Watanzania tunashida ya utambuzi. (Lema's incident)

Watanzania tunashida ya utambuzi. (Lema's incident)

Gunner11

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
16,680
Reaction score
31,798
Maybe because of poverty?
Maana huwa tunakosa logic kwenye vitu simple sana.

Inamaana watu mmeshindwa kabisa kuchuja, maneno ya Lema na hali ya kisiasa? Lema ni nani katika siasa? Au kisa ni CHADEMA ndo' awe na autonomy ya kuongea kitu hata kama hakina mashiko basi kizingatiwe?

Yaani chama kinaacha mambo ya msingi, kina anza ku discuss kuhusu mange? Ambaye hata ukiangalia yeye hahusiki kabisa na chama?

Mimi sina chama, wala sio mfatikiaji wa siasa, ila ukweli usemwe watanzania ni kweli kabisa, huwa hatuna consistency ya kujua kinacho endelea.. Yaani mtu anaweza kutupumbaza kwa kutoa punchline ya kijinga ambayo inaweza kufuta kabisa fikra zetu..

Tukaanza kujadili punchline, ambayo kimsingi haina mashiko yoyote.

Hivi ni waulize, kati ya Mange na Lema, nani anayepush mabadiliko?

Mnataka Mange aje auwawe huku na kuteka kama wakina pole pole?

Tena inabidi mkae mkishukuru kuna mtu kama Mange, hakuna kiumbe anayeweza kurisk maisha yake namna ile. Haya maviongozi uchwara ya CHADEMA kama li lema, ndo yalikuwa yana subiri hiki kipindi yaje yavuruge.

Heche and Lisu, ndo watu ambao wako genuine. Ila kama ni wao tu na wachache kati yao ndo wana operate katika misingi bora ya chama, unategemea walio baki wataweza kushinda hongo za mawakala wa kizimkazi?

Lilikuwa swala la muda tu, chama kitachezewa tena, na cycle zile zile zitajirudia.. Kwa sababu watz huwa ni kama wanakosa upepo mbele ya distractions.

Mbowe yuko wapi leo? Si alionekana na Mama? Unahisi ego yake ingemruhusu kubaki na wakina Lissu baada ya kuvuliwa uenyekiti?

Hisia ndo silaha kubwa ya jamii maskini maana huwa lazima atakuwa under survival, wamepita wangapi CHADEMA?

Kwa Hali hii tu sahau any change any time soon. Tutaendelea kuburuzwa maana akili ya kujua na kutofautisha, ujinga na ukweli hatuna.
 
Back
Top Bottom