Watanzania tusiogope mabadiliko. Tumekuwa katika mfumo wa CCM kwa zaidi ya miaka 60 sasa (1954-2020) actually kwa miaka 66 sasa mfumo CCM unatawala akili za watanzania. Mnataka CCM itawale kwa miaka mingapi? 100? Nchi zinazotuzunguka zote walishabadilisha vyama vikongwe vyote, ni sisi tu tumebaki na vitu vikuu kuu.
Mfumo uliopo ulitufaa wakati wa kupigania uhuru. Baada ya hapo mfumo huu ulikuja na siasa zisizofaa za kijamaa ambazo ndio zinaeleza kwanini Tanzania imekuwa moja kati ya nchi maskini zaidi duniani. Nyerere kwa kuwa muwazi aliona makosa yake na kuamua kujiuzulu kupisha mabadiliko.
Lakini cha ajabu watanzania hawakutaka mabadiliko hadi Nyerere mwenyewe akaamua kuwachagulia mfumo wa vyama vingi pamoja na ukweli kwamba asilimia 80 walitaka chama kimoja kiendelee.
Leo hii bado kuna watu ambao itabidi Nyerere aje awaambie sasa CCM basi chagueni chama kingine. Watanzania hata kama tunapata faida binafsi CCM tunapaswa kukubali mabadiliko. Au mpaka Nyerere arudi?