Watanzania wakati wa Mapinduzi ni huu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania wakati wa Mapinduzi ni huu...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yo Yo, Dec 7, 2011.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania,
  Leo nipo hapa kwenu kuwapa nguvu,hamasa na hali ya kuweza kujikomboa.Tumenyanyaswa vya kutosha tumenyonywa kiasi cha kutosha ila sasa basi,imetosha ndugu Watanzania.
  Ni wakati wetu sasa tujikomboe....ni wakati wa kufanya mapinduzi....mapinduzi yatakayotutoa kwenye dhama hili...mapinduzi ndio solution iliobaki.....

  Ndugu wenzangu lazima tufanye mapinduzi juu ya fikra zetu....haya ndio mapinduzi ninayotaka watanzania tufanye....hamna muda wa kulala tena ni wakati wa kila mmoja wetu kuamka...

  Kuna wakati Namnukuu Mwalimu Nyerere alisema, "Sungura alimuuliza siafu unakwenda wapi, Siafu akajibu KUMUUA TEMBO!!! Sungura kwa mshangao akasema lakini Tembo mkubwa sana mtamuweza?? Siafu akajibu TUTAJARIBU TENA TENA TENA NA TENA..."

  Wengi wetu tuna hasira kali na nchi yetu iliyotuangusha na kuzidi kutuangusha hadi hivi sasa. Kuanzia masuala ya mishahara ya Walimu; ada za shule; umeme usiotabirika; kufa kwa huduma za halmashauri ya Jiji; kuporomoka kwa huduma za afya ya msingi; utamaduni wa ufujaji na rushwa kwa wafanyakazi na viongozi wa serikali yetu; uwekaji rehani wa mali ya mtanzania katika jina la ubinafsifishaji na soko huria na kadhalika.
  Kuwa na hisia kali ni jambo zuri tu kwani nchi yoyote iliyoendelea au mfumo wowote uliowahi kufanya kazi vyema ulijengwa na wale wenye hisia zenye mrengo mkali.

  Leo hii hakuna kujaribu ni tufanye.....huu mchezo wanaotuchezea watawala hawa sasa basi.....
   
 2. Jackson jonh

  Jackson jonh Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I like it,niko pamoja na wewe mkuu
   
 3. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja mkuu.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Msigonge key-board tu fanyeni kweli!!
   
Loading...