Watanzania ulipozaliwa ndiyo kwenu, acheni Ujinga na Ujima!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,815
Mna mambo ya kizamani sana na wala hamfiti kwenye Dunia ya leo, unakutana na mtu anakuuliza kwenu wapi unamwambia Morogoro au Mtwara anakuuliza hapo siyo kwenu bali useme walikotoka wazazi wako, huo ni ujinga na ujima, Dunia nzima mahali ulipozaliwa na kukulia ndiyo kwako, kama wewe Wazazi wako walitoka Songea lkn umezaliwa Muheza, basi ukiulizwa unatoka wapi sema natoka Muheza, na siyo Songea ambapo wala haupajui!

Nawajua watu ambao wamezaliwa na kukulia Arusha City lkn ukimuuliza kwenu wapi anakwambia walipotoka Wazazi wake wkt wala hapajui na hajawahi kufika, na Arusha City ndiyo sehemu anayoijua klk yoyote ile Dunia hii...
 
Siku ukifa ndio watu wanahangaika kukupeleka kwenu wakati ukiwa hai akuna aliyekuwa anashughulika.

Ulikozaliwa ndiyo kwenu acheni hayo mambo ya kulazimishana kuwapangia watu kwao wapi, na mpango wa kurudishana kijijini kuzikana kwa kuwa Wazazi walitoka huko ni ujinga uliopitiliza!
 
Naweza kusema kwetu ni Dar es Salaam lakini wazazi wangu ni watu waliotoka Kilimanjaro na Mm nimezaliwa Dar es Salaam
 
Mna mambo ya kizamani sana na wala hamfiti kwenye Dunia ya leo, unakutana na mtu anakuuliza kwenu wapi unamwambia Morogoro au Mtwara anakuuliza hapo siyo kwenu bali useme walikotoka wazazi wako, huo ni ujinga na ujima, Dunia nzima mahali ulipozaliwa na kukulia ndiyo kwako, kama wewe Wazazi wako walitoka Songea lkn umezaliwa Muheza, basi ukiulizwa unatoka wapi sema natoka Muheza, na siyo Songea ambapo wala haupajui!

Nawajua watu ambao wamezaliwa na kukulia Arusha City lkn ukimuuliza kwenye wapi anakwambia walipotoka Wazazi wake wkt wala hapajui na hajawahi kufika, na Arusha City ndiyo sehemu anayoijua klk yoyote ile Dunia hii...
Kama mzazi kazaliwa arusha na wewe umezaliwa dar na mnakaa mfano nyumba ya serikal huyo baba akifa akarudshwa au kuzkwa arusha utaishi dar au arusha?
 
Kama mzazi kazaliwa arusha na wewe umezaliwa dar na mnakaa mfano nyumba ya serikal huyo baba akifa akarudshwa au kuzkwa arusha utaishi dar au arusha?

Ulikozaliwa ndiyo kwenu, hivyo kama nimezaliwa na kukulia Arusha City, hapo Arusha City ndiyo kwangu na nitazikiwa hapo!
 
Taratibu basi na mada yako hii, mbona una jazba?

Mimi nimezaliwa kijiji cha Nyibhoko, Kata ya Kisaka, Tarafa ya Ngoreme, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara. Nikiwa na miezi 9, wazazi wangu wamehamia Mwanza, nikiwa na miaka 2, wakahamia Dar es Salaam mpaka walipofariki. Hapa Dar ndio tuna nyumba 3 na fremu za biashara. Wazazi wangu ni wazaliwa wa Tarime mkoani Mara. Mimi kwetu ni wapi?
 
Dar ndiyo kwako!
 
Hii mada imejaa hasira!!Any way kwa mtazamo wangu kila mtu ana kwao na kwake na panaweza kuwa tofauti,kwangu siyo lazima pawe kwetu.
 
hata kama nikizaliwa kibondo, kigoma....mimi bado ntakuwa mchaga na kwetu kutakuwa moshi...acha niwe mjima...
 
Back
Top Bottom