibaka ndio waliofanya makosa, Barrick ilisimamishwa kufanya kazi kwa muda mpaka walipoweza kithibitisha kuna ulinzi wa uhakika wa kuzuia vibaka kuja kufanya kama walivyofanya.

Lakini pia, huwezi kulinganisha uwekezaji katika utafutaji na uchimbaji madini na kupewa mbuga za wanyama. Japo ni kweli hata huko kwenye madini, wapo wababaishaji lakini wanajiita ni wawekezaji. Nao hatuwezi kuwafumbia macho.

Utafiti wa madini unahitaji tekinolojia kubwa na aghali, niambie mwarabu anayepewa mbuga ya wanyama Ngorongoro, amewekeza nini hata kuweza kupewa sifa ya kuwa mwekezaji? Unalinganisha vitu visivyoendana. Uchimbaji madini siyo kazi ndogo kama unavyofikiria, ndiyo maana mpaka sasa hivi ni zaidi ya miaka 30, tangu kugundulika kwa chuma Liganga na Nickel. Kabanga, licha ya mmamia ya mamilioni kutumika kwenye utafiti, mpaka leo hatujapata mwekezaji wa kuweza kuchimba.

Mpaka sasa hivi Umoja wa mataifa unatoa leseni ya uchimbaji madini kwenye deep sea (international water), kila kampuni kutoka nchi yoyote inaruhusiwa kuomba, lakini ni kampuni chache sana Duniani, zilizothubutu.

Hapa hatuongelei wawekezaji wa kweli, bali hawa waporaji wanaochukua rasilimali za nchi zisizohitaji uwekezaji wowote au tulikwishatengeza aenyewe: watu wanakuja wanapewa bandari yetu badala ya kupewa eneo wakajenge bandari; bafala ya kupewa eneo wakajenge uwanja wa ndege, wanapewa uwanja wa ndege ambao umekwishajengwa na unafanya kazi. Huu ni uhuni!!
 
Back
Top Bottom