Watanzania tusinyamazie uovu kama huu

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Juzi nilisafiri toka DSM kwenda Mbeya, nilipofika Iringa nikataka kujaza mafuta gari. Hamadi..vituo vyote havina diesel, nikajaribu kuulizia kulikoni na kwa uchunguzi mdogo nikagundua vituo vitatu mjini au zaidi anamiliki yule tajiri wa maziwa ya ASAS dairies. Kuhusu kwa nini amefunga vijana pale wakanijuza:

Bei ya mafuta imepanda kwahiyo ameamua kufunga vituo leo ili kesho akifungua abadilishe bei mpya. Sikupata mafuta hadi nilipofika Mafinga nikapata kituo kimoja tu kinauza na hata nilipofika Mbeya ni kituo kimoja tu kiliuza mafuta na kweli kesho yake vituo vingi vilifugua vikiwa na bei mpya.

Iweje mafuta yaliyonunuliwa kwa bei ndogo kabla yachukue bei mpya? Hata kama soko la kimataifa lilibadilika kwanini wasipandishe mafuta yatakayoingia hapo baadaye? Na Iweje bei ilipotangazwa kushuka wafanyabiashara wote wakapinga? Ilihali bei ya mafuta ya taa kesho yake tu mafuta yale yalipanda?

Huu ni uhalifu ambao mimi sitaki tuunyamazie....na kama serikali ya CCM inashindwa kuuzuia ninawaomba wananchi tusinyamaze...kila mtu kwa nafasi yake, na tafadhali serikali mchukue tahadhari maana pia vituo vya mafuta na EWURA wanavyotesa wananchi wana faida gani?

Kama wananchi wataamua kuweka viberiti katika vituo hivi kuna ubaya gani kama vituo hivi havina manufaa kwao zaidi ya kuwaongezea machungu?. Mimi nimekerwa na kama ninyi pia mnakerwa mniunge mkono kupinga haya na mengine kama ya TANESCO.

Kama serikali imeshindwa kuwadhibiti hawa matajiri (Nasikia wakubwa na watoto wao wanamiliki vituo kama vya Lake Oil) basi nguvu ya wananchi tu itaweza kumaliza hili.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom