Seneta Wa Mtwiz
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 3,622
- 4,138
Maombi yenu wakuu,
Majuzi mama mwenye nyumba hapa nilipopanga kawapa kazi wanawake watatu wa kikurya kutoka tarime.
Ni kazi ya kulima eneo la heka 4,
Na kubeba tofali kama 900 hivi,
Pamoja na kugonga kokoto tani 3,
Kujaza maji simtaki la lita 1500,
Kisha kung'oa visiki vya miembe
Na kutibua matuta makubwa ya viazi.
Na akanikabidhi hela waliyopatana ili niwakabidhi wakishakamilisha kazi zote,
Huku akinisisitiza kuwa
" #seneta_wa_mtwiz,
Hakikisha unawakabidhi hawa akina mama kwa wakatinwakishamaliza."
Kutokana na kazi zinavyoadimika kipindi hiki hawa akina mama wamepiga job wiki nzima kuanzia alfajiri hadi usiku jua liliwawakia na mvua ziliwanyeshea ila hawakupumzika mpaka walipomaliza leo hii.
Sasa nd'o wamekuja kwangu kuchukua hela sasa hivi.
Kiukweli mimi nilidhani ile kazi ingechukua kama miezi miwili, hivyo ile hela nikawa nimeiwekeza kwenye mradi kubeti mechi za ulaya ili izae ila mpaka sasa mikeka yote imechanika na hela yote imeisha na hawa akina mama waliambiwa na kushuhudia kabisa pindi nikikabidhiwa hela yao ambapo wakimaliza waje kwangu niwape yote.
----------
Sasa wakuu,
Nitumie mbinu gani ya kuwapiga sound hawa akina mama ili wawe wapole na wasubiri angalau hadi mwisho wa mwezi ujao?
Nimeganda hapa nusu saa natafakari na huko nje nasikia wanazungumza maneno flani ya kikurya, ingawa sielewi maana yake ila kwa mizuka ya sauti zao naona kama yanaashiria uvunjifu wa amani maeneo haya.
Kwa wenyeji wa Tarime, nipeni saikolojia yao kidogo ili niwatulize jazba kwa maneno laini na ya kukonga nyoyo.Maana'ke wamekuja na majembe, wananisubiri hapo nje niwape hela muda huu.
Maombi yenu wakuu