Watanzania, Upole wetu unatuponza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania, Upole wetu unatuponza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji192, Feb 8, 2011.

 1. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Sisi watanzania tuko wapole sana.

  Tunaelewa kabisa sasa kuwa mmiliki wa Dowans ni Rostam. Hilo nalo linathibitishwa na ukweli kwamba hata wakili Fungamtama ameajiliwa na Rostam, ndiyo maana ndiye amewasilisha mahakama kuu madai ya kulipwa pesa hizo, Bilioni 94. Huyohuyo ndiye aliyewahi kulishtaki gazeti la Mwanahalisi mwaka 2008 kama wakili wa Rostam. Huyu lazima atakuwa anafahamu who are Dowans!! Bosi aliyemtuma ni Rostam, anajua kila kitu. Ni mfanyakaazi wa Rostam.

  Kwa nini tusimshtaki Rostam? Kwanini Rais asiamuru huyo mbunge avuliwe uanachama, akamatwe, afunguliwe mashtaka?? Kwanini mali za Dowans zisitaifishwe?

  Huu ndio uzembe wa Rais wetu unapodhihirika. Anasogeza wakati ili 2015 ifike aondoke zake. Tusikubali kudanganywa eti Rais hamjui kuwa Rostam ndiye mmiliki wa Dowans. Kama ndivyo hana nia ya dhati ya kuisaidia nchi hii. Ndiyo maana na hotuba yake juzi alisema, hawezi kufanya kitu kipya kwa watanzania. Tutabaki hapa hapa tulipo, no development. Maana yake, ufisadi ushamiri chini ya mikono yake, achume kilicho chake, akimbie after 2015.

  Tunahitaji kukasirika pale tunapogundua kuonewa.
   
 2. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa tumekwisha onekana mabwege, tunakamuliwa kodi matumizi yake nadhani wote tunashuhudia kinachojiri mjengoni. Wanajua tu kuwa wakiandamana ni kuwapiga mabomu. Yaani kwa kifupi wanatudharau sana. Tufanyeje? wakutusaidia walikuwa ni vyombo vya dola kwa kuwa upande wetu lakini wao wako kimya!

  Suluhisho? nashauri sasa imefika wakati wa kulipatia kazi jeshi letu. Wao baada ya vita vya Kagera wako likizo wanaoteana vitambi. Nadhani uzoefu katika jambo ni kitu cha msingi. Kusema kweli hivi sasa tukipigana na jeshi la Rwanda msishangae tunapigwa vibaya pamoja na vifaa, watu na utajiri wetu.

  Natamani atokee angalau copro mmoja wa jeshi alianzishe tumuunge mkono, hata kama asipo pata kuungwa mkono na wenzie askari kitaa tupo kibao. Hao magenerali na vyeo vingine vya juu hawawezi kufanya lolote kwa kuwa wanakula na mafisadi.

  Bora tupigane ili wachache watakao baki na vizazi vya baadae wafaidi neema tuliyojaliwa katika nchi hii. Tutakapo baki na mashimo matupu yaliyobaki baada ya kuchimba dhahabu kuna faida gani? au kuna faida gani kuishi katika dhiki hii ambayo inaongezeka kila kukicha? Woga wetu hauto tusaidia na ndio wanautumia kutumaliza.
   
 3. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,180
  Likes Received: 10,372
  Trophy Points: 280
  Kama ulikuwa kwenye mawazo yangu. Mimi niko tayari hata leo
   
 4. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana na kufadhaika sana moyoni hivi amani na utii wetu ndio unatuponza tunyanyasike? Watunga sheria ni mashabiki na walaghai tu leo wametia chumvi na pilipili kwenye kidonda kibichi.

  Kwa hela hizi za NSSF nasema sina imani na Bunge. Wote waliokuwa humo hawatakii nchi hii amani nasema hawaitakii nchi hii amani.
   
Loading...