Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,300
- 33,919
Historia inaonesha vita katika nchi nyingi za Afrika huanzishwa kwa chama kilichoko madarakani kudekezwa na vyombo vya dola na nchi kuwa na mahakama dhaifu.
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda hayakuanzishwa na waliokuwa nje ya serikali bali yalianzishwa na watu waliokuwa wanaendesha serikali.
Wakati chama kilichokuwa madarakani cha Mouvement républicain national pour la démocratie et le développement -MRD kiliporuhusu Jumuiya yake ya vijana (Interahamwe)kuwasakama na baadae kuanza kuwaua wapinzani wa chama hicho, vyombo vya dola na Mahakama walishindwa kusimama upande wa wanaoonewa.
Ajabu ya Mungu hata viongozi wa wa dini nao kitu pekee walichokuwa wanafanya ni kuwaombea viongozi wao eti wawe watu wema. Nchi ikatekwa na muelekeo ukabadilishwa toka kuwa taifa badala yake ikawa ni nchi inayoongozwa kwa makali ya Upanga.
Hapa kwetu inaonekana CCM inaiteka nchi na kulielekeza taifa letu kwenye njia ya Maangamizi. Inaanza kujengeka hisia kwamba ukionewa na CCM hakuna jinsi utaweza kutetewa na chombo chochote cha dola wala mahakama.
Nayajua matukio ya watu kuonewa na watu wa CCM hakuna chombo cha dola wala mahakama vilivyoweza kuwasaidia watu hao. Unaweza kuwaza mtu anawezaje kutishia kumuua Lissu mitandaoni na Polisi wanapoambiwa wachukue hatua wanasema mwenye kuona amekwazwa aende mahakamani kushitaki. Kosa la jinai linaweza kupelekwa mahakamani na raia wa kawaida?
Kuna kila dalili na ushahidi kwamba watu wa CCM sasa wameota mapembe dhidi ya sheria zote za nchi hii. Wao wanaweza kufanya uovu ama jinai na wakaendelea kudunda mitaani.
Kuna kijana mmoja alipigwa kisu cha kifuani na vijana wa CCM anaowajua lakini polisi hawajawahi kuwakamata vijana hao wa CCM ingawa walishapewa majina yao mara tu baada ya tukio.
Watu wasio wana CCM wanajua ni kwa kiasi gani wanavumilia kutokutoa mawazo tofauti na CCM ili biashara zao ama kazi zao zisiharibiwe. CCM inaogopwa si na watu wabaya bali inaogopwa na watu wema wasio upande wao.
Ukiona maoni ya watu wa CCM kuhusu matukio kama ya kupotea kwa Diwani wa Kata ya Kagezi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo, Ben saanane, Tundu Lissu, na wengineo unabaki kuishangaa mioyo waliyo nayo wana CCM.
CCM ni lazima izuiwe kuisambaratisha nchi yetu.