Watanzania: Tusiogope mabadiliko, yanakuja

Watanzania: Tusiogope mabadiliko, yanakuja

Ni kweli mabadiliko tunayata sana, lakini fikilia wagombea wanaoletwa na upinzani!!

Lakini pia fikilia, kama hao wapinzani wananunuliwa hii ina maana wanapenda pesa zaidi ya utu wao, vyama vyao na hata nchi yao. Je tukiwakabidhi nchi si watanunuliwa wao, watatuuza wananchi wote na watauza mali asili zetu zote!!

Viongozi wakuu wanalewa mpaka wanavunjika miguu, wakipewa nchi si watarudisha viroba ili wananchi wote tulewe tuvunjike vichwa!!

Naunga mkono hoja
 
Dhana potofu kabisa, pamoja na kwamba nilikubaliana na mengine uliyoweka kwenye mada yako.
Ni wapi Afrika ambako hapakuwa na ujamaa pamebadilika zaidi ya ilivyobadilika Tanzania. Wote hao walikuwa na ujamaa?

Unapoimbishwa wimbo, jaribu kuelewa maana yake usiimbe tu wimbo kama kasuku.
Nchi zote zilizochukua mfumo wa kijamaa duniani siku hizi ndizo nchi maskini zaidi hili linajulikana na watu wote. Rejea nchi za Amerika ya Kusini, Ulaya ya Mashariki, Asia, nk Huu mfuno bado upo hata kama hatujitangazi, mfumo wetu bado ni huo kivitendo. Tubadilike tusisubiri Nyerere aje kutoshauri tuachane na siasa zisizo na tija.
 
Aiseee, achana na hili ndani ya mada yako, unaivuruga.

Kama unataka anza nyingine hili lijadiliwe huko. Inaelekea bado upo usingizini sana kuhusu hili.
 
Kununuliwa wabunge wa upinzani analalamika JPM?

Basi sawa wewe endelea kusifia ushoga wa Lissu na ulevi wa Mbowe
Hivi wewe kweli unamini Lissu anatetea ushoga au Mbowe ni mlevi? Ndio maana nasema propaganda za ccm zimewaingia sana na hata hamjui hilo.
 
Ni kweli mtoa mada, mabadiliko ya kweli yatakuja pale CCM itakapoondoka madarakani. Haiwezekani mfumo huo huo unaongoza kwa zaidi ya nusu karne alafu tutegemee mabadiliko. No way..
 
Najuta sana wajukuu wangu watanicheka kwa kutawaliwa na chama kimoja zaidi ya miaka 50 aibu kubwa sana.
Vijana tuamke hakuna nyuvu ya umma imewahi shindwa
 
Usiongee kama KASUKU huu uchaguzi unaangaliwa pia na JUMUIYA mbali mbali za KIMATAIFA. Usidhani Tanzania ni KISIWA ambacho UDHALIMU unaweza kukithiri huku jumuiya za kimataifa na nchi za Wafadhili zikikaa kimya. Wakifanya yale mnayoyapenda hamkawii kuwaita NCHI ZA WAFADHILI lakini wakionyooshea kidole UDHALIMU na DHULMA zinazoendelea Nchini basi mnageza kauli na kuwaita MABEBERU. Tia akili kichwa so that you can think OUTSIDE THE BOX.
Well....jumuiya ya KIMATAIFA haingilii Mambo ya ndani ya SOVEREIGN states mpaka kuwe na madhila makubwa kutishia uhai wa wananchi...

Museveni AMEKUWA akiitwa dikteta kwa jinsi anavyowapelekapeleka wapinzani wake...Wala hajanyimwa hiyo MISAADA USEMAYO......

UHURU Kenyatta pamoja na mtangulizi wake aliyeapishwa IKULU na Mwenyekiti wa tume kuikimbia nchi Wala HAWAJANYIMWA HIYO MISAADA sanasana OBAMA ameCement UHUSIANO na Kenya..

Pamoja na kuwa Kenyatta na Rutto walikuwa charged na Hague kutokana na vile VIFO VYA WATU ZAIDI YA ELFU MOJA,hatujaona wakiwekewa TRAVEL BAN NA ECONOMIC EMBARGO.

KAGAME the same. Burundi iliingzwa BLACK BOOK kwa sababu ya shinikizo pia kutoka kwa kamanda Kagame(rafiki wa US) na pia CNDD-FDD haipendelewi na RPF ya Rwanda.

Zimbabwe imekaangika kwa sabb ya sera ya kuyachukua mashamba ya walowezi wa KIINGEREZA(conflict of interest).

Kongo inaendelea kutaabika Wala hawajawekewa INTERNATIONAL RESTRICTIONS.

KIUKWELI MNAYOYADAI YANASHANGAZA KUSIKITISHA KUCHEKESHA na wakati mwingine KUCHUSHA.
 
Inawezekana ni sisi watanzania kuwa jasiri na wenye akili kwani woga umezidi.
Naona huna umakini na mada yako.

Ni mada mhimu lakini unajipigia tu bora liende.

Wakati huu unataka kufanyike nini ili kuwezesha hiyo tume huru kuwepo kabla ya uchaguzi mkuu?
 
Naona huna umakini na mada yako.

Ni mada mhimu lakini unajipigia tu bora liende.

Wakati huu unataka kufanyike nini ili kuwezesha hiyo tume huru kuwepo kabla ya uchaguzi mkuu?
Tuache woga tuingie mtaani tudai tume huru na hiki kiwe kigezo au sharti la uchaguzi mkuu October. Bila tume huru tusishiriki. Wewe unapenda tume huru au ndio wale wa lolote na liwe ilimradi nakula ugali.
 
Well....jumuiya ya KIMATAIFA haingilii Mambo ya ndani ya SOVEREIGN states mpaka kuwe na madhila makubwa kutishia uhai wa wananchi...

Museveni AMEKUWA akiitwa dikteta kwa jinsi anavyowapelekapeleka wapinzani wake...Wala hajanyimwa hiyo MISAADA USEMAYO......

UHURU Kenyatta pamoja na mtangulizi wake aliyeapishwa IKULU na Mwenyekiti wa tume kuikimbia nchi Wala HAWAJANYIMWA HIYO MISAADA sanasana OBAMA ameCement UHUSIANO na Kenya...
LOoo, mkuu nimekusikia (kusoma) unavyowika hapa!

Hakika mifano uliyoitoa kujenga hoja inapiga penyewe hasa na kuweka matumaini kwa hao wanaotukandamiza kuendelea kukandamiza bila uoga, kwa kujua hizo kelele zetu hata wakizisikia walio nje hazisaidii kitu. Hii inawapa nguvu sana wazidi kukandamiza.

Binafsi naikubali sana hiyo mifano uliyoweka ndio maana huwa sina tegemeo la mabadiliko yatoke nje ya nchi.

Mabadiliko ni yetu kuyaleta, hao wa nje hatuwezi kuacha kuendelea kuwapigia makelele huku tukitafuta njia zetu sisi wenyewe za kutondoa kwenye ukandamizaji.
 
Mabadiliko labda ya hali ya hewa ila sio mabadiliko ya kuitoa CCM madarakani.
 
Tuache woga tuingie mtaani tudai tume huru na hiki kiwe kigezo au sharti la uchaguzi mkuu October. Bila tume huru tusishiriki. Wewe unapenda tume huru au ndio wale wa lolote na liwe ilimradi nakula ugali.
Hapa hakuna kiongozi anayeweza kuamsha na kuongoza hayo unayoyataka. Angekuwepo, tungekwishaona dalili na kumpa 'support.'

Sasa hivi hakuna na muda uliopo, hategemewi mmoja aote kama uyoga na kuanza kukoga nyoyo za watu hadi kufanuikisha hayo unayoyaandika hapa.

Hili limekwishapitwa na wakati wake, ndio maana CCM haliwasumbui tena na kulipa muda wa kuliwazia.

Wapinzani wamekubali kuingia kwenye uchaguzi, hawasemi chochote, wako kimya na wametulia kabisa kama wanajua wanachokifanya ambacho wana uhakika wananchi watakitambua na kukikubali ifikapo wakati wake.

Au ndio basi, wamekwishakubali matokeo ya uchaguzi mkuu unaokuja na hawana la ziada wanaloweza kufanya kubadili mwelekeo wake.

Hawasemi kitu. Wametulia tuli, kama maji ndani ya mtungi.
 
Nchi zote zilizochukua mfumo wa kijamaa duniani siku hizi ndizo nchi maskini zaidi hili linajulikana na watu wote. Rejea nchi za Amerika ya Kusini, Ulaya ya Mashariki, Asia, nk Huu mfuno bado upo hata kama hatujitangazi, mfumo wetu bado ni huo kivitendo. Tubadilike tusisubiri Nyerere aje kutoshauri tuachane na siasa zisizo na tija.
Sasa Nimeanza KUUFAHAMU uelewa wako vizuri.

Bwana fazili,Nyerere hakuacha UKOMUNISTI wala UJAMAA ule wa kina KARL MAX na wenzke.

Nyerere alitujengea UJAMAA was kiafrika.
NI ujamaa wa kipekee kabisa.

Sera za huo ujamaa wa kiafrika hasa KUHUSU uchumi zimebadilishwa pale alipong'atuka na kupendekeza vpengele vya SOKO HURIA......

Kwa hyo tuko na MISINGI ya huo ujamaa wa kiafrika na uchumi wa soko huria.

Nje ya hapo sijui unapendekeza sera zipi tuige na kuzirasimisha katibani TUBADILISHE Yale maneno "nchi ya ujamaa na kujitegemea"....
 
Ni kweli mtoa mada, mabadiliko ya kweli yatakuja pale ccm itakapoondoka madarakani.
Haiwezekani mfumo huo huo unaongoza kwa zaidi ya nusu karne alafu tutegemee mabadiliko. No way..
Umekariri.....aliyekwambia nusu Karne NI miaka mingi kakukaririsha wewe....
 
Sasa Nimeanza KUUFAHAMU uelewa wako vizuri....

Bwana fazili,Nyerere hakuacha UKOMUNISTI wala UJAMAA ule wa kina KARL MAX na wenzke........

Nyerere alitujengea UJAMAA was kiafrika......
NI ujamaa wa kipekee kabisa......

Sera za huo ujamaa wa kiafrika hasa KUHUSU uchumi zimebadilishwa pale alipong'atuka na kupendekeza vpengele vya SOKO HURIA......

Kwa hyo tuko na MISINGI ya huo ujamaa wa kiafrika na uchumi wa soko huria........

Nje ya hapo sijui unapendekeza sera zipi tuige na kuzirasimisha katibani TUBADILISHE Yale maneno "nchi ya ujamaa na kujitegemea"....
Naelewa ilikuwa African Socialism, lakini pengine ndiyo the poorest form of socialism kwani ilikuwa too idealistic and based on seeing poverty as a virtue. Hii ndio kitu mbaya zaidi iliyonasa kwenye bongo zetu hadi leo, poverty is virtue! Zamani ukiwa na nyumba mbili unaambiwa umepata wapi fedha? Ndio chanzo cha wachagga kuitwa wezi kwani walionekana kujikusanyia mali na hii iliwafanya waonekane wenye kupenda hela mno. Mfumo huu umeacha kovu kwa watanzania hadi leo.

Tunachopaswa kufanya sio tu ku-declare we are not a socialist nation, kwani hii haisaidii kitu, bali ni kubadilisha mifumo yetu ya kiuchumi na fikra. Kumiliki ardhi kubwa ni kikwazo hapa nchini. Bado kwenye makaratasi kuna sheria zinazomzuia mtu kufanya mambo kwa uhuru.

Serikali bado hadi leo inataka kufanya biashara! Angalia ATCL, Railway, Bandari, na hata siku hizi serikali imeanzisha vituo vya kuuza mafuta! Makosa makubwa, hayo achia sekta binafsi, serikali chukua share ndogo tu waachie watu binafsi undeshaji. ATCL imeshafeli watu wengi hawajui kwamba kilichobakia ni propaganda tu na usiri mkubwa.
 
Back
Top Bottom