Watanzania ni wepesi kuibwa akili sana

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,487
5,111
Tanzania bwana ni hatari
Watu wote washasahau habari ya budget wamehamia kwenye simu fake
Chaajabu ni kwamba simu fake kibao zinadunda hazijafungwa tatizo ninini? Au mtambo wa kuzimia nao ni fake?

Au hii ilisukwa makusudi ili watz wasahau habari ya budget ili wazee wa ndio waipitishe kirahisi?

Kwann akili zetu zinageuzwageuzwa kama chapati? Au akili zetu nazo ni fake maana zinasahau vitu vya msingi zinakimbilia upupu

Issue ya sukari ambayo ni tatizo mpaka leo tumeisahau na tumeipotezea kwa igizo dogo tuu la dakika 2 (bialism and kitwangalism in bungelism)
Igizo hilo fupi sana likahamisha akili zetu tukasahau shida ya sukari na issue ya lugumi,

Leo tamthilia ya simu fake ambayo ililtangazwa kwa mda mrefu imekuja kivingine imetuhamisha hakili tumesahau swala la budget ambalo ni muhimu kuliko hii tamthilia ya simu fake

Pindi tamthilia hii itakapofika ze end tayari budget ishapitishwa kiulainiiii
Ndipo tutashtuka na kuanza kutapatapa bila msaada

Kuna haja ya kuzima hizi hakili fake zetu watanzania ili tubaki na hakili original

Vinginevyo yawezekana hata nchi yetu ni fake.

Hiyo ni ndoto yangu ya mkesha wa simu fake
 
simu fake ikoje ..hakuna simu fake ila kwa kuwa wenye nazo wanataka soko lao liwe la uhakika lazima wawakandamize wanaoibukia ktk kutengeneza sim za bei rahisi
 
Tanzania bwana ni hatari
Watu wote washasahau habari ya budget wamehamia kwenye simu fake
Chaajabu ni kwamba simu fake kibao zinadunda hazijafungwa tatizo ninini? Au mtambo wa kuzimia nao ni fake?

Au hii ilisukwa makusudi ili watz wasahau habari ya budget ili wazee wa ndio waipitishe kirahisi?

Kwann akili zetu zinageuzwageuzwa kama chapati? Au akili zetu nazo ni fake maana zinasahau vitu vya msingi zinakimbilia upupu

Issue ya sukari ambayo ni tatizo mpaka leo tumeisahau na tumeipotezea kwa igizo dogo tuu la dakika 2 (bialism and kitwangalism in bungelism)
Igizo hilo fupi sana likahamisha akili zetu tukasahau shida ya sukari na issue ya lugumi,

Leo tamthilia ya simu fake ambayo ililtangazwa kwa mda mrefu imekuja kivingine imetuhamisha hakili tumesahau swala la budget ambalo ni muhimu kuliko hii tamthilia ya simu fake

Pindi tamthilia hii itakapofika ze end tayari budget ishapitishwa kiulainiiii
Ndipo tutashtuka na kuanza kutapatapa bila msaada

Kuna haja ya kuzima hizi hakili fake zetu watanzania ili tubaki na hakili original

Vinginevyo yawezekana hata nchi yetu ni fake.

Hiyo ni ndoto yangu ya mkesha wa simu fake
Hilo linaeleweka kuwa tunayumbishwa kirahisi. jamaa wanacreate diversions mara kwa mara ili wafanye mambo yao. lakini kwa hili la bajeti inayojadiliwa bungeni sioni mahusiano yake. Wabunge wanajadili na wananchi hatuna sauti kule tofauti na hao tuliowatuma kule ili wawe sauti zetu. kama wameamua kupitisha, sisi huku hatuna namna ya kuzuia, iwe kwa simu feki, makalio feki au whatever. After all, ulitegemea KWELI kuwe na tatizo kwenye upitishaji wa bajeti? Labda tuongelee sukari na si bajeti maan utaratibu wake upo hivyo miaka yote, ni wa kuunga mkono mia kwa mia hata kama muungaji mkono amesinzia muda huo.

Kwa kuwa umekazania sana suala la bajeti, naomba msaada wa ushauri hapa. kama pasingekuwepo mjadala wa simu feki, wananchi huku kwetu mitaani tungewezaje kuizuia hiyo bajeti isipite? Kwa kuandamana? kwa kufunga na kuomba? Au kwa kutambika mizimu? The way I see it, we simply have no role to play! Wacha wapitishe tu kama ilivyo ada.
 
Tuondolee akili mgando hapa, ebho! Wewe unataka tugande akili kwenye jambo moja tuuu mpaka kiama! Akili za binadamu timamu ziko dynamic na multi_ functional, zina uwezo wa ku-compartmentalize mambo chungu mzima at a time na kuanza kuya-process kulingana na mazingira yaliyopo na vipaumbele vya mhusika. Kwani hii imekuwa north korea ambako Kim Jongun akisema piga makofi taifa zima linapiga makofi mpaka akumbuke kusema sasa kalaleni!!! watu tuna vipaumbele tofauti tofauti, usitake kutuimbisha kwaya za kikomunisti, kwanza baadhi yetu hatujui maana ya bajeti na au hatuoni kama tuna uwezo wa kubadilisha chochote na isitoshe tuna wawakilishi wetu mahsusi bungeni wa kufanya kazi hiyo, wakishindwa tutawasubiri kwenye sanduku kura!
 
Tanzania bwana ni hatari
Watu wote washasahau habari ya budget wamehamia kwenye simu fake
Chaajabu ni kwamba simu fake kibao zinadunda hazijafungwa tatizo ninini? Au mtambo wa kuzimia nao ni fake?

Au hii ilisukwa makusudi ili watz wasahau habari ya budget ili wazee wa ndio waipitishe kirahisi?

Kwann akili zetu zinageuzwageuzwa kama chapati? Au akili zetu nazo ni fake maana zinasahau vitu vya msingi zinakimbilia upupu

Issue ya sukari ambayo ni tatizo mpaka leo tumeisahau na tumeipotezea kwa igizo dogo tuu la dakika 2 (bialism and kitwangalism in bungelism)
Igizo hilo fupi sana likahamisha akili zetu tukasahau shida ya sukari na issue ya lugumi,

Leo tamthilia ya simu fake ambayo ililtangazwa kwa mda mrefu imekuja kivingine imetuhamisha hakili tumesahau swala la budget ambalo ni muhimu kuliko hii tamthilia ya simu fake

Pindi tamthilia hii itakapofika ze end tayari budget ishapitishwa kiulainiiii
Ndipo tutashtuka na kuanza kutapatapa bila msaada

Kuna haja ya kuzima hizi hakili fake zetu watanzania ili tubaki na hakili original

Vinginevyo yawezekana hata nchi yetu ni fake.

Hiyo ni ndoto yangu ya mkesha wa simu fake
Mtu mwenye NJAA ni rahisi kupelekwa kama boya. Akiambiwa huku kuna wali atakimbilia kule akale ashibe kesho tena akiambiwa ugali upo mtaa ule basi mbio, Ndio maisha ya mwenye nyaa. Dawa yake sio kumlaumu bali kumpa shibe ya uhakika (akilini) atatulia na kupambanua maisha yake ya mbeleni.
 
Kajipange vyema ukitaka kutukana watu,maana kijijini kwenu watu waliacha kununua redio kwa kutegemea mchina zenye muziki mkubwa!
 
Mtu mwenye NJAA ni rahisi kupelekwa kama boya. Akiambiwa huku kuna wali atakimbilia kule akale ashibe kesho tena akiambiwa ugali upo mtaa ule basi mbio, Ndio maisha ya mwenye nyaa. Dawa yake sio kumlaumu bali kumpa shibe ya uhakika (akilini) atatulia na kupambanua maisha yake ya mbeleni.
Mleta mada bado hajasema hao wananchi anaowazungumzia alitaka wahusike vipi na mjadala wa bajeti...
 
Vyote vina umuhimu wake na wakati wake ila mfano bajeti iko juu ya uwezo watu sisi wananchi, wale ambao wangeijadili hii bajeti ni wabunge wa upinzani na wa chama tawala
 
Kwanza Unaishi Dar,halai wewe unaakili Feki IME yako ya Ubongo imekuwa edited.
Issue ya Sim fake sio ya leo,ni issue ya muda mrefu saana na inajuliakana.

Na suala la Budget ni suala binafsi,sio kila mtu anapenda mambo ya Siasa,wengine wanapiga zao hela hata Budget hawaijui ndio nini
.

Kulemaa kwako na akili ya kisiasa usone wote hawana akili,kuna watu humu wanapiga hela kwenye biashara zao hata ukimuuliza Waziri wa Vijana hamjui.Sasa suifanye ujumla namna hiyo.

Wanaohusika na masuala ya Budget wanaendelea na ya kwao,Hivi Budget na kupata msiba wa kufiwa na mtu kipi kinaumiza zaidi?Mtu anafiwa na baba yake mzazi na bado kama ni mfuatiliaji anaendelea kufuatili,itakuwa hili la simu fake?
 
Ukawa mwaka huu mtadandia kila kitu, nyie endeeleni kususia vikao vya bunge tu mkifikiri wananchi watawaunga mkono ....hapa kazi tuu
 
Back
Top Bottom