GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,746
- 109,187
Na hili lazima niliseme ukweli bila kupepesa, kutikisa wala kumung'unya kuwa katika Mawaziri ambao nadhani Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ' amepatia ' katika kumteua ni Waziri wa Viwanda Mheshimiwa Charles Mwijage.
Katika kumfuatilia kwangu kwa marefu na mapana yake yote nimegundua kuwa kwa aina ya uwezo wake mkubwa wa ' kupambanua ' mambo, uzoefu wake na commitment yake kama Watanzania tutamtumia vilivyo nina uhakika muda si mrefu tunaweza kuwafukuza akina Malaysia, Singapore, UAE na hata China katika maendeleo ya Viwanda.
Tuache Siasa zetu za ' maji taka ' tulizonazo na zinazotupotezea muda na tumpe ' ushirikiano ' huyu Waziri wa Viwanda Mheshimiwa Mwijage na kuna siku Tanzania ' tutaheshimika ' Kiviwanda. Na nitoe tu Wito tena kwa Mawaziri wengine kuwa hebu jifunzeni kitu kutoka kwa Waziri Mwijage kwani yeye hazungumzi tu ' blah blah ' bali ' anatenda ' na kuna indicators za kutosha kuwa kwa muda mfupi tu aliokuwa ' madarakani ' Tanzania tumeanza kusogea kwenda huko tunakokutaka katika Tanzania ya Viwanda.
Hongera sana Waziri wa Viwanda Charles Mwijage na nina imani kubwa na Wewe na hakika Tanzania ya Viwanda itakuwa kweli. Kila la kheri.