Watanzania tuwe na uzalendo tafadhali!

mtingi1

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
945
923
Wasalaam,

Nimekutana na matangazo ya ya vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya covid19 nimechoka,

Barakoa 1@2000?
Sanitaiza 250ml@10,000?
Sanitaiza 100ml@5,000?

Sisi wenye vipato vidogo tutamudu kweli?

Hii ni kwa MUJIBU wa utafiti mdogo, sijui kwako ulipo mwanaJF.

Kama bei hizi zimeenea sehemu kubwa ya nchi ni balaa kwetu.

WITO KWA SERIKALI.

Ikiwa vifaa tiba hivi vinalipishwa kodi basi visamehewe ili viuzwe kwa bei nafuu zaidi tutakayoimudu wenye vipato vidogo.

WITO WANGU KWA WAFANYA BIASHARA

Huu sio muda wa kujipatia faida kubwa katika bidhaa hizi zinazohitajika kwa wingi sasa

Tuonyeshe uzalendo, kwa kusaidiana katika kipindi hiki taifa linakabiriwa na hii changamoto ya covid19.

Mungu ibariki Tanzania .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom