Watanzania: Tusiogope mabadiliko, yanakuja

Watanzania: Tusiogope mabadiliko, yanakuja

Hapa hakuna kiongozi anayeweza kuamsha na kuongoza hayo unayoyataka. Angekuwepo, tungekwishaona dalili na kumpa 'support.'

Sasa hivi hakuna na muda uliopo, hategemewi mmoja aote kama uyoga na kuanza kukoga nyoyo za watu hadi kufanuikisha hayo unayoyaandika hapa...
Haya na Lissu na Mbowe ndio hivyo walishavunjwa miguu.
 
Haya na Lissu na Mbowe ndio hivyo walishavunjwa miguu.
Mkuu, CHADEMA wanadai wana wanachama wao, sijui idadi yao ni wangapi, na pia wanasema kuna wapenzi wa chama hicho ambao pia idadi yao haijulikani. Ongeza na waTanzania wanaopenda mabadiliko, kuondokana na ukoloni wa CCM, nao wapo wengi tu, idadi ya wote kwa jumla haiwezi kukosa kuwa mamilioni ikiwa ni pamoja na wanachama wa vyama vingine vya upinzani - wapo watu wa kutosha kabisa kukataa kuendeshwa kama mifugo.

Hawa wote wanahitaji uongozi tu wa kusimamia na mpangilio mzuri wa kuyatafuta mabadiliko hayo. Wangeonyeshwa 'progam' nzuri ya kuyapigania mabadiliko hayo hakuna serikali ambayo ingekataa kutekeleza matakwa hayo, kama ya kuwa na tume huru na mambo mengine mengi ya unyanyasaji yangekoma.

Hakuna viongozi wa aina hiyo hadi sasa.

Mbowe alijaribu, akajikuta anaishia Segerea na kikundi chake bila ya wananchi..., ambao baadae ilibidi wamchangie kumtoa jela, lakini sio kusimama naye pale Kinondoni kudai haki, na hizo tume na mengine mengi..., ajiulize yeye pamoja na viongozi wenzake ndani ya chama, kwa nini iko hivyo.

Ninahakika wakijua mwelekeo wa wananchi ulipo, itawawia rahisi kuwahimiza wananchi wayalete mabadiliko wanayoyataka.
 
Kuiondoa CCM siyo wazo baya angalau kinadharia lakini tatizo sisi wananchi tunaangalia Chama mbadala cha kurithi mikoba ya CCM tunakosa kabisa, Vyama vya upinzani vimekuwa legelege na havina consistency kwenye malengo ya kukamata dola, vinazidiwa mikakati na mbinu na CCM na kubaki kulalamika muda wote badala ya suluhisho jadidi(practical solution).

Siasa ni sayansi na ni taaluma ni budi kujipanga vizuri na kufanya uchambuzi wa kubaini uwezo , udhaifu na fursa ya chama husika yaani kufanya SWOT analysis.CCM wako vizuri kwa hilo. Na hubadilisha mbinu kila wakati mithili ya kinyonga.

Upinzani jiongezeni sana badala ya kulalamikia vyombo vya dola na sababu nyinginezo someni mchezo na kufanya tathmini ya ndani (self assessment.) Na kisha muwe focused. Vinginevyo wacha CCM iendelee kutawala wananchi hawawezi kuitoa kwa mazingira ya ku risk. VIVA CCM !
 
Watu wakiamua kuzivaa watakamata wangapi? Wataua wangapi? Usicheze na NGUVU ya UMMA pale wanapoamua kwamba tumechoka LIWALO NA LIWE! Idadi ya Polisi nchini ni ndogo sana kulinganisha na idadi ya Watanzania. TUME HURU ya Uchaguzi ni haki yetu Watanzania wala si hisani kutoka kwa yeyote yule.
Ndoto ya miaka mitano. Mwisho wake kumekucha hakuna mabadiliko. Kilichopo ni CCM bora zaidi. Kila kona umma umekubali CCM inafanya .
 
Kuiondoa CCM siyo wazo baya angalau kinadharia lakini tatizo sisi wananchi tunaangalia Chama mbadala cha kurithi mikoba ya CCM tunakosa kabisa, Vyama vya upinzani vimekuwa legelege na havina consistency kwenye malengo ya kukamata dola, vinazidiwa mikakati na mbinu na CCM na kubaki kulalamika muda wote badala ya suluhisho jadidi(practical solution). Siasa ni sayansi na ni taaluma ni budi kujipanga vizuri na kufanya uchambuzi wa kubaini uwezo , udhaifu na fursa ya chama husika yaani kufanya SWOT analysis...
Mambo hayaendi namna hiyo kwa SWOT n.k. Inashangaza msomi kama wewe kushindwa kuelewa kuwa watu wanapaswa kupewa nafasi ili waweze kufanya kazi badala ya kusubiri huku mkiwadhibiti kwa mbinu chafu za kuwafunga kamba na kuwavunja miguu. Wakoloni wangeangalia kwamba akina Nyerere wangeweza pengine tusingepata uhuru hadi 2090. Hivi kweli unaulaumu upinzani kwa kuzidiwa "ujanja" na ccm? na hivyo hatuwapi kura kwani mmezidiwa ujanja na ccm? eehheeee!
 
Kuiondoa CCM siyo wazo baya angalau kinadharia lakini tatizo sisi wananchi tunaangalia Chama mbadala cha kurithi mikoba ya CCM tunakosa kabisa, Vyama vya upinzani vimekuwa legelege na havina consistency kwenye malengo ya kukamata dola, vinazidiwa mikakati na mbinu na CCM na kubaki kulalamika muda wote badala ya suluhisho jadidi(practical solution). Siasa ni sayansi na ni taaluma ni budi kujipanga vizuri na kufanya uchambuzi wa kubaini uwezo , udhaifu na fursa ya chama husika yaani kufanya SWOT analysis.CCM wako vizuri kwa hilo. Na hubadilisha mbinu kila wakati mithili ya kinyonga. Upinzani jiongezeni sana badala ya kulalamikia vyombo vya dola na sababu nyinginezo someni mchezo na kufanya tathmini ya ndani (self assessment.) Na kisha muwe focused. Vinginevyo wacha CCM iendelee kutawala wananchi hawawezi kuitoa kwa mazingira ya ku risk. VIVA CCM !
Kimsingi ninakubaliana na wewe katika haya uliyoandika hapa.

Kitu au jambo linalotatiza ni hili: je hakuna ukomo ambao wananchi wataona wanayofanya CCM ni heri waondoke wajaribu angalau kwa miaka mitano kuwapa nafasi wapinzani, na kama ikionekana uwezo wao ni mbovu zaidi wawaondoe na ikilazimu wawarudishe hao CCM ambao pengine watakuwa wamekwishapata funzo la kuwekwa pembeni?

Itakuwaje siku zote kuamini tu kwamba wapinzani hawawezi bila hata ya kuwajaribu?

Sasa angalia janga linaloinyemelea nchi ; hata hiyo CCM sio CCM tena kama tulivyoizoea na ubovu wake. Sasa ni CCM ya mtu, anayetumia tu jina la chama, na anajenga misingi ya kutoweza kumwondoa hapo alipo kwa kura au kwa njia nyingine yoyote! Hili sio janga la nchi?
 
Ni kweli mabadiliko tunayataka sana, lakini fikilia wagombea wanaoletwa na upinzani!!

Lakini pia fikilia, kama hao wapinzani wananunuliwa hii ina maana wanapenda pesa zaidi ya utu wao, vyama vyao na hata nchi yao. Je tukiwakabidhi nchi si watanunuliwa wao, watatuuza wananchi wote na watauza mali asili zetu zote!!

Viongozi wakuu wanalewa mpaka wanavunjika miguu, wakipewa nchi si watarudisha viroba ili wananchi wote tulewe tuvunjike vichwa!!
Mkuu hao unaodai walinunuliwa, mnunuzi alikuwa nani, na baada ya kununuliwa mnunuzi aliwafanya nini? Aliwachinja? Aliwauza? Aliwatunuku? Hebu tujuze hatima ya walionunuliwa.
 
Maccm hawana hati miliki ya Tanzania, Tanzania ni yetu sote kama haturidhiki na utawala wa kidikteta uliojaa udhalimu ni lazima tuseme hadharani bila WOGA wala KIFICHO. Tanzania ni yetu sote.

Nani aliyetegemea Mkapa aliyewahi kuwaita Wapinzani MALOFA iko siku ataongea kauli moja na upindani!?

#WATATUELEWATU

Mkuu kuiondoa CCM madarakani ni pale CCM wenyewe wakiamua kuondoka na kuweka chama mbadala!!Waamue wenyewe na sio vinginevyo!!
 
Hujui! Jibu ni kwamba huwatumia atakavyo.
Hee..?! Hapo tena! Hiyo kali. Kwani wakubwa hilo hawajaliona au wamelifumbia macho, kwamba iwe funika kombe mwanaharamu apite...!
 
Mkuu hao unaodai walinunuliwa, mnunuzi alikuwa nani, na baada ya kununuliwa mnunuzi aliwafanya nini? Aliwachinja? Aliwauza? Aliwatunuku? Hebu tujuze hatima ya walionunuliwa.
Muulize mnaedai anawanunua atakuwa na jibu sahihi. Kumbuka wanaodai wanachama wao hasa wabunge na madiwani wananunuliwa ni wapinzani na siyo CCM.
 
2451474_EcRD_1vXQAAFZJs.jpg
Mnakumbuka shuka kumekucha? Tena kwa kuamshwa na askofu?

Subirini tu kipigo
 
Suala si tu kubadilisha vyama vikongwe....kwani hata vikibadilishwa huwa vinaweza kurudi Tena baada ya miaka mingi kupita.

Kwa hiyo wala WANANCHI hawana Mchoko wa rangi ya Chama Tawala kama unavyotuaminisha hapa.

Agenda ya WANANCHI ni mabadiliko ya kweli km WANAVYOYASHUHUDIA kipindi hiki Cha awamu ya 5.

Agenda ya WANANCHI ni kuondoa sintofahamu ya kuitafuna nchi kipapa kunakofanywa na maOLIGARCHS.

Ukiiona nchi yoyote RAIS wake anaanza kupambana na mfumo kizingiti wa RUSHWA KUBWAKUBWA kwa UNTOUCHABLE ELITE-oligarchs AMBAO wako katika chama chake ujue hapo UKO katika nchi SALAMA.

Magufuli ameshayafanya hayo.
ANAENDELEA kuyafanya kwa FAIDA ya taifa hili.

Majirani zetu Malawi walikiondoa chama kikongwe baada ya kupoteza udhibiti wake DHIDI YA RUSHWA ZA KIPAPA za watendaji wa serikali YAKE.

Miaka mingi baadae CHAMA KILEKILE kimerudi Tena.....wamekirudisha kupitia mchungaji Chakwera.

Kwa hiyo narudia tena kusema kwamba wamalawi WALIWACHOKA WATU WALIOWAAMIMI ktka hcho chama,Almanusra kapatikana MUAMINIFU CHAKWERA(km magufuli) na hatimaye WAMEMCHAGUA kupitia chama KILEKILE kikongwe KALAGHABAHO!!
so unamini Magu muaminifu?tuna safari ndefu Sana na swali butu je Kama amefanya mengi mazuri kwann anahofia Sana wapinzani hata mpk anafanya mwenyewe siasa?
 
Muulize mnaedai anawanunua atakuwa na jibu sahihi. Kumbuka wanaodai wanachama wao hasa wabunge na madiwani wananunuliwa ni wapinzani na siyo CCM.
Hujanijibu niliyotaka kuyajua.
 
so unamini Magu muaminifu?tuna safari ndefu Sana na swali butu je Kama amefanya mengi mazuri kwann anahofia Sana wapinzani hata mpk anafanya mwenyewe siasa?

Kweli ni MUAMINIFU.....

Hahofii Wapinzani Bali Anaujua Unafiki wa waafrika wengi Ktka kutafuta FURSA wanaweza kutumia NJIA za kificho Cha "siasa za demokrasia" kukwaza MALENGO MAKUBWA YA NCHI.....

Yuko sahihi Mia fil mia....

Cha Chakwera Wa Malawi Ni Ushahidi Tosha kuwa WAPINZANI WA AFRIKA WAKO KIFURSA TU KUFANIKISHA malengo ya KIUONGOZI kwa kutumia hila na mbinu yoyote.....
 
Kimsingi ninakubaliana na wewe katika haya uliyoandika hapa.

Kitu au jambo linalotatiza ni hili: je hakuna ukomo ambao wananchi wataona wanayofanya CCM ni heri waondoke wajaribu angalau kwa miaka mitano kuwapa nafasi wapinzani, na kama ikionekana uwezo wao ni mbovu zaidi wawaondoe na ikilazimu wawarudishe hao CCM ambao pengine watakuwa wamekwishapata funzo la kuwekwa pembeni?

Itakuwaje siku zote kuamini tu kwamba wapinzani hawawezi bila hata ya kuwajaribu?

Sasa angalia janga linaloinyemelea nchi ; hata hiyo CCM sio CCM tena kama tulivyoizoea na ubovu wake. Sasa ni CCM ya mtu, anayetumia tu jina la chama, na anajenga misingi ya kutoweza kumwondoa hapo alipo kwa kura au kwa njia nyingine yoyote! Hili sio janga la nchi?

Kalamu1

Nimekuelewa Sana...
Pia inabidi jamii ielewe nadharia ya kisiasa ya mabadiliko.. yatagusa vipi jamii na sera mpya zitakazo leta mabadiliko na maendeleo..

Vyama vya upinzani wanatakiwa sio kukosoa hotuba au kupinga maamuzi wanapaswa kuiambia jamii Ni Nini wataleta baada ya kuchukua madaraka...
 
Back
Top Bottom