Sisemi mimi kama Chereko bali nachereka na maneno ya Waziri Kapuya kama nilivyosoma kwenye habari Leo jumamosi iliyopita -eti Watanzania sio waaminifu na hawajui kiingereza ndio maana kwenye mahoteli wafanyakazi wageni wamezidi. Je huyu ni Profesa na Waziri anayefaa kushughulikia mambo ya ajira nchini kwake? Kama kitengo chake cha kuhakiki kazi kwa wageni kimeshindwa kazi abainishe wazi!
1. Kujua kiingereza sio kujua kazi - kule ufaransa mahotelini wafanyakazi wengi tu hawajui kiingereza - sio huko tu, China, Ubelgiji, Urusi, Hispania, Italia, Brazil yale maneno "huyu anaongea kiingereza kigumu" ni jambo la kawaida. Wapo rafiki zangu walienda mji mmoja unaitwa Nice, siku ya kwanza hawakula chakula hotelini kwa kukosa mkalimani wa kiingereza. Kama huduma bora ni lugha, huduma bora hapo ulaya iko wapi?
2. Profesa si ametembea? Wengi wetu pia tumetembea, je si ni hoteli nyingi tu kubwa duniani hukuti mtu wa kukupokea mlangoni?. Hapa kwetu nenda movenpick, kempinski, New Africa, Southern Sun utapokelewa mlangoni vipi leo Waziri anasema "Watanzania wakiona mgeni wanababaika"!!! Si hoteli nyingi tu huku nje wakikuona ni mtu mweusi wanakudharau? Je hao wafanyakazi wa kigeni kazi yao ni kupokea wageni? Hiyo kazi si wanafanya watanzania kwa kuwa ni kazi isiyo na heshima?
3. Mahotelini kote kuna ziada ya wafanyakazi wa kigeni ambao kazi zao zingeweza kufanywa na watanzania, wanalipwa mishahara minono huku wakilipiwa nyumba, watoto wao wanasomeshwa kwa gharama za hoteli, Waziri haoni kuwa hii inapunguza mapato na hivyo kupunguza kodi ambayo ingelipwa serikalini? Idadi hii kubwa inasababisha gharama za uendeshaji wa hoteli kuwa kubwa hivyo bei kuwa kubwa jambo ambalo linasababisha wageni kuona hoteli zetu ni ghali hivyo kuathiri idadi ya watalii waingiao nchini.
4. Kwa kuwa wageni hao wanakuwa wakali kwa wafanyakazi raia wa Tanzania na wengi wao ni wabaguzi wa rangi, wafanyakazi wa ngazi za chini wanaolipwa kiduchu wanakuwa na hasira katika kazi ndio maana wanaweza kuonekana kutopenda kazi zao na kuathiri utendaji wao. Sambamba na pendekezo la Waziri kwa VETA kuweka mtaala fulani kwenye elimu ya mambo ya hoteli, ipo haja ya kutoa tahadhari kali kwa wafanyakazi wageni kabla ya kupewa kibali cha kazi nchini kuwa Tanzania sio nchi ya ubaguzi wa rangi.
5. Ni ukweli pia kwamba kuna wafanyakazi wengi wageni wapo nchini kwenye mahoteli hawana elimu inayokidhi au kufanana na ajira zao - kwa mfano nasikia pale Kempinski yupo mjerumani ambaye hana cheti chochote cha maana na analipwa pesa kibao pamoja na kuwa ni mbaguzi sana wa rangi. Watu kama hawa wapo wengi sana malipo ya mgeni mmoja tu yangeweza kuwa mshahara wa wafanyakazi wengi tu kwa watanzania au mishahara mizuri wangeweza kupatiwa watanzania kadhaa badala yake. Mheshimiwa Waziri usisahau ahadi ya Serikali ya kutengeneza ajira milioni moja!
Haya Mheshimiwa Waziri tumekutonya tuone basi kama wadhifa wako unautumia ipasavyo, kazi kwako. Tafadhali upate ripoti kwenye mahoteli yote makubwa, watu wangapi ni wageni, wana elimu gani, wanalipwa nini na wanafanya kazi gani. Ukipata nafasi utembee ukaongee nao usikie malalamiko yao badala ya kukaa ofisini ukingoja ripoti. Wewe ni Professa.
Chereko anapenda kuchereka hivyo tucherekeshe basi Mh. Waziri, au kwa lugha nyingine tupe raha Watanzania badala ya kututia huzuni. Samahani kama ukweli huu haukuupokea vema.
Watanzania ni marafiki, wanapenda wageni na wanaipenda lugha yao ya Kiswahili - tabasamu sio lazima kujua kiingereza, tabasamu halina lugha.