jembe afrika
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,602
- 3,781
watanzania sisi ni watu wa kulalamika ila kuthubutu hatuwezi
watanzania sisi ni watu wa kulalamika ila kuthubutu hatuwezi
tukitoka kuandamana tunananyooshewa vidole as if sisi tunaishi rwanda hatustahili kudai haki zetuTumeshajua kuwa sisi ni watu wa kulalamika, nini kimafanyika kuanzia n awewe kubadiliha hii hali? au tuendelee kulalamika kuwa watanzania ni watu wa kulalamika?
watanzania sisi ni watu wa kulalamika ila kuthubutu hatuwezi
Lengo ni kuonyesha kuguswa na suala hili. Tulifanye hili kama ishala kwa watawala watambue wasipokuwa makini lolote laweza kutokea.
= ishara
watanzania tunahitaji kubadilika na kujenga tamaduni mpya! tuna tabia ya kushabikia sana jambo na baadae tunachoka kabla jambo halijafika mwisho wake iwe ni sad or happy ending! wazungu wanaita perseverance yani kukomaa hadi mwisho uone kimeeleweka! katika hili la Escrow tukomae hadi mwisho hadi tuone watu wamerudisha pesa na wamefungwa na huu uwe ndio utamaduni wetu mpya na tuachane na tabia ya kulalamika bila kuchukua hatua jambo ya kupaza sauti kukataa ujambazi huu wa wazi wazi wa majangili haya. tukijijengea utamaduni huu mpya watawala wataacha kuiba manake kwasasa tunajua watafanya jitihada kubwa kuizima hii Escrow na kama kawaida wataibua issue ingine kubwa ili watuhamishe kwenye mada ya Escrow na wanaweza kudelay mchakato mzima hadi pale wataona wadanganyika tumechoka kufuatilia tumerudi kukamata majembe ya mkono kuitikia wimbo wa kilimo kwanza basi nao watapumua na kurelax kwa kwenda Dubai kula bata kwa mabilioni waliyowaibia wanyonge wa Danganyika! Mungu tubariki vijana wa sasa tunaochukia wizi wa mali zetu za umma! Aisee jamaa wamevuka mipaka , yaani hata aibu hawana tena wanagawana pesa za watanzania kupitia benki ya Kitanzania? hii ni too much! hawa hawamjui Mungu tena ni washkaji zake shetani!
Ninaomba kutoa ushauri wangu kwa watz wenzangu juu ya sakata/kashfa inayohusiana na Tegeta escrow. Kwa sehemu lilipofikia suala hili linahitaji si tu nguvu ya Bunge bali hata nguvu ya wananchi. Wananchi tuonyeshe HISIA zetu kwa kukerwa na jambo hili. Kwa wenzetu mliopo Dodoma kusanyikeni nje ya ukumbi wa bunge kwa muda wote wa bunge siku ya jumatano.
Sie tulio nje ya Dodoma tujitahidi kuwa makundi makundi kwa kadri ya maeneo husika tukifuatilia shughuli za bunge siku ya jumatano.
Lengo ni kuonyesha kuguswa na suala hili. Tulifanye hili kama ishala kwa watawala watambue wasipokuwa makini lolote laweza kutokea.