Watanzania tushindwe wenyewe lol!

Mocrana

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
536
122
VODACOM imetoa namba na ya bure kwa ajili ya kuupigia kura Mlima Kilimanjaro kuwa moja kati ya maajabu saba ya dunia, jinsi ya kupiga kura andika neno KILI au KILIMANJARO, kwenda namba 15771, jamani ni bureeee, mimi nimeshapiga kura mara ya ishirini na naendelea, tufanye hima jamani, pongezi kwa vodacom, IT CAN BE DONE LET US PLAY OUR PART!
 
kwanza tuelimishe kwa sasa tunafaidikaje na uwepo wa mlima kilimanjaro ...afu ndo utushauri tupige kura..
 
kwanza tuelimishe kwa sasa tunafaidikaje na uwepo wa mlima kilimanjaro ...afu ndo utushauri tupige kura..

Ni kweli mkuu maana Kenya wananufaika zaidi kupitia mlima Kilimanjaro kuliko sisi. Na pesa zenyewe zikipatikana zinaishia mikononi mwa mafisi-adi. Yapasa viongozi wetu waonyeshe uzalendo wa kweli na wauambukize kwa raia ndo tutaona maendeleo na faida ya kufanya kitu kwa ajili ya nchi yetu. Otherwise watu tuko demoralized na uongozi uliopo. Wanyama wetu hai wanachukuliwa kwenda Uarabuni, Waarabu wana nchi yao ndani ya nchi yetu. Lol! Inakatisha tamaa kwa kweli.
 
Hiyo promo kafanyie kenya labda watakusikia mi sioni faida yake. Wangesema tupigie ziwa victoria ingekua sawa maana sato nawala
 
Waambie TTB na hao panya wa Wizara ya Maliasili watumie simu zao wapige kura. Mimi sipigi Ng'ooo!!! Shenzy type, nina hasira nao sana.

Barua ya ushiriki wametumiwa mwaka 1997 toka Uswisi, kuna NGO ikataka kufanya promo ikaomba endorsement kwa wizara, masikini wakawa wanapigwa tarehe as if wanaomba mkopo benki. Siupigii kura yangu ng'oooo!!!!!
 
Hata watalii wa dunia nzima wakija bongo, wanaofaidika ni mafisadi wachache. Kwa hiyo huo mlima wacha hata usipopigiwa kura maisha yanakwenda
 
Back
Top Bottom