Hukumu ya ICC yamtaja Rostam Aziz mmiliki wa Dowans!

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Ukiisoma hii story ya KULIKONI kwa makini, inaelekea kuwa hukumu ya ICC inamtaja Rostam Aziz ndiye mmiliki wa Dowans! Sote tunajua mtu anayeimiliki Richmond/Dowans si mwingine bali ni Rostam kwa kushirikiana na Edward Lowassa. Je, tutaipataje hukumu original ya ICC ambayo haijachakachuliwa wana JF? Kwani rulings zao hazitakiwi zitolewe kwa members of public?

Nahisi kampuni ya REX Attorneys ndiyo iliiwakilisha Tanesco ICC na mmoja wa wanasheria wake ana nakala ya hukumu hii lakini katishwa na Rostam asiitoe.

REX Attorneys, inayomilikiwa na balozi wa Tanzania wa zamani wa U.K. (sasa wa U.S.), Mwanaidi Maajar, ililipwa na Tanesco a cool 5 billion/- kwa kazi hii...

Mbunge wa Dowans 'achakachua' nyaraka

* Ni baada ya jina lake kutajwa kwenye hukumu

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

MBUNGE wa Tanzania, ambaye pia ni mfanyabiashara anayehusishwa na kashfa kubwa za ufisadi hapa nchini, ametajwa kwenye nyaraka za hukumu iliyotolewa na mahakama ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya Dowans Holdings.

Mbunge huyo, jina tunalo, hivi sasa anafanya jitihada kubwa kujaribu "kuchakachua" hukumu hiyo ili kuficha jina lake lisionekane.

Mwanasiasa huyo tayari ametumia pesa nyingi na vitisho kuhakikisha kuwa hukumu hiyo kamili inafichwa ili isijulikane kwa umma kuwa yeye ndiye mmiliki wa Dowans ambaye amekuwa siku zote hataki kujitokeza hadharani.

Habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kuwa hata Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajapatiwa nakala ya hukumu kamili iliyotolewa na ICC.

"Tangu hukumu ya Dowana kutolewa na ICC kuitaka TANESCO iilipe kampuni hii ya kitapeli shilingi bilioni 185, imeshindikana kusajili hukumu hii kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania," alisema mwanasheria mmoja wa serikali.

"Hii inatokana na kuwa kuna jitihada za kifisadi zinafanywa kucheza na hii hukumu ili kunyofoa kurasa ambazo zinamtaja mbunge huyu kuwa ndiye mmiliki wa Dowans."

Hukumu kamili ya ICC kwenye shauri namba 15947/VRO la Dowans Holndings SA (Costa Rica)/Dowans Tanzania Limited (walalamikaji) dhidi ya TANESCO (mlalamikiwa) ina takriban kurasa 150.

Hata hivyo, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na waandishi wa habari wamepewa nakala za sehemu tu ya hukumu hiyo.

"Aliyekuwa anakwenda kwenye mashauriano ya keshi ya ICC ni mmoja wa wafanyakazi wa Mbunge huyu. Baada ya majaji kumbana mfanyakazi huyo, alimtaja bosi wake kuwa ndiye mmiliki wa Dowans," alisema mwanasheria huyo wa serikali.

"Ukisoma hukumu kamili ya ICC na mwenendo wa kesi yenyewe utaona kuwa jina la XXXXXX (anamtaja Mbunge huyo) limo sehemu kadhaa kwenye nyaraka hizo."

Ili Dowans iweze kufuatilia malipo yaliyopendekezwa na ICC, ni lazima hukumu kamili ya shauri hilo isajiliwe kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa kampuni ya wanasheria iliyoiwakilisha TANESCO kwenye shauri dhidi ya Dowana ICC inayo nakala ya hukumu kamili lakini kuna vitisho vimetolewa na mbunge huyo ili hukumu hiyo isitolewe hadharani.

Viongozi wa serikali wazoefu wa masuala ya sheria wanaona hakuna uhalali wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kujihusisha na mikataba ya utata kama wa Dowans.

"Dowans na Richmond ni ndugu wale wale. Hakuna serikali yoyote duniani inayo simamia haki inaweza kulazimishwa kuwalipa Dowans," alisema Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Sitta alisema kuwa wamiliki wa Richmond na Dowans ni genge moja la watu watatu wanaotaka kutumia pesa hizo kujiandaa kuununua Urais mwaka 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Wahusika kwa nini hawajakamatwa? Mkataba wa Dowans ni kimyume na sheria ya manunuzi ya umma. Serikali gani ina wajibu wa kuheshimu mkataba wa kihuni?"

Sitta alihoji kuwa iweje baada ya Richmond kushindwa kazi, kampuni hiyo hiyo tena iiteuwe Dowans kurithi mkataba huo badala ya serikali kuifukuza Richmond na kutangaza upya tenda kama sheria ya manunuzi ya umma (Public Procurement Act) inavyosema.

Mbunge huyo ambaye pia amehusishwa na kashfa ya wizi wa fedha za Benki Kuu kupitia akaunti ya EPA anatajwa kuongoza kundi la wanasiasa waovu ndani ya CCM wenye lengo la kuutwaa Urais wa nchi baada ya Kikwete.

"Huyu mbunge mwenyewe kwanza uraia wake una mashaka na hakubaliki na Watanzania nje ya jimbo lake la ubunge. Lakini ana nguvu kubwa za kifisadi ndani ya CCM kutokana na utajiri mkubwa alionao wa pesa haramu," alisema mbunge mmoja wa CCM.

"Lengo lake ni kuiibia serikali kupitia Dowans na mikataba mingine ya kifisadi ili aweke Rais wake 2015 na kuendelea kufilisi rasilimali za Tanzania."

Kuna wabunge watatu wengine waandamizi wanatajwa kumsaidia mbunge huyo mwenzao ili kupata malipo ya Dowans.

"Mmoja wa wabunge hawa alikuwa na cheo kikubwa sana serikalini, mwingine ni mwanasheria naye aliwahi kuwa kigogo serikalini na mwingine ni mwanasheria na ni mfanyabiashara mkubwa. Ni genge la wanasiasa hatari mafisadi," alisema afisa mmoja wa serikali.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema hivi karibuni kuwa serikali inaipitia hukumu ya Dowans ili kuona ni hatua gani za kisheria inaweza kukuchukua.

Hata hivyo, habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kuwa serikali yenyewe haijapewa nakala ya hukumu kamili ya ICC ambayo pamoja na mambo mengine, inamtaja mbunge huyo kuwa ni mmiliki wa Dowan.

"Sasa hivi kazi iliyopo ni ku-doctor (kuchakachua) hukumu halisi ya ICC ili nakala ya hukumu itakayopelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania kusajiliwe isiwe na jina la huyu fisadi mkuu Tanzania kama mmiliki wa Dowans," alisema mwanasheria mmoja anayefahama suala hilo.

"Hii inadhihirisha kuwa serikali sasa imesalimu amri kwa mafisadi na wanafanya chochote wanachotaka kwa kutumia nguvu ya pesa zao haramu."

Source: KULIKONI issue ya Desemba 24-30
 
IMMA advocates= Masha + Rz1
REX Attorneys=Maajar aka Tanzania ambassador to USA, her firm work against government(TANESCO) paid about Tshs 5 billions

Mkono advocates=Mkono who had a dubious deal to represent BOT,paid almost Ths 8 billions!
 
Ukiisoma hii story ya KULIKONI kwa makini, inaelekea kuwa hukumu ya ICC inamtaja Rostam Aziz ndiye mmiliki wa Dowans! Sote tunajua mtu anayeimiliki Richmond/Dowans si mwingine bali ni Rostam kwa kushirikiana na Edward Lowassa. Je, tutaipataje hukumu original ya ICC ambayo haijachakachuliwa wana JF? Kwani rulings zao hazitakiwi zitolewe kwa members of public?

Nahisi kampuni ya REX Attorneys ndiyo iliiwakilisha Tanesco ICC na mmoja wa wanasheria wake ana nakala ya hukumu hii lakini katishwa na Rostam asiitoe.

REX Attorneys, inayomilikiwa na balozi wa Tanzania wa zamani wa U.K. (sasa wa U.S.), Mwanaidi Maajar, ililipwa na Tanesco a cool 5 billion/- kwa kazi hii...
sijaona alipotajwa hebu nionyeshe mkuu

mbona na wewe unakua kama wale tena?
 
Ndiyo maana siku yakitokea mapinduzi kazi ya kumuua RA nitaifanya mimi kwa mikono yangu bila kutumia silaha
 
sijaona alipotajwa hebu nionyeshe mkuu

mbona na wewe unakua kama wale tena?

Duuh, kwani Mbunge na business tycoon gani anayehusishwa na Richmond/Dowans siku zote hizo ni nani kama si Rostam Aziz? Soma ripoti ya kamati ya Mwakyembe. Mtu aliyekuwa anaiwakilisha Dowans kwenye kesi ya ICC ni mfanyakazi wa CASPIAN Construction inayomilikiwa na Rostam. Alipobanwa na majaji aseme nani mmiliki wa Dowans jamaa akamtaja Rostam. Hii iko kwenye ruling ya ICC. Eti TANESCO ambao ndiyo wahusika wakuu wa kesi hii hawana nakala kamili ya uamuzi wa ICC.
 
please jamani watanzania tuache tabia zakutofuatili mambo kwa usahihi wake,huyu mwandishi anatakiwa kutaja kile hukumu inachozungumza na nani anatajwa katika hukumu hiyo,sio swala la kutuambia mbunge,tuna wabunge wengi sio lazima awe rostam.riport ya richimond inasema mmiliki wa kampuni hizi hajulikani ni kampuni za kitapeli,hivi mpaka kampuni inashinda kesi mahakamani bado mmiliki wake ni jambo la kuendelea kuhisi?tuache tabia za uzandiki wa kutumiwa vibaya na wanasiasa mfilisi.nyie waandishi wa habari andikeni vitu kamili na sahihi,sio kutaka kuuza magazeti yenu tu,nasi jf hoja zisizo na kichwa wala miguu hatuna sababu ya kuzizarau na kuwambia wawasilishaji wale fulldata za habari zao.​
 
watanganyika, ni heri kufa tukiipigania nchi yetu kuliko kukaa kimya huku tukinyanyaswa na mafisadi KWANINI TUSIINGIE VITANI? tena itakua vita nzuri sana. Peoples power vs mafisadi. Natoa hoja
 
Duh kweli TZ noma!! Mpaka hukumu ya ICC inachakachuliwa?? Sasa Pinda alivyosema watalipa, wanalipaje bila kuona hukumu??
 
Duuh, kwani Mbunge na business tycoon gani anayehusishwa na Richmond/Dowans siku zote hizo ni nani kama si Rostam Aziz? Soma ripoti ya kamati ya Mwakyembe. Mtu aliyekuwa anaiwakilisha Dowans kwenye kesi ya ICC ni mfanyakazi wa CASPIAN Construction inayomilikiwa na Rostam. Alipobanwa na majaji aseme nani mmiliki wa Dowans jamaa akamtaja Rostam. Hii iko kwenye ruling ya ICC. Eti TANESCO ambao ndiyo wahusika wakuu wa kesi hii hawana nakala kamili ya uamuzi wa ICC.

Birds of the same feather fly together! Unafikiri TANESCO haiko chini ya CCM ambamo akina Rostam wamo?
 
please jamani watanzania tuache tabia zakutofuatili mambo kwa usahihi wake,huyu mwandishi anatakiwa kutaja kile hukumu inachozungumza na nani anatajwa katika hukumu hiyo,sio swala la kutuambia mbunge,tuna wabunge wengi sio lazima awe rostam.riport ya richimond inasema mmiliki wa kampuni hizi hajulikani ni kampuni za kitapeli,hivi mpaka kampuni inashinda kesi mahakamani bado mmiliki wake ni jambo la kuendelea kuhisi?tuache tabia za uzandiki wa kutumiwa vibaya na wanasiasa mfilisi.nyie waandishi wa habari andikeni vitu kamili na sahihi,sio kutaka kuuza magazeti yenu tu,nasi jf hoja zisizo na kichwa wala miguu hatuna sababu ya kuzizarau na kuwambia wawasilishaji wale fulldata za habari zao.​

Biashara ya magazeti ngumu kaka, ukiingia kichwa kichwa kutaja majina sometime utajikuta pabaya na serikali ikakuruka. Hukuona juzi MWANAHALISI ilisema wamiliki wa Dowans hawa hapa lakini haikutaja majina ingawa ukiisoma habari yenyewe kama inawataja Rostam Aziz, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Nimrod Mkono, etc
 
Mbona MwanaHalisi iliwahi kuibandika "list of shame" kama ilivyo wandugu? Tuseme siku hizi "wameshajirudi?"
 
Lakini hukumu lazima iwe public knowledge. Kama siyo mbona habari za gharama tunazotakiwa kulipwa zimepatikana haraka haraka tu wakati majina yanafuata baadaye!!
 
Duuh, kwani Mbunge na business tycoon gani anayehusishwa na Richmond/Dowans siku zote hizo ni nani kama si Rostam Aziz? Soma ripoti ya kamati ya Mwakyembe. Mtu aliyekuwa anaiwakilisha Dowans kwenye kesi ya ICC ni mfanyakazi wa CASPIAN Construction inayomilikiwa na Rostam. Alipobanwa na majaji aseme nani mmiliki wa Dowans jamaa akamtaja Rostam. Hii iko kwenye ruling ya ICC. Eti TANESCO ambao ndiyo wahusika wakuu wa kesi hii hawana nakala kamili ya uamuzi wa ICC.
Hivi EL sio tycoon?
 
Mijitu mingine haina haya kweli kweli, utadhani huyo RA katajwa kweli kumbe ni hallucination!
 
Mimi naona suala hili limechukua muda mrefu kulitatua kutokana na kusitasita kwa Serikali kwa sababu zisizoeleweka. Hakuna ubishi kwamba Richmond ilitutapeli kwa kuleta mitambo isiyokidhi viwango tilivyolipia. Kampuni yenyewe ime-prove ni feki huko Merikani.

Pili, Dowans imethibitishwa na Mwarabu (Mwana Mfalme = Prince) aliyetajwa kuwa ndiye mwenye hisa kwamba ni feki. Hata huko Costa Rica kunakodaiwa mmiliki mwingine yupo, Serikali ya nchi hiyo imethibitisha taarifa hiyo ni ya uongo. Kwa hiyo hii Dowans ni feki pia.

Kwa hiyo bila hata kuwahusisha hawa vigogo Wabunge na Wanasheria wa hapa kwetu, wanaotajwa na Kubenea na Samwel Sitta, napendekeza Serikali ichukue hatua ya kutaifisha hii kampuni ya Dowans kwa kupitisha Sheria Bungeni kwa tukitumia nguvu yetu ya Sovereignty. Tutamke katika hiyo sheria kwamba hatutalipa fidia kwa atayejitokeza kwamba ni mmiliki wa Dowans. Sababu ya kutolipa fidia ni kwamba TANESCO wameshawalipa vya kutosha hawa mafisadi.
 
Vyombo vya habari Tanzania vinatia kichefuchefu habari inaandikwa kimafumbo mafumbo utadhani tuko kwenye taarabu. Yani ili gazeti limeshindwa kuwasiliana na ICC na kuomba kopi ya hiyo hukumu?
 
Back
Top Bottom