Rais Samia aweka Rekodi Makusanyo ya Kodi 1.9 Trilioni Mwezi Septemba 2021

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWEKA REKODI MAKUSANYO YA KODI 1.9 TRILIONI MWEZI SEPTEMBER

Na, Mwandishi wetu,
Dar es salaam

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa Rais wa kwanza Tanzania kuweka rekodi ya makusanyo ya Tshs. 1.9 trilioni kwa Mwezi September pekee. Taarifa hii ipo kwa usahihi ukipata wasaa wakuona chapisho la mamlaka ya mapato Tanzania juu ya kodi kwa kipindi cha miezi mitatu mfulukizo.

Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni na mamlaka ya mapato (TRA) makusanyo ya Julai mpaka September jumla ya 5.15 trilioni zilikusanya na Mwezi wa September pekee kiasi cha Tshs. 1.9 trilioni kilikusanywa na kuwa rekodi ya aina yake toka awamu zote zilizopita.

Nikumbushe tu kwanini tunampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan rekodi inaonyesha hata watangulizi wake kila mtu aliweka mpango namna ya kukusanya kodi lakini yeye anasisitiza uwazi na kodi iliyo halali kwa serikali. Tujikumbushe watangulizi wake kwenye suala la makusanyo ni kama ifuatavyo;

Hayati Rais Mkapa anaondoka madarakani serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs.322 bilioni kwa Mwezi.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka madarakani serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs 850 Bilioni kwa Mwezi

Na pindi cha Hayati Rais Magufuli anaaga dunia serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs. 1.4 trilioni kwa Mwezi.

Wakati serikali ya Rais Samia imepanga kutumia jumla Tshs 36.33trilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mwaka ulioanza tarehe 01.07.2021 ambapo mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Tshs 26.03 trilioni sawa na 71.7% ya bajeti yote.

Kati ya mapato hayo, mapato ya kodi ni Tshs 22.18 trilioni sawa na 13.5% ya pato la Taifa . Aidha Serikali inalenga kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya Tshs 2.99 trilioni na mapato kutoka vyanzo vya halmashauri ni Tshs 863.8 Bilioni.

Hakika Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kasi yake ya Tshs 1.9 trilioni kwa mwezi mmoja. Ebu vuta picha una Tshs 1.9 trilioni kwa miezi 12 utapata jumla ya Tshs 22.8 trilioni tutavuka lengo kwa 3% naomba mfahamu tangu uhuru hakuna Rais aliwahi kutenga Tshs 36.33 trilion kwa ajili ya bajeti ni Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pekee.

Ili tuendelee kupiga hatua hatuna namna ya kumuunga mkono Mhe. Rais juu ya kuibua vyanzo vipya na kuhamasisha wananchi kuendelea kulipa kodi kwa halali kwa maendeleo ya Taifa lao.

#Twende Pamoja
# KwaMatokeoYaHaraka.

20211006_143110.jpg
 
Tena tumepeleka bila shurutiiii na msg ya asante kwa kulipa on time
 
Unawezaje kulinganisha makusanyo ya kodi ya miaka ya 2000 na 2021 kweli upo seriuos kabisa?

Umeangalia hali ya kiuchumi ya mwaka 2000 na sasa 2021 zinalingana? Vipi kuhusu idadi ya watu wanalingana? Tax payer base ipo sawa? Maendeleo na teknolojia vinalingana? N.k

Sidhani kama ni sawa kumpa mtu credit kwa kigezo cha kulinganisha na watangulizi ambao kimazingira sababu nyiginezo hawako sawa kabisa.

Kama tunataka kuwapima hawa basi tubainishe vigezo kulingana na wakati alafu tuone kwa kila mmoja kwa wakati wake alipaswa kukusanya kiasi gani ndio tujue kama anafanya vizuri au yupo ambaye uongozi wake ulifanya vizuri zaidi. Hapo sasa ndio tutoe credit, nasema hivyo kwa maana kwamba inawezekana kabisa haya matrilioni tuyasikiayo inawezekana kabisa haya yeye bado hajafikia anachostahili kukusanya kwa wakati huu lakini kwa sababu tunasikia ni nyingi ukilinganisha na za hao watangulizi basi tunataka kutoa tu credit.
 
serikali ya mama ikipandusha cheo inalipa hapohapo.


huyu tutamwongezea nae hadi afie ikulu
 
Back
Top Bottom