Watanzania tuwe makini kuhusu matukio

Watanzania tuwe makini kuhusu matukio

donniebrasco

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
887
Reaction score
775
Mandela aliwahi kuulizwa kuhusu uhusiano wake na Gaddafi, Yaseer Arafat na Fidel Castro akajibu kuwa wale ni marafiki zake ni watu waliowasaidia wakati wa shida sana na akasema wasilazimishe maadui zao kuwa maadui zake, Vilevile Nyerere alikuwa hawaamini sana USA na wenzake.

Sasa kama wewe ni mtu wa uelewa hata kidogo tu utaona jinsi viongozi wazalendo hai bila kujali dini zao walikuwa hawawaendekezi USA na wenzake, USA wanaweza kufanya ubaya wowote ili tu wapate watakayo, sasa kuna ndugu zangu wengi hata humu ambapo huwa tunaamini kila kinachosemwa na hawa jamaa tutaambiwa Wachina wabaya , Warusi wabaya , Wahindi wabaya , Wairan wabaya, Wajapan wabaya. Waislamu wabaya, Sasa mi naomba niwakumbushe tu kwa haraka ubaya wao hao Mabomu ya nuclear Japan, Vita Vietnam, Vita Iraq, Vita Afghan, Vita Libya, Vita Syria. Wametengeneza makundi ya kigaidi duniani kama ISIS. Wamevuruga amani ya dunia,

Tanzania tuwe makini sana tusikubali kuletewa fitna za kijinga kuwa nchi yetu ina "ugaidi" huo wanaoutaka tuuelewe tuwe makini kuhusu matukio yaliyotokea, yanayotokea, na labda yatakayotokea. Tuangalie nchi yetu tumeishi kwa amani bila chuki hizo za dini.

Matukio yanaweza kutengenezwa wakalipwa baadhi ya watu wakalipue makanisa au misikiti halafu taratibu huwa chuki zinapandikizwa na silaha wanayoitumia kubwa ni pesa na ujinga wa wenyeji walengwa.

Nawasihi sana tuwe makini sana kuchunguza matukio hawa jamaa wako hapa nchini wakishirikiana na sisi katika maeneo mbali mbali ikiwemo kijeshi.

Siamini kama USA wana uadui na Tanzania kwa namna yoyote lakini tuwe makini sana sababu ya historia ya mambo waliyoyafanya na wanayoyafanya kwa wengine.

Mbinu za kutengeneza matukio kwao ni kitu kidogo tu ili baadae yawe ambayo watakayotaka tuwe makini sana kila mtu kwa nafasi yake kama ikitokea, asikubali kudanganywa au kushawishiwa kushiriki uovu huo.

Pia ushawishi unaweza kupitishwa hata kupitia vikundi vinavyojiita vya kidini hata kutokea nchi nyingine za jirani na kuwadanganya vijana wetu.
Tujitahidi kuelimishana ili vijana wetu wasije wakarubuniwa.

Na pia na sisi kwa ujumla wetu tusiwe watu wa kushangilia chuki zikipandikizwa tukumbuke tulikotoka na tujifunze kutoka kwa yaliyowakuta.

Mungu Tulinde na Utubariki Watanzania.
 
Amina mkuu, umenena vizuri sana.

Naamini na wengine watakuelewa pia!!
 
Mbona hayo uliyosema hayapo sasa au unamaanisha kuhusu makinikia?!
Mkuu sijasema kuna kitu kipo nimesema tuwe makini na matukio kwa mfano nimesoma sasa hivi kuna mtu kapost kuwa magaidi 11 wamekamatwa kibaha au wametajwa sasa inatakiwa tuwe makini Na mambo huwa yanaanza taratibu, mfano mwingine mwaka jana kuna waislamu walikatwa na mapanga msikitini mwanza wengine walikufa wengine walijeruhiwa, polisi kuuliwa na kunyanganywa silaha, sasa haya mambo hayakuwa kawaida yetu lazma tuumuze vichwa kuchukua tahadhari na kuhoji vizuri taarifa sio kuziaamini tu.
 
Wamerakani hawana shida na Tanzania yako mkuu.

Watanzania wenyewe tu Kuna mambo wanaiga yanayotokea huko ktk nchi zingine na baadhi wanapenda yatokee hapa nchini.

Mfano kwa Waislam kuongozwa na Bakwata wengine hawataki kabisa kusikia na wako radhi kufanya lolote Kulikoni kuongozwa na Bakwata

Kuna wengine suala la michanganyo na makafiri ni kuweka unajisi kwao Haya mambo yako wazi underground lakini yanakua taratibu ingawa zamani hatukuishi kabisa.

Serikali inatumia akili ya ziada sana kuhakikisha hali ya amani inaendelea kuwepo na kudhibiti kabisa utengano na hawa radicals.

Radicals popote pale duniani ni hatari sana.
 
Wamerakani hawana shida na Tanzania yako mkuu.

Watanzania wenyewe tu Kuna mambo wanaiga yanayotokea huko ktk nchi zingine na baadhi wanapenda yatokee hapa nchini.

Mfano kwa Waislam kuongozwa na Bakwata wengine hawataki kabisa kusikia na wako radhi kufanya lolote Kulikoni kuongozwa na Bakwata

Kuna wengine suala la michanganyo na makafiri ni kuweka unajisi kwao Haya mambo yako wazi underground lakini yanakua taratibu ingawa zamani hatukuishi kabisa.

Serikali inatumia akili ya ziada sana kuhakikisha hali ya jamani inaendelea kuwepo na kudhibiti kabisa utengano na hawa radicals.

Radicals popote pale duniani ni hatari sana.
Nakubali kweli unalosema kidogo lipo lakini hata hao radicals unaowa-refer ni kutokana directly au indirectly na USA kutokana na sources mbali mbali mpaka kuwafund na kuwatrain kwa muda atakaotaka wamsaidie akiwa anatayarisha akili mbovu na ufisadi aidha akijua au kutojua wengine wanaweza kuiga
 
Suala si kutokuwaamini tu.ni kuwa ni uwezo wa kiitelijensia kupambana nao.bahati nchi karibu zotewana intelijensia kwa ajili ya mambo ya kisiasa si kiulinzi au kiuchumi
 
USA hawezi pigana vita ambayo haina manufaa kwake, akija Tanzania ujue kuna kitu apa anakitaka,
 
USA wamesema TZ kuna ugaidi? Una ushahidi gani kwamba wao Ndo wametengeneza makundi ya ugaid? Hizo nchi zenye ugaidi hazijui kwamba USA ndo chanzo hadi wewe uliopo Ileje unajua ila wao hawajui tu? Hivi Leo nikikupa bunduki nikikwambia muue ndugu yako na wewe ukamuua hapo mjinga nani mimi au wewe? Chukueni full responsibility ya matendo yenu sio kila kitu USA
 
Mkuu sijasema kuna kitu kipo nimesema tuwe makini na matukio kwa mfano nimesoma sasa hivi kuna mtu kapost kuwa magaidi 11 wamekamatwa kibaha au wametajwa sasa inatakiwa tuwe makini Na mambo huwa yanaanza taratibu, mfano mwingine mwaka jana kuna waislamu walikatwa na mapanga msikitini mwanza wengine walikufa wengine walijeruhiwa, polisi kuuliwa na kunyanganywa silaha, sasa haya mambo hayakuwa kawaida yetu lazma tuumuze vichwa kuchukua tahadhari na kuhoji vizuri taarifa sio kuziaamini tu.
Kwahiyo wamarekani hawana shida na Tz yako ?

Huu unaweza kuwa uchochezi pia
 
USA wamesema TZ kuna ugaidi? Una ushahidi gani kwamba wao Ndo wametengeneza makundi ya ugaid? Hizo nchi zenye ugaidi hazijui kwamba USA ndo chanzo hadi wewe uliopo Ileje unajua ila wao hawajui tu? Hivi Leo nikikupa bunduki nikikwambia muue ndugu yako na wewe ukamuua hapo mjinga nani mimi au wewe? Chukueni full responsibility ya matendo yenu sio kila kitu USA
Ndugu hilo ndilo nalolisema nakupa mfano kuna tukio lilitipotiwa duniani kuwa magaidi wameshambulia baa ya mashoga Orlando naomba fuatilia uone uongo huo na ukatangazwa dunia nzima kupitia CNN , BBC,Al-Jazeera na vyombo vyote nakuomba wewe ingia mtandaoni uone wananchi wa huko huko kwao walivyowaumbua kuwa kulikuwa hakuna tukio hilo kabisa walitengeneza tukio zima kimaigizo halafu hadi Obama akaenda kuweka maua na kuomboleza msiba feki YouTube fuatilia uone uongo wao walivyofanya maigizo hawa watu ni hatari sana Hata haya mabomu yaliyopigwa manchester juzi juzi hakuna ushahidi ni kutengeneza uongo tu yaani wanajitahidi kila mbinu mengine wanaua watu kweli mengine wanaigiza halafu wanauimba uongo mpaka ukuingie akilini tena huwa wanaimba pamoja CNN,BBC, Sky,Al-Jazeera
 
Kwahiyo wamarekani hawana shida na Tz yako ?

Huu unaweza kuwa uchochezi pia
Naona bado hujanielewa kwa mfano isitokee kundi la watu wakasema waliokamatwa na polisi wameonewa ili kutupotosha na tukawaamini na pia polisi au serikali isitokee ikawaonea baadhi ya watu pia tukawaamini kirahisi pia wasitokee watu kuturubuni kuchafua amani tukawaakubalia yaani kila wakati tuwe makini na kila kinachotokea inataka kujitambua na kusaidia kuelimishana. Na sisemi USA ni adui yetu hapana. Nachosema tuwe makini tusijisahau na tujifunze kutoka kwa yaliwakuta,mambo huanza taratibu tukizubaa tu nchi inaweza kuwa mbaya mungu atuepushie mbali
 
Ndugu hilo ndilo nalolisema nakupa mfano kuna tukio lilitipotiwa duniani kuwa magaidi wameshambulia baa ya mashoga Orlando naomba fuatilia uone uongo huo na ukatangazwa dunia nzima kupitia CNN , BBC,Al-Jazeera na vyombo vyote nakuomba wewe ingia mtandaoni uone wananchi wa huko huko kwao walivyowaumbua kuwa kulikuwa hakuna tukio hilo kabisa walitengeneza tukio zima kimaigizo halafu hadi Obama akaenda kuweka maua na kuomboleza msiba feki YouTube fuatilia uone uongo wao walivyofanya maigizo hawa watu ni hatari sana Hata haya mabomu yaliyopigwa manchester juzi juzi hakuna ushahidi ni kutengeneza uongo tu yaani wanajitahidi kila mbinu mengine wanaua watu kweli mengine wanaigiza halafu wanauimba uongo mpaka ukuingie akilini tena huwa wanaimba pamoja CNN,BBC, Sky,Al-Jazeera

You're delusional. Nipo USA na tukio la Orland lilitokea kama unabisha na hilo Sina sababu ya kuendelea kubishana na wewe. Sio kila kitu sababu mtu kaweka YouTube kwa sababu zake binafsi unaamini, wadanganye watu wameuwawa kwa faida ya nani? Ili nini kitokee? Sahizi unapinga na tukio la Manchester sio kweli, really!!

YouTube haiwi filtered so mtu anaweka chochote hata Mimi Leo naweza kuweka video YouTube kwamba Hakuna mauaji kibiti na wajinga kama wewe wataamini ila hiyo haiondoi ukweli kwamba Kibiti kuna mauaji yanaendelea.

Kuna mengi sana yanaendelea USA shootings zipo kila siku hizo ulizosikia ni chache tu sababu zilikua mass shootings, Leo city yangu kuna watu wameuwawa na haipiti mwezi bila watu kufumuana kwenye miji huko, Jana San Francisco mtu kaenda kuua watu post office ambayo husikii na hizo utasema wamesababisha wenyewe ili iweje?
 
Kwani ukiwa USA ndo nini tena watu wa huko ndo shida kweli mnadanganywa kama watoto video na news kibao tunasoma watu wanaishi orlando hapo hapo wameyaumbua hayo maigizo na ukitaka ni kutolee links hapa
 
Boy bye.
 
Back
Top Bottom