maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kuna uwezekano mkubwa kwamba serikali inatudanganya kuhusu makusanyo ya kodi ya shilingi trilioni 1.4 kwa mwezi Januari 2016 pekee na kujinasibu kwamba imevuka kusanyo lolote la kodi lililowahi kukusanywa katika kipindi cha mwezi mmoja.
Ninachoamini ni kwamba hakuna kusanyo lolote hapa la kushangaza wala kujitapia kwamba TRA imevunja rekodi kwa kukusanya kodi kubwa kwa mwezi mmoja, isipokuwa wasiojua wanapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Ilichofanya serikali ni kukusanya kodi ya nyuma iliyokuwa inakwepwa kulipwa kwa makusudi na uzembe kama ile ya makontena na kuirundika yote kwenye mwezi wa Januari na kuwadanganya watanzanzania kujitafutia sifa.
Kama kweli lengo limevukwa ebu hawa wanaojitapa watupe ushahidi na watuambie ni vyanzo gani vipya vya kodi vya uhakika walivyobuni kama si vile vile vilivyokuwepo, isipokuwa fedha nyingine iliyoongezeka ni arrears za miaka na miezi ya nyuma walizokuwa hawazikusanyi kwa maslahi yao binafsi na wakwepa kodi wengine.