Watanzania, na hasa Wataganyika, wanapitia kipindi kigumu sana, kipindi cha huzuni na mateso, kuliko wakati wowote wa uhai wa Taifa lao.
1. Mtanzania mwenzao anayeaminika sana kwa ukweli, utetezi wa haki, na uzalendo usio na shaka kwa Taifa lake, amewekwa gerezani kwa uonevu mkubwa, na kisha kutengenezewa kesi bandia ya uhaini.
2. Binadamu wenzao, Ali Kibao, Soka, Mdude na wengine kwa makumi wametekwa, wameuawa, na wengine wamepotezwa, na watawala wasiopenda kukosolewa hata wakifanya uovu wa kupindukia.
3. Watanganyika wakatoliki kiongozi wao, katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Father Dr. Kitima amevamia kwa lengo la kumwua, kwa sababu tu ya kupinga uporwaji wa rasilimali za nchi na kisha kupewa waarabu.
4. Watanganyika, rasilimali zao, bandari, mbuga za wanyama, hifadhi za misitu na viwanja vyao vya ndege, vimeporwa na kisha kukabidhiwa kwa waarabu.
5. Watanzania wanachezewa akili zao na kudharauliwa kwa kutengenezewa Tume bandia ya Uchaguzi, wamenyimwa haki zao za kueapata viongozi wanaowataka, huku chama kikuu cha upinzani kikizuiwa kushiriki uchaguzi.
6. Watanzania hawana mahakama tena, waovu wameziteka na kuzifanya zitumike kuwatesa Watanganyika wasiowataka.
HALAFU, mtu mmoja anaitwa Msigwa, anashangaa kwa nini Watanzania hawaendi kushuhudia mechi za CHAN. Ina maana:
1. Msigwa hajui kuwa Mpira ni burudani? Tangu lini mtu mwenye huzuni kuu akaenda kwenye burudani?
2. Msigwa hajui kuwa mpira ni starehe? Tangu lini mtu anayedhulumiwa haki zake akaenda kusherehekea?
3. Msigwa hajua kuwa michezo ni kiashiria cha furaha? Tangu lini mtu ambaye binadamu wenzake wametekwa, wameuawa, wengine hata miili yao haijaonekana, akaenda kufurahia?
Hima Watanzania wote wenye upendo, tuungane na Wakatoliki kufanya maombolezoya kuiombea haki nchi yetu ambayo mashetani yameiteka na kisha kuwadhulumu binadamu wenzao haki zao kwa namna mbalimbali.
Mungu mkuu, tunaomba mkono wako wenye nguvu na mamlaka utuokoe na hawa waovu, kwa maana wadhulumu wetu wamedhamiria kutuangamiza. Kama ulivyotenda kwa Farao, tunaomba utende na sasa. Tunaomba hayo yote kwa jina la mwanao Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu.