Watanzania tuione hii, inatutesa sisi na watoto wa watoto wetu

StingRay

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
503
628
Wakati mchakato wa kuandaa katiba mpya kila mwananchi wa Tanzania ndani ya moyo wake alikuwa anatamani hivi, "natamani katiba hii imalize matatizo haya yoteeeee..........." halafu Mtanzania huyu anayataja matatizo hayo kwa dhati ya moyo wake.

Lakini............

Kilichotokea ni UKAWA kususuia bunge na kambi ya pili dhidi ya UKAWA ikaendelea kwa madai ya kuandaa katiba ya wananchi.

Ukichunguza kwa unadni wake utaona wanaoendelea na mchakato huo Dodoma, wanadai wanafanya hivyo kwasababu sheria inawaruhusu kufanya hivyo, kisheria na kimantiki ni sawa kabisa kama tu endapo yale yaliyowasilishwa na tume ya Mh. Jaji Warioba yangeendelea kuwa "msingi" wa majadiliano ya kila hatua ya bunge maalumu la katiba.

Mf. Tume iliwasilisha kuwepo kwa serikali tendaji (hizi sio serikali za nchi tu bali ni mfumo-tendaji i.e collaborative governance) ambao kimsingi hata sasa upo na ndio unaofanya kazi kiuhalisia kwa shughuli za kila siku.

Hali halisi: wanaondelea na mchakato wakatiba kinachofuata ni laana ya wananchi wenyewe wa Tanzania kwa bunge maalum lakatiba kwani kwa umoja wao na maono yao walipendelea kuweka historia ya tiers tatu za utendaji kutatua malalamiko yao, ila wamekataliwa. Na kwasasa wanalazimishwa waendele na serikali mbili kwa ahadi kama za maisha bora kwa kila mtanzania, kuwa changamoto zitamalizwa tu. Sipendi kutoa rejea ya wengi lakini hapa nirejee kidogo tu juzi Mh Rais anatoa mchango wake pale Kenya anasema sitanukuu bali natohoa "ugaidi unazalishwa na serikali au taasisi kuminya haki za msingi za makundi fulani"

Swali: Wanaondelea na bunge la katiba Dodoma hawajui hili? Mh Rais wakati akinena haya hakujua hili?
wanakuwa na vichwa vigumu hapa wananikumbusha kitabu cha enzi hizo cha Chinua Achebe "Things Fall Apart".
Nimekumbuka hiki kitabu kwasababu kina fundisho kubwa sana kwa hawa wanaondelea na mchakato wa katiba Dodoma, kwanini?

  1. Okonkwo was demonstrating a "a fear of failure" (wana-CCM hawataki kukubali wameshindwa)
  2. but he ended up failing himself -kifo cha majitaka kabisa........ katiba haitapatikana na fedha zitakuwa zimetumika kwa jambo ambalo silo kabisa,



Ahh, inachosha kila siku tuwapigia kele wao tu Watanzania tufanya maamuzi sahihi sasa bila kuwaachia hawa mwanya wa kuja na lugha nyingine tena.


mengi wana JF wanayo..........................................
 
Back
Top Bottom